Hakuna Mvua, njaa imeingia. Umesema serikali haina Shamba! Huu ni mtihani, Mungu hajaribiwi

6c3e68cfef86e55099f9acf6ed9a86b8.jpg
sijui itakuwaje, maana jua linawaka, tingatina tuangalie na sisi?
 
Yatupasa tuombe tu rehema kwa Mungu,yawezekana kuna sehemu tumekosea au hata hatujakosea lakini Mungu kaamua tu kutujaribu ili tuuone ukuu wake,maana sie wanadamu tuliumbwa na tukapewa akili na pia kumbukumbu. Mbaya zaidi tulipewa kitu kinaitwa KUSAHAU,saa zingine tunapofanikiwa au Mungu anpotubariki na baraka zikatujalia,sie wanadamu huwa tumsahau Mungu. Yamkini,tumepewa baraka na Mungu ,tujisahau hadi tukamsahau yeye alietupa hizo baraka. Mungu kaamua kuchapa tu vijibakora na si bakora ukweli hizi...bado ni rasharasha,sasa ni wakati wa kuomba rehema,tuachane na majivuno ya kufikiria kama tulishayavuka majaribu,kana kwamba hatujaribiwi!!! Sisi ni wanadamu,majaribu kwetu ni kawaida ili tuuone ukuu wa Mungu!
Huu si wakati wa kulaumiana,si watawala na si watawaliwa,huu ni wakati wa kuomba rehema na naamini Mungu ni mwingi wa rehema hili nalo tutalivuka na tutavuka salama.
Hili ni jaribu kwa utawala wa awamu ya TANO,sio siri na wala haiitaji PHD kulijua hilo, tupige magoti kumuomba Mungu atuvushe salama. Tusimchokoze kwa kauli za kumjaribu,narudia tena,Mungu ni mwingi wa rehema ila hajaribiwi.

Mungu bariki watanzania wote,tusame pale tulipokukosea, shusha baraka zitokazo kwako,tunaona hili balaa likitunyemelea la njaa,wewe u bab na tunaamini kupitia kwako hakuna kishindikanacho,Mungu shusha mvua ya kutosha,mazao yakamee mashariki,magharibi,kusini na kaskazini. Hakuna mtanzania hata mmoja atakufa kwa njaa tukiamini kupitia wewe.
Ameeen.
Mkuu huu ushauri unatakiwa umpe " yule' aliyesema hajaribiwi. Ndo anajaribiwia sasa na àliye juu yake na tumuone.
 
Lenyewe linabughia na kushindilia ugali wa bure had linavimbiwa had inamsababisha aropokeropoke nakuleta mizaha Kwa wahanga.

lingelazwa njaa japo masaa manne tu lingekuwa Na lugha ya staha
 
Me nimesikia waziri mkuu akiwa abatembea na kukagua Ghala la chakula,,
1. Iweje serikali ina sehemu za kuhifadhia chakula ili hali serikali haina shamba??????
 
Bora nchi angepewa diamond, maana serikali hii mkoa utakao kumbwa na bara la njaa itakua ni Kama Yale yale kagera ya tetemeko.........na serikali inaweza piga hela na ikasepa
 
Bora nchi angepewa diamond, maana serikali hii mkoa utakao kumbwa na bara la njaa itakua ni Kama Yale yale kagera ya tetemeko.........na serikali inaweza piga hela na ikasepa
nchi apewe nani...? sio bure we in kijana wa Mulugo.............
 
Habari za muda wakuu,

Kama tunavyojua Mkuu Mtukufu sana amesema hakuna chakula cha msaada na kwamba Serikali haina Shamba,

Watu waende mashambani wakalime. Naona ni kama Mungu anaamua kumpa mtihani mkuu wa nchi maana mpaka muda huu tunaoongea maeneo mengi nchini hayana kabisa mvua au wanapata za rasha rasha .

Hii ni ishara kwamba Mwaka huu kutakuwa na njaa isiyo na mfano. Sasa sijuwi tutakwenda wapi jamani na tumeshaambiwa hakuna msaada wa chakula.

Mh. Rais tunaomba ubadili maamuzi yako uweze kutusaidia hali ni mbaya sana kwa sasa Gunia la mahindi ni Laki moja na elfu Thelathini na hakuna dalili ya kupata mvua za kutosha mwaka huu.
Twafaaaaa.
Usisahau ROZARI ilimsaidia kupita uchaguzi.
ROZARI hiyo hiyo italeta Mvua!!!!
 
Kumbe wasukuma sio wakarimu kama nlivokuwa nawachukulia siku za nyuma , maana mjomba mergu ni mfano tosha.
 
Nafikiri wale ndugu zangu wa vijijini ndio wanalalamika sana njaa na ndio walio mpa mkuu kura, sasa hakuna msaada wa chakula waende wakalime mahindi yanayokomaa masaa 72.
anyway acha wasome XL
 
Habari za muda wakuu,

Kama tunavyojua Mkuu Mtukufu sana amesema hakuna chakula cha msaada na kwamba Serikali haina Shamba,

Watu waende mashambani wakalime. Naona ni kama Mungu anaamua kumpa mtihani mkuu wa nchi maana mpaka muda huu tunaoongea maeneo mengi nchini hayana kabisa mvua au wanapata za rasha rasha .

Hii ni ishara kwamba Mwaka huu kutakuwa na njaa isiyo na mfano. Sasa sijuwi tutakwenda wapi jamani na tumeshaambiwa hakuna msaada wa chakula.

Mh. Rais tunaomba ubadili maamuzi yako uweze kutusaidia hali ni mbaya sana kwa sasa Gunia la mahindi ni Laki moja na elfu Thelathini na hakuna dalili ya kupata mvua za kutosha mwaka huu.
Twafaaaaa.
mbona mikoani inanyesha:uku kanda ya kati inanyesha,na jana imenyesha hapa meatu wakati naangalia nyanya zangu hapa pembezoni mwa mto mwanhuzi!
labda nikuulize:wewe uko wapi?
usije ukawa una lalamika humu wakati ulipo mvua inanyesha uku unaleta stori za kusadikika!
 
Kila mtu aubebe mzigo wake
kweli bwna, watu wana kaa wanafikiri kuwa JPJM atatatua matatizo eti kwa sababu aiahidi. Watu wapunguze jazba na matumaini maana vipaumbele vya mheshimiwa sana na sirikali yake vinaweza kubadilika kulingana na jinsi anavyotaka. Yeye ni raisi na hakuna mwingine!
 
Mungu ameamua kutupiga fimbo ya njaa kwa ujinga wetu wa kuichagua CCM na bado kama tutaendelea kuichagua tena ataleta gharika ya maji,mpaka tupate akili ya kuikimbia CCM.
 
haya Mr MAVI
Sorry kama umenielewa tofautisha: hadi leo mfumuko Wa bei unga ni 1500kg1 na kitengo cha maafa kilichopo chini ya ofisi ya Wazir Mkuu imesitisha kutoa vibara vya kununua Mahindi kwenye maghara ya Chakula yaliopo nchini chini ya (NFRA). Na leo waziri Mkuu kaenda kukagua maghara hayo ya chakula jijini Dar es saalam chang'ombe na kusema hamna kibari kutoka hadi bei elekezi itakapo toka. Na kama tunavyoelewa kula ni razima na nchi aina Shamba.
 
Back
Top Bottom