Hakuna mtu anayependa kuishi Uswahilini. Hata sisi Waswahili tunatafuta nyumba na viwanja mbali na Uswahili

Kwangu uswahilini ni sehemu yeyote yenye makazi yasiyopimwa!! Sehemu ambayo haijapimwa imekaa hovyo hovyo unaweka dirisha lipo karibu na choo cha mtu au hakuna njia ya kuingia gari,hao wetu wenye mageti uswahili ni wale wenye kipato wamewavua watu viwanja vya pembeni yao ili kujivinjari.
 
Lakin semeni yote jamani uswahilini kuna raha yake, tukianza kuzitaja burudani zinazopatikana uswazi tutajaza nyuzi nyingi sana
 
Uswahilini mnakokukimbia ni wapi? Inawezekekana mnakimbia kushirikiana jiko, choo na bafu kwanye nyumba ya kupanga lakini hata Manzese, Mbagala, Mwananyamala kwa Kopa Kinondoni Shamba kuna nyumba self contained na gate kabisa mlangoni, ukiingia na gari yako hakuna mtu anaejua maisha yako.

Nifundisheni huu uzungu unaofanya mkimbie Uswahilini. Huko Uzunguni kuna nini cha ziada? Au oxygen wanauovuta ni tofauti na hii ya kwetu?

Uzungu na Uswahili unaubeba mwenyewe na jifunze jinsi ya kuishi na watu wanaokuzunguka
Sky Eclat kama unaweza kuwaepusha watoto wako na maisha ya uswahilini, please fanya hivyo ndugu yangu.

Mimi nilikulia uswahilini kabla ya wazazi kuhamisha makazi mapya pahala pengine.

Asilimia 70 ya ambao nilisoma nao shule ya msingi katika mtaa ule kwa sasa ni mateja na walevi wa kutupwa.
 
Back
Top Bottom