Hakuna Mtanganyika (mtanzania bara) Anayemiliki Ardhi/Nyumba Zanzibar

Gagurito

tuwekee ushahidi wa unayoyasema

kule huwa twatimuliwa, wazenji hawapo kimuungano kabisa, machoni mwao ni kama vile watanganyika ndio maadui zao. Nashangaa wajapo kwetu humiliki mali na majumba ya gharama, viwanja na maduka makubwa! They are more selfish!
 
Nd. Makame, soma nukuu hii toka katika katiba ya Zanzibar.

"Mtanzania Bara haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar!

THE LAND TENURE ACT, 12 - 1992
ENACTED by the House of Representatives of Zanzibar.


Right of a Grant of land.

24.(1) The right of occupancy shall only be granted to
Zanzibaris who are above the age of eighteen.

“Zanzibari” means:

(a) any person who is a citizen of Tanzania in
accordance with the laws relating to citizenship
and that he was born or has been residing in
Zanzibar before and up to the 12th of January
1964;

(b) any person who, as from the 26th day of April,
1964 is a citizen of Tanzania and was born in
Zanzibar with both of his parents being
Zanzibaris or either his father or mother being
Zanzibari in accordance with the Zanzibari Act,
1985;

(c) any person who is a citizen of Tanzania and was
born or has been residing in Zanzibar before the
26th day of April, 1964; and

(d) any person who is a citizen of Tanzania with
both of his parents being Zanzibaris or either his
father or mother being Zanzibari in accordance
with paragraph (a), (b) or (c) above.


57: Zanzibari requirement.

If it is determined that:

(a) any grantee is, at any time, proved to be a non-
Zanzibari; or


(b) an interest holder-makes, or attempts to make, a
transfer of his right of occupancy to a non-Zanzibari;

an order of termination shall be issued by the Minister which
shall provide that the right of occupancy is terminated and
the land shall be vacated forthwith.

Ibara ya 57 ya sheria hiyo inasema ukigundulika wewe sio Mzanzibar na unamiliki ardhi utafutwa haki hiyo na kutakiwa kuondoka mara moja!"

Mtikila anajulikana kuwa ni mzushi na mfitinishaji. During the First Multi Party Elections in 1995 alikuwa anawazungumzia MAGABACHORI; leo imekwisha issue ya MAGABACHORI; he has cashed in. He is cheap and has controversial views. I would not view any issue he utters as credible.

La Msingi; iwekwe sera ya Ardhi ya Zanzibar hapa Jamvini.
 
ACTUALLY, NAANDIKA HII MADA KWA MAKUSUDI ILI TUJADILI...


Watz bara wanakatazwa kunujua ardhi kule visiwani, lakini wavisiwani wanaweza kununua ardhi kubwa kiasi wakipendacho hapa bara....swali langu ni, kuna haki hapo? pia, wazanzibari waliojenga bara (tukianza na mwinyi na familia yake wenye majumba mengi mikocheni na maeneo mengine dsm), wenye mashamba mengi hapa tz, siku muungano ukivunjika kama wazenji wanavyotaka, wataendelea kumiliki au ndo watavirudisha kwa wazanzibari...

Wapemba wenye maduka kila kona dsm watafungasha virago au watabadilisha kuwa wawekezaji kupitia kituo cha uwekezaji TIC.....wawe na mtaji si chini ya milioni 300 ambazo nina uhakika hawana......wataondoka wote kurudi makwao wakarundikane kwenye mitaa?...

Mbona viongozi kama mwinyi na wengine wamenyamaza kimyaaa, au ukivunjika wao wataomba uraia wa tz....
 
muungano ukivunjika madhara yake na mtikisiko wake mkubwa sana, ila madhara makubwa zaidi yatatokea kwa wazenji zaidi ya kwa wabara. amini usiamini ndio hivyo...
 
muungano ukivunjika madhara yake na mtikisiko wake mkubwa sana, ila madhara makubwa zaidi yatatokea kwa wazenji zaidi ya kwa wabara. amini usiamini ndio hivyo...
Nasubiri kinuke kuna mpemba ana viji heka 20 nimepakana nae....
 
Nimekaa na kutafakari kuhusu haki ya umiliki wa ardhi ya Zanzibar kuwa ni vigumu kwa raia toka huku kwetu Bara kumiliki kipande cha adrhi "nchini Zanzibar" lakini hawa wenzetu wakija huku kwetu wana haki ya kumiliki ardhi wawezavyo. Hii ni sera ya kibaguzi sana pamoja na kuwa ardhi ya Zanzibar ndiyo kwanza inaishia baharini lakini haki iko pale pale. Tunajiuliza na hawa Wazanzibar ni wawekezaji huku Bara?

Singependa kabisa kueleweka kuwa mchochezi lakini napenda kuonyesha hisia zangu kwamba hapa haki haitendekei upande mmoja tena kwa baraka za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ili kujiridhisha serikali ilichambue na kulitolea maamuzi sahihi ili ile dhana ya kuimarisha Muungano ielweke kwani kwa sisi wa Tanzania Bara hii ni kero ya Muungano.
 
