Hakuna Mtanganyika (mtanzania bara) Anayemiliki Ardhi/Nyumba Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna Mtanganyika (mtanzania bara) Anayemiliki Ardhi/Nyumba Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Jul 9, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Nd.wana jf. Nasikia ati ni marufuku kwa mtu kutoka bara (tanganyika) kumiliki aridhi,nyumba au jengo huko Zanzibar. Je ni kweli?
  Kama jibu ni NDIYO. Kwa nini huku Tanganyika hatujawa na sera kama hiyo kwa wazanzibar?

  Wazanzibar hawapaswi kumiliki ardhi huku Tanganyika. Kwani katiba inasemaje? Si kwamba mtanzania ana uhuru wa kuishi popote ndani ya Jamhuri ya Muungano. Kwa nini watanganyika hawamiliki aridhi kule?

  =========
  June 2012:
  July 2013:
   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii tetesi yako ni hatari kama ni ya kweli au ya uongo
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii nadhani itakuwa uongo mkubwa..., mtu kutoka bara?, je wali ambao wanatoka nje ya Tanzania?
   
 4. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  duh! kama hiyo ni kweli basi itakuwa ni hatari!
   
 5. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Yani nataman aje atokee rais kichaa huku bara..aamue kuuvunja 2 huo muungano..hauna faida kwa watanganyika kabisa.
   
 6. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Msikurupuke kusema uongo wakati jambo hili la ubaguzi linafanyika. Nina rafiki yangu mfanyabiashara Kariakoo, pia amefanya/anafanya biashara zake Pemba. Aliona shamba akataka kununua ili alime karafuu. Mwenye eneo alikubali, walipokwenda kwa Sheha ili waandikishiane Sheha akaleta kauzibe. Ukatokea mvutano kati ya Sheha na mwenye shamba. Ndipo Sheha akapasua, " Huyu mtu wa bara hawezi kununua ardhi huku kwetu wao wanamapori mengi". Hadi leo rafiki yangu hajapata eneo sehemu yoyote, si Unguja wala Pemba.

  Kama haitoshi mwaka jana Novemba nilimwuuliza muunguja,"Hivi Unguja yote imejaa kiasi cha kwamba wazanzibari hawawezi kupata viwanja?" akasema "Haijajaa, viwanja na mashamba yapo. Watu mbona wanauziana kila uchao? Ni pesa yake mtu na maelewano na mwenye mali" Nikamuuliza "Na mimi naweza kupata nikiwa na hela ya kutosha?" Akajibu "Huwezi kupata." Nilipomdadisi zaidi kwanini siwezipata na yeye anawezakupata. Jibu lilikuwa, "Mbona wewe unatokea Bara, huwezi kupata." And I concluded on how racist are they.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Sitta alisema jana, ka mbuai mbuai bwana! Mambo yawekwe hadharani na kama Muungano uvunjwe na ijulikane hivyo, sio kujishaua tuu!!
   
 8. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Huu ni uongo uliokithiri na kushtadi.

  Mfano mzuri ni maeneo ya Chake-Chake, Kusini, Pemba ambako Kanisa la Roman Catholic wanamiliki kiwanja na wamejenga kindergarten

  Hapa hapa Chake-Chake, Kanisa la SDA wanamiliki kiwanja na wamejenga hospitali.

  Unguja, maeneo ya Cheju, Kanisa la Roman Catholic wanajenga high school.

  Lakini kubwa ni kwamba karibu mtaondoka, viwanja vya nini?

  Nyie huku mje mlime tu mpaka "muungano" utakapo kata roho.
   
 9. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo ni watu kutoka bara tu, au ni watu kutoka nje ya zanzibar
   
 10. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zanzibar, ardhi yote ni mali ya Serikali, yenu wapeni magabachori tu.

  Mtakufa kwa pombe na ufisadi.
   
 11. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  kwahiyo mzanzibar na yeye aruhusiwi kupata ardhi, zanzibar????, pia kuna wanzanzibar wengi tu (kina Ali Hassan Mwinyi n.k.) wana ardhi bara je na wenyewe ni magabachori?
   
 12. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  'The man shall rise from the hills and save the people at their hour of need'.

  Kukiwa na mgombea Urais atakayesema atavunja Muungano kura yangu anayo hata kama ni Fisadi kama EL, nitamchagua tu kuondoa hii kero ya miaka mingi. Ee Mwenyezi Mungu inua kiongozi thabiti atakayefanya maamuzi magumu ambayo wengine wameshindwa.
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hizi ni fitna na choko choko kuna mimi mtanganyika, mbona nina nyumba nimejenga na nimepangisha Zanzibar!!!!. Acheni fitina zisizokuwa na mpango
   
 14. Jobab

  Jobab Member

  #14
  Jul 9, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina uhakika na watanganyika kutomiliki ardhi Zanzibar ila makanisa na taasisi za kidini ni tofauti sana na mtu binafsi, na hata hivyo, kanisa kama RC, SDA, KKKT, TAG na mengineyo kutoka tanganyika pamoja na kuwa na usajili wa kanisa huku tanganyika, bado wanapoenda kuanzisha makanisa zanzibar lazima tena watume maombi na wapewe usajili wa makanisa yao. Huwezi toka hapa tanganyika na usajili wa hapa ukanzisha kanisa zanzibar, usajili wa bara hautambiliki zanzibar...huu muungano una matatizo kibao
   
 15. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ali Hassan Mwinyi kwao Mkuranga, Unguja alikuja kusoma Quran tu na hakutoka tena. Yeye na wenzake kibao.
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Acheni upotoshaji mimi mwenyewe na nyumba Zanzibar nimejenga nimepangisha, na mimi ni Mtanganyika safi naishi bara
   
 17. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Wakuu,
  Naomba kufahamishwa endapo kanisa katoliki, sabato/SDA wanapo milikishwa ardhi wanaiwakilisha Tanzania Bara?
  maana nimeshindwa kuelewa jibu hili.
   
 18. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio. Kwa sababu Zanzibar ni nchi yenye Sheria zake tofauti na Bara.
   
 19. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ritz,

  Watu wengine wa ajabu sana majungu na fitina zisizo na mpango ndio jadi, kama umeingizwa mjini ulipotaka kununua kiwanja au nyumba na wajanja zanzibar bora useme ukasaidiwa na sio kutoa visingizio visivyo na mpango
   
 20. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katika orodha ya mambo ya muungano suala la ardhi halimo. Wenzetu zanzibar wapo makini kulinda ardhi yao kuliko bara.
  Kama yanavyoonekana hapa chini:
  NYONGEZA YA KWANZA_________(Imetajwa katika ibara ya 4)Mambo ya Muungano​
  1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.2. Mambo ya Nchi za Nje.3. Ulinzi na Usalama.4. Polisi.5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.6. Uraia.7. Uhamiaji.8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwanchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta nasimu.12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili yamalipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamojamabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusikana fedha za kigeni.13.Leseni ya viwanda na takwimu.14.Elimu ya juu.15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa yamotokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo zamafuta au bidhaa, na gesi asilia.16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yoteyanayohusika na kazi za Baraza hilo.17.Usafiri na usafirishaji wa anga.18.Utafiti.19.Utafiti wa hali ya hewa.20.Takwimu.21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine​
  yanayohusiana navyo.
   
Loading...