Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Kama jamii inayojitambua; kwa kweli, tulitaka kuweka misingi imara na bora kupitia katiba mpya, lakini tulisahau kwamba la kuvunda halina ubani.
Na ukiniuliza mimi kwa sauti ya ukali kuwa sasa kumbe tunasubiri nini?
Nitakujibu kwa upole kwamba; tunasubiri mambo yajitibu yenyewe kupitia kanuni mduara ya asili.
Hebu nitoe mfano kidogo pengine nitaeleweka.
Iwapo wanadamu hawaweki sheria au kanuni za kuhifadhi mazingira hali hii moja kwa moja itapelekea majanga makuu yatakayowaondoa hao walioshindwa uhifadhi juu ya uso wa dunia! Na pindi hilo likitokea;
Ndipo hapo tena mazingira hayo-hayo huianza safari ya kuirudia hali yake nzuri ya awali.
Cha msingi hapo ni sisi kuchagua, kati ya kujitibu wenyewe au kusubiri mambo yajitibu yenyewe!
Ingawa siku zote kusubiri mambo yajitibu yenyewe tatizo lake huwa ni ukubwa wa gharama!