Hakuna mwanasiasa asiyejipendelea hata Tundu Lissu na Zitto waliwapendelea dada zao Ubunge Viti Maalum!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
39,967
2,000
Tunakumbushana tu.

Tundu Lissu alikuwa na dada yake Bungeni

Zitto Kabwe alikuwa na dada yake Bungeni.

Dkt. Slaa alikuwa na mtalaka wake Bungeni

Ndesamburo alikuwa na mwanae pamoja na mkwewe bungeni

Mbatia alimpeleka dada yake bunge la Afrika Mashariki nk nk

Kila jambo na wakati wake, awamu ya tatu kabila fulani kule Kaskazini lilifaidika sana walijimilikisha TRA eti wanajua sana hesabu na uhasibu.

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
 

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,091
2,000
Bila kusahau JPM alivyojaza ndugu zake kwenye nafasi nyeti serikalini!
Nways kwa lugha nyingine ni kwamba unakiri kuwa miradi inayoendelea Chato ni ya upendeleo!Hatimaye mnakuja kukiri ukweli kama mnavyouona ila mnasema hata akina fulani wana upendeleo!
 

Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
2,191
2,000
Acha kutaka kuhalalisha uovu wenye maslahi kwao kwa rejea ya maovu ya kufikirika,je unaowazungumzia walikuwa na sifa au laa,je upendeleo upo katika muktadha gani.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,035
2,000
Kama unajua kuwa una akili fupi fupi siyo vyema kuanzisha uzi hapa JF.Unaelewa kuwa two wrongs can't make a right?Tundu Lissu,Zitto Kabwe,e.t.c kujipendelea haiwezi kuhalalisha au kufanya kujipendelea kuwa ni jambo sahihi au jambo jema!
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,596
2,000
Unaweza ukawa sahihi lakini kama Wamarekani walivyosema baada ya kunyongwa sadam Hussein huku akidhihakiwa walisema "we could have done it in more better way".

Viti maalum kwa Chadema kama nina kumbukumbu vizuri kuna wakati waliajiri consultant "Kitila Mkumbo"kw aajili ya kutafuta namna bora ya kuteua viti maalum.Hilo pekee linakuonyesha ya kuwa angalau walikuwa na "nia njema ya kutenda haki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom