Hakuna mwanasiasa anazungumzia tatizo la ajira Tanzania, wengi wamejikita kutoa misaada ya matundu ya vyoo na taulo za kike

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,566
Siyo CCM wala Upinzani hakuna mwanasiasa anayezungumzia tatizo kubwa la ajira linaloikabili nchi yetu.

Wanasiasa wengi wamejikita kwenye kutoa misaada myepesi kwa wananchi kama vile kujenga matundu ya vyoo na kugawia watoto wa kike taulo.

Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka, serikali iwe makini.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hahahahahah mtoa maada na yeye inaonekana Hana ajira

Hata Mimi Kuna kipindi nilikuwa naumia Sana kabla sijapambana kuipata nikawa nakuja kutoa lawama daily hapa na kipindi hiko nilikuwa mfuasi wa JPM ila now Ni kama vile nimewasahau ambao hawana. Komaeni kitaa bajeti bado ndogo Ila pesa ikipatikana taratibu zitatoka..
 
Watu wanahangaika ku- improve maisha yao kupitia mahitaji ya wengine.

Wapo huko kwasasa kuimarisha uaminifu na uwajibikaji "WENYE TIJA KWAO"
 
Ni kweli ,ukitaka kujua hilo ona musukuma alivyotetea kuhusu kuhamishwa kwa machinga alivyoshambuliwa na chadema pamoja na ccm kwa ujumla.
 
Changamoto ya ajira utaiongelea wapi?.Kuvaa tu tishet ya tume huru au katiba mpya ni kosa la jinai.hiyo ajira utaiongelea wapi wakati liko wazi kua tatizo la ajira nchini nimatokeo ya sera mbovu ya ccm na serikali yake.Ata hivyo usifikiri utatuzii wa tatizo la ajira ni jambo jepesi lakupiga propaganda kama hilo la vyoo uliloliongelea hapo juu ambalo utatuzi wake ni kukusanya pesa na kujenga.Ajira ni jambo kubwa sana kuliko unavyofikiria kuanzia sera ya uchumi,elimu na mambo mengine.
 
Ni kweli ,ukitaka kujua hilo ona musukuma alivyotetea kuhusu kuhamishwa kwa machinga alivyoshambuliwa na chadema pamoja na ccm kwa ujumla.
Chadema wamemshambulia wapi msukuma au unaweweseka kutaka kuhamisha magoli.
 
Siyo CCM wala Upinzani hakuna mwanasiasa anayezungumzia tatizo kubwa la ajira linaloikabili nchi yetu.

Wanasiasa wengi wamejikita kwenye kutoa misaada myepesi kwa wananchi kama vile kujenga matundu ya vyoo na kugawia watoto wa kike taulo.

Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka, serikali iwe makini.

Maendeleo hayana vyama!

yeye mwenyewe kaajiliwa na kulipwa mshara aje kukwambia ajira tamu ni siasa
 
Siyo CCM wala Upinzani hakuna mwanasiasa anayezungumzia tatizo kubwa la ajira linaloikabili nchi yetu.

Wanasiasa wengi wamejikita kwenye kutoa misaada myepesi kwa wananchi kama vile kujenga matundu ya vyoo na kugawia watoto wa kike taulo.

Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka, serikali iwe makini.

Maendeleo hayana vyama!
Wamesema MJIAJIRI sasa unataka AJIRA GANI
 
Alafu wanavyokabidhi vyoo wanakuja na waandishi wa habari na wabunge na mawaziri wanakata utepe, aibu hii.. yan tunafanya mambo yaliyofanywa na wenzetu miaka ya 1920
 
Bwashee hongera kwa kumeza dawa zako leo. Dishi limetulia utadhani wa UFIPA!!! 😂😂😂

Siyo CCM wala Upinzani hakuna mwanasiasa anayezungumzia tatizo kubwa la ajira linaloikabili nchi yetu.

Wanasiasa wengi wamejikita kwenye kutoa misaada myepesi kwa wananchi kama vile kujenga matundu ya vyoo na kugawia watoto wa kike taulo.

Tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka, serikali iwe makini.

Maendeleo hayana vyama!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom