Hakuna mwanasiasa wa CCM fisadi?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Awamu ya tano ilijinasibu kuwa inapambana na ufisadi lakini kati ya watu waliokamatwa na kufikishwa mahakamani na mchakato wa kesi ukaendelea hakuna mwanachama maarufu au kigogo wa ccm bali wengi ni wafanyabiashara na watumishi wa umma.

Lakini historia inaonyesha kwamba dili zote zilizopangwa na zinazoendelea kupangwa zinawahusisha moja kwa moja wanasiasa wa chama tawala. Baadhi ya taarifa zilizotolewa kuhusu wizi wa Mali za umma Kama Richmond na escrow walitajwa wanasiasa kwa majina yao lakini hadi leo hawakukamatwa si kwa uhujumu uchumi wala kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Ningependa kuuliza, ukiwa CCM na ukawamtiifu kwa chama upaswi kushtakiwa? Au ni vigezo gani utumika kuwaweka watumishi wa umma years and years kwa uhujumu uchumi wakati uchunguzi ukiendelea lakini vigezo hivyo haviwezi kutumika kuwaweka ndani wanasiasa wakati uchunguzi unaendelea.

Tanzania Kuna vita ya ufisadi au tunavita ya chama tawala against makundi yasiyo wanachama wa chama hicho?
 
Mnaweza kuiba watu kumi ,ila kila mmoja atatiwa hatiani kwa uhusika wake,unaweza ukala mgao na usibanwe,ngoma ni kwa yule alieidhinisha pesa na aliepokea akijua si fedha halali,ndio maana unaona watumishi wa serikali na wafanyabiashara ndio wanaouhusika moja kwa moja.

Mwanasiasa hakuna sehemu utakuta amehusika moja kwa moja katika kuinyofoa pesa serikalini,bali yeye hula mgao ili kumnyamazisha,na ndio maana unaona sakata nyingi zinawakosa,hata hivyo account zao na ukwasi usio na maelezo hua freezed kimyakimya ,ukiwapeleka mahakamani watakusumbua tu
 
Swali lako zuri sana, ukitaka kupata jibu ingia upinzani na kiduka cha mtaji mil.20 uone majibu yake. Hapo ndipo utajua huku ni Tanzania halafu kule ni ccm
 
Ukiona kina Rugemalira na Seth wako ndani jua mafisadi walioshiriki nao wako mtaani wanadunda na ni wasafi kwelikweli...
 
Nani aliuza nyumba za serikali na nyingine kujigaia yeye pamoja na ndugu na washkaji zake? Huyu siyo fisadi?
 
Back
Top Bottom