Hakuna mtu aliyewahi kutekwa na Wanausalama akarudi halafu akasimulia

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Mnaweza mlaumu sana Roma lakini ukweli unabaki kuwa hakutekwa na kakikundi tu ka kawaida. hawa ni watu maalum ambao wanafanya kazi maalum kwa maelekezo maalum toka kwa mhusika au wahusika. si rahisi akaachiwa then akaja kusimulia alitekwa na akina nani au alikuwa wapi.

moja ya masharti ya watu hawa kuachiliwa huwa inakuwa asithubutu kusema jambo lolote na siku akisema tu ajue maisha yake pengine na familia yake ameyaweka rehani. hivyo katika harakat zakuokoa maisha na kuyatunza mtekwaji huwa hasemi milele labda mpaka roho wa Mungu amjilie.

ushahidi upo kwa dr ulimboka. huyu aliteswa na kuachwa akidhaniwa amekwisha kufa lakini Mungu wake alitaka kutuonesha jambo nasi tulijue. kauli ambayo ilitumika na kipindi kile ilikuwa ile le ambayo inasemekana imetumika kwa roma "kwa nini unaisumbua serikali?"

dr ulimboka aliisumbua serikali ya kikwete kilichompata ni yeye mwenyewe anakijua pamoja na waliohusika kumteka kuwekwa wazi au hadharani na kuwa mmoja alisemekana kuwa ikulu hakuna hatua zilizokuja kuchukuliwa. na hilo suala likaishia hapo. kilichofuatia ni dr ulimboka kuwekewa ulinzi mkubwa sana ili asiweze zungumza na mtu na mpaka leo hajaweza weka hadharani nini kilifanyika huko na akina nani anaoweza wa identify kwa sura.

roma asingeweza kusema jambo pamoja na wenzie maana tayari anawafaham wahusika waliomhoji kwa sura na sauti. ameyafaham maficho yao na ni wazi si wageni au mhusika mkuu si mgeni machoni pake.

tusimlaumu roma. hata wewe usingeweza kusema kwa sababu hapo ungekuwa unaiweka idara hiyo uchi.
 
Mambo tusiyoyajua ni kama usiku wa Giza, maana ni mteremko wa speculation za hali ya juu!
 
kama hii issue ni ya kweli, Roma asingerudi salama kama wanamuziki na watz kwa ujumla wasingeishikia bango issue yake. ndio alikuwa either ameng'olewa meno na kucha, au kuuawa kabisa. ajabu yake ni kwamba alitekwa mchana kweupe.
 
hivi ikitokea ben akawa hapatikani milele, nini kitatokea? na unafikiri watakuwa wamemficha sehemu tu hadi sasaivi au atakuwa ameshaoza? hivi wanatembeaga na sped? walishachimba kabisa na makaburi au huwa wanawatupa wapi? au wanawala nyama,...manake sio kwa ukatili huo hao watu sio binadamu wa kawaida.
 
Hatumlaumu.Bali kauli za makonda na babu tale.zina tupa mashaka kwamba ile ni movie yao.wao na Roma.kama Roma alitekwa kweli.inabidi ahoji ilikuwaje babu tale aseme makonda aulizwe yeye ndo anajua walipo.hapo hapo anakuja makonda anasema watapatikana kabla ya jumapili.wakati hakuna hata mapambano yaliyotokea kuonyesha kuwa wamekombolewa.hii ni movie.
 
Mnaweza mlaumu sana Roma lakini ukweli unabaki kuwa hakutekwa na kakikundi tu ka kawaida. hawa ni watu maalum ambao wanafanya kazi maalum kwa maelekezo maalum toka kwa mhusika au wahusika. si rahisi akaachiwa then akaja kusimulia alitekwa na akina nani au alikuwa wapi.

moja ya masharti ya watu hawa kuachiliwa huwa inakuwa asithubutu kusema jambo lolote na siku akisema tu ajue maisha yake pengine na familia yake ameyaweka rehani. hivyo katika harakat zakuokoa maisha na kuyatunza mtekwaji huwa hasemi milele labda mpaka roho wa Mungu amjilie.

ushahidi upo kwa dr ulimboka. huyu aliteswa na kuachwa akidhaniwa amekwisha kufa lakini Mungu wake alitaka kutuonesha jambo nasi tulijue. kauli ambayo ilitumika na kipindi kile ilikuwa ile le ambayo inasemekana imetumika kwa roma "kwa nini unaisumbua serikali?"

dr ulimboka aliisumbua serikali ya kikwete kilichompata ni yeye mwenyewe anakijua pamoja na waliohusika kumteka kuwekwa wazi au hadharani na kuwa mmoja alisemekana kuwa ikulu hakuna hatua zilizokuja kuchukuliwa. na hilo suala likaishia hapo. kilichofuatia ni dr ulimboka kuwekewa ulinzi mkubwa sana ili asiweze zungumza na mtu na mpaka leo hajaweza weka hadharani nini kilifanyika huko na akina nani anaoweza wa identify kwa sura.

roma asingeweza kusema jambo pamoja na wenzie maana tayari anawafaham wahusika waliomhoji kwa sura na sauti. ameyafaham maficho yao na ni wazi si wageni au mhusika mkuu si mgeni machoni pake.

tusimlaumu roma. hata wewe usingeweza kusema kwa sababu hapo ungekuwa unaiweka idara hiyo uchi.
nadhan ulimboka hakutekwa na wana usalama walikua ni wajumbe wa kamati kuu ya ccm
 
Inawezekana keshasagwasagwa huyo coz akirudi maswali yatakuwa mengi na nchi inaweza kutetemeka maana hatakuwa tayari kusema ukweli labda iwe alifungwa gereza la ughaibuni akanyimwa mawasiliano.
 
Back
Top Bottom