Kuna fununu kwamba Watanganyika wanaoishi Zanzibar wametaarifiwa kuwa warudishe ardhi yote waliyomiliki
sababu hawaruhusiwi kumiliki ardhi.

Je viongozi wetu wanalijua hilo?,nina rafiki yangu mbongo (anaishi Zanzibar) alinunua shamba vilevile amejenga na nyumba juzijuzi amedokezwa kwamba inabidi auze kila kitu kwa maana ipo hatari ya kupoteza kila kitu.
 
na kwa nini ikamiliki ardhi zanzibar hali ya kua umeacha ardhi kubwa ata halijaguswa, eneo kubwa tu..
uo ni ubnafsi walionao watu wabara dhidi ua zanzibar, ukanganganie ki ardhi cha zanzibaar eti kwa kua tupo kwenye muungano na wazanzibar wamemiliki ardh bara. si mliwapa wenyewe
 
Watanganyika tunastahili kejeli zote,kwani huku hatujamaliza ardhi, bado wanzetu wanakwenda ng'ang'ania ardhi ya visiwa visivyo vya Tanganyika.Tanganyika inakila kitu kilichopo Zanzibar! Kama swala ni kukaa visiwani,mbona tuna visiwa vingi kuliko huko wenzetu walikokimbilia kuchokoza!Tena huku kwetu tulivyo barikiwa,unaweza chagua kuishi kisiwa cha maji chumvi(mf.Mafia) au kisiwa cha maji baridi(mf.Ukerewe)Kama swala ni kuishi ufukweni mbona Tanganyika ina eneo kubwa la fukwe kuliko huko ndugu zetu wanako itwa "machogo" vilevile unauchagua fukwe ya bahari au fukwe ya Ziwa Tanganyika,Nyasa,Victoria n.k.Sasa wenyewe wanaonekana hawahitaji wa Tanganyika mnacho ng'ang'ania kitu gani???
 
Wapendwa Watanzania wenzangu,

Zanzibar tangu enzi Dr Amani Karume alibadilisha katiba ili Watu wenye Asili ya Tanganyika wasimiliki Ardhi Zanzibar, badala yake wakodishwe na serikali kwa masharti ya uwekezaji sawa na wawekezaji we Nchi nyingine duniani.

Je, katiba ijayo itawarudishia Watanzania haki sawa? Au ndio na Wazanzibari walio wengi Tanganyika walipie kama kodi mahekalu, mashamba na Viwanda wanavyomiliki?
 
Wana JF, Nina maswali kidogo hapa, Hivi kama kwa sasa Mtanganyika hawezi miliki ardhi Zanzibar lakini Mzanzibar anaweza miliki huku Tanganyika, itakuwaje baada ya hii Rasimu kupita? Katiba yao itaruhusu kweli Watanganyika nao wamiliki ardhi kwao? I don't foresee this...Kama hawatakubali si itabidi na katiba ya Tanganyika izuie wao kumiliki huku kwetu? Na wale wanaomili kwa sasa huku kwetu si itabidi waondolewe au?
 
wana jf, nina maswali kidogo hapa, hivi kama kwa sasa mtanganyika hawezi miliki ardhi zanzibar lakini mzanzibar anaweza miliki huku tanganyika, itakuwaje baada ya hii rasimu kupita? Katiba yao itaruhusu kweli watanganyika nao wamiliki ardhi kwao? I don't foresee this...kama hawatakubali si itabidi na katiba ya tanganyika izuie wao kumiliki huku kwetu? Na wale wanaomili kwa sasa huku kwetu si itabidi waondolewe au?

hili ni dhahiri lazima watanganyika tukomae, haki iko wapi hapa? Hata ajira wazenji wanajazana huku kwetu na elimu zao za kuunga lakini zanzibar mtanganyika kuajiriwa ni issue labda uwe kitukuu cha mtume
 
Wana JF, Nina maswali kidogo hapa, Hivi kama kwa sasa Mtanganyika hawezi miliki ardhi Zanzibar lakini Mzanzibar anaweza miliki huku Tanganyika, itakuwaje baada ya hii Rasimu kupita? Katiba yao itaruhusu kweli Watanganyika nao wamiliki ardhi kwao? I don't foresee this...Kama hawatakubali si itabidi na katiba ya Tanganyika izuie wao kumiliki huku kwetu? Na wale wanaomili kwa sasa huku kwetu si itabidi waondolewe au?
Kweli mkuu; Tanganyika ni shamba la bibi !! nasikitika kusema wapo wakenya wanamiliki ,waChina,waHindi,Waganda,WaRundi,wageni nk. wanamiliki ardhi... Je, na wao waondolewee?
 
Iyokopokomayoko, sasa haki iko wapi? Kuna usawa kweli hapo? Kwanini wao wanufaikie Tanganyika? Huu sio ukoloni?
 
Back
Top Bottom