Hakuna mtu mwenye akili timamu duniani ambaye atapinga au kuzuia Katiba ya nchi kuboreshwa, kwa sababu huwezi ukaboresha Katiba ikawa mbaya zaidi

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Labda watu hawaelewi maana ya Katiba au umuhimu wa Katiba ya nchi, au Katiba ya nchi ni kwa ajili ya nini na nani.

Lakini hakuna mtu duniani, kama ana akili timamu, atazuia wazo la kuboreshwa kwa Katiba ya nchi. Mtu anaefanya hivyo ni mwendawazimu, au hajui kazi ya Katiba ni nini, au utaratibu wa kuboresha Katiba ukoje. Na ukiona kuna watu wendawazimu wachache wanapinga Katiba ya nchi kuboreshwa au kufanyiwa mabadiliko ya msingi, basi ujue hiyo nchi haina usawa kuna watu wachache wanafaidika na Katiba iliyopo.

Hivi ukiwa na akili timamu, kwa nini ugombane na watu wanaotaka kujadili kuboresha Katiba kabla hata hujasikia wanataka mabadiliko gani ya Katiba? Una akili kweli wewe? Hivi unategemea watapendekeza tufanye mabadiliko ya Katiba Raisi wa Tanzania atoke Rwanda? Au kila Raisi akiingia awamu ya pili tumuue?

Sijawahi kuona Katiba ya nchi imeboreshwa na matokeao ikawa ni kuwakandamiza watu au kikundi fulani, ikiwa mabadiliko yalifanywa kwa uwazi na kidemokrasia. Acha watu wajadili mabadiliko, waseme wanataka nini.

Kwa mfano, ikiwa tutaboresha Katiba ili dhamana iwe haki ya Mtanzania yeyote bila kujali amefanya kosa gani, na itolewe siku yeyote ya wiki, kuna ubaya gani?

Au kwa mfano, tukisema tuboreshe Katiba kuwe na wagombea wa Ubunge wasio na vyama, kuna ubaya gani?

Au tukisema tubadilishe Katiba, tusiwe na wakuu mikoa au wilaya bali Wakurugenzi wa mkoa au wilaya watakao teuliwa au kuomba kazi kwa sifa za kitaaluma badala ya sifa za kisiasa, kuna ubaya gani?

Hivi Watanzania tukoje tunagombana kwa ajili ya vitu kama Katiba? Kwa nini serikali inafanya makusudi kupotosha umma ili waone suala la mabadiliko ya Katiba ni la Chadema na sio la Watanzania?

Kama suluhisho la kukata mzizi wa fitina, mie napendekeza kwamba tufanye Referendum basi, kila Mtanzania aulizwe ikiwa tunahitaji kufanya mabadiliko ya Katiba au la, ili ijulikane kama kweli hili ni jambo la Chadema au Watanzania kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom