Hakuna msaada wowote wa viwanja Makonda ni msanii na mfanyabiashara tu

Bila kujali anasaidia biashara ya nani, jambo la kupongezwa ni kwamba anasaidia watumishi kupata viwanja kwa bei nafuu yaani sq mita moja kwa 4,000.

Hii ni nzuri na mimi binafsi sina tatizo na GSM kwa sababu kama kweli viwanja vipo na watu watapata basi hakuna tatizo.
Labda kama una ugomvi binafsi
Kwa hiyo unaona ni sawa kwa kiongozi wa umma kuwa kuwadi/dalali wa wafanyabiashara? Miiko ya uongozi inaruhusu hii? Je, kama anapata commission kwa ukuwadi/udalali huo?

Kama alichokisema mleta mada ni kweli, basi kinapaswa kufikishwa kwenye Tume ya Maadili ya Umma. Hii ni kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa tu. Maana kama ilivyokuwa kwa wasilisho juu ya elimu yake, Tume haikulifanyia kazi!
 
Sina chuki na mako hata kidogo,and he is doing fine kwa bahati mbaya wachangiaji wengi wanalihusisha hili swala na sasa,najiuliza kwa nini GSM kwa nini sisi wadau wengine wenye makampuni kama hayo na viwanja tunavyo hatujashirikishwa !?hoja yangu ipo kiuchumi zaidi kuliko kisiasa kama wengi walivyojaribu kuzungumza
Mkuu toa hints kidogo! Weka bei za walau makapuni matatu ili tulinganishe. Unaweza kukuta nyie mnapata wateja zaidi kuliko hata hao GSM.
 
Sasa usanii upi square mita moja inauzwaje kwa mfano viwanja tu vilivyo pimwa na halmashauri tena ambazo haziuzwi na makampuni ya real estate embu tupe scales sio kulalamika tuuu elfu4 ni usanii aya tupe bei ya viwanja kwa square mita zinasemaje kwa dar.
Maadili ya utumishi wa umma yanamfunga huu ni ujangiri wa hali ya juu ni sawa na kumsaidia mkandarasi kisa kapunguza bei ya ujenzi na kakupa 10%.Kiuhalisia huyu kijana na kundi wamemfanya mkulu kama Babu yao wanajivunia kadri wawezavyo.
 
Makonda ajaribu kuwa muwazi tu kwamba hivyo viwanja alivyotangaza kugawa kwa watumishi wa serikali mkoa wake, sio kwamba anagawa ama anauza kwa bei nafuu ukweli ni kwamba anajaribu kuwasaidia wale akina gharibu wa GSM kufanya biashara zao za viwanja kupitia kampuni yao ya real estate inaitwa Property International.

Hata ule mradi wa kupeleka wafanya biashara wenye yard za magari kutoka mjini kwenda Kigamboni ni usanii vilevile eneo lililotengwa kwa ajiri ya hiyo kazi ni la hao hao Property International. Kama hivi karibuni kuna mtu kapita hii njia ya Kibada-Mwasonga atakuwa shuhuda mzuri, pale ilipokua ofisi za hao Property International ndo pamewekwa eneo (kigamboni industrial erea) kwa ajiri ya hao wauza magari.

Makonda awe mkweli kwamba baada ya kupewa eneo amekubali kutumika kutangaza biashara za watu, hiyo bei ya 4000 aliyosema ni pungufu kwa idadi ya watu 3000 aliyosema wote wakifanikiwa kununua viwanja hao jamaa hawata kuwa na hasara yoyote!

Makonda aache usanii.
Mimi najua makonda ana uwezo mdogo sana kiakili! Pia mamini watumishi wa umma ni sehemu ya tatizo na watu wasiojielewa kwenye hii nchi. Najua bashite yawezekana hata motivation theories hajui huyu! Unawapa watumishi wa dar. Viwanja ili wengine wajione wana bahati mbaya kwenda kuishi nyaishozi? Huyu mkuu wa mkoa ana akili za ajabu sana aisee .
 
Ukitaka kujua ni usanii wa ki zero brain Kwa nini alipokuwa hana accessibility ya vituo vya tv hakutangaza hayo?
 
Bila kujali anasaidia biashara ya nani, jambo la kupongezwa ni kwamba anasaidia watumishi kupata viwanja kwa bei nafuu yaani sq mita moja kwa 4,000.

Hii ni nzuri na mimi binafsi sina tatizo na GSM kwa sababu kama kweli viwanja vipo na watu watapata basi hakuna tatizo.
Labda kama una ugomvi binafsi
Wewe hata ukiambiwa Bashite ni baba yako utaamini tu, unaambiwa akili za kuambiwa changanya na zakwako, ni lini na wapi tanzania kukawa na bei permanent ya kiwanja au viwanja? unawezaje kuthibitisha hiyo anayosema ni pungufu ya elfu nne? Tanzania tuna biashara huria, ukimkuta mtu na shida zake au mtu akikuta na shida zako mnaelewana, shida ndio huwa zinadetermine bei ya eneo husika, hakuna bei elekezi. Angalia bei anayokwambia sasa ni bei ya punguzo, afu nenda kaangalie watu wengine wanauzaje maeneo hayo. By anyway huyo mtu wenu tunamjua hakuna operation yake imewahi kufaulu, zote zinaishia kuangukia pua.
 
Shida ni jinsi anavyoi represent kwenye public..mkuu makampuni yanayodeal na viwanja yapo mengi kwa nini GSM!?manispaa kila siku zinatangaza mauzo ya viwanja kwanini hajapita uko!?hyo bei ya 4000 isikutishe mkuu hakuna hasara yoyote hapo..kibaha tu hapo viwanja vinauzwa sqm 2000 itakua hyo 4000!?
Sasa Kibaha na Kigamboni unalinganishaje bei!!?
Cha msingi walengwa wapate maeneo kwa bei iliyotajwa maana huwezi mpangia mtu bei ya kuuza, kwani nini mbaya mtu kuwaombea punguzo kwa muuzaji!!?
 
Katika viongozi wanaochukiwa nafikiri mako ni No 1.nasaabu za kumchukia sizioni. Watu tujaribu kuwa na subra.sio kila kitu lazima utukane
 
kwani shida ni GSM au waru kupata viwanja bei nafuu? je wewe na kampuni yako ya ufipa limited unaweza ukawapa wanatumish viwanja kwa bei nafuu zaidi ya 4000? au ni genye zinawasumbua .makonda akijaribu kuwa mbunifu nyie wafipa lazima muweke kimavi wakati nyie ata jengo mnalomiliki kama chedema hamna kazi kubwabwaja.
 
maelezo mareefu lakini hakuna mahali umeonesha namna huo usanii ulivyofanyika.
 
Sina chuki na mako hata kidogo,and he is doing fine kwa bahati mbaya wachangiaji wengi wanalihusisha hili swala na sasa,najiuliza kwa nini GSM kwa nini sisi wadau wengine wenye makampuni kama hayo na viwanja tunavyo hatujashirikishwa !?hoja yangu ipo kiuchumi zaidi kuliko kisiasa kama wengi walivyojaribu kuzungumza
Mkuu biashara ushindani hivyo kama hujamuendea RC na kumueleza atajuaje unaeneo na uko tayari kuuza viwanja kwa bei nafuu!? Yeye aote au angepanga bei elekezi hapo silingekuwa tatizo lingine!? Approach zetu kwenye baadhi ya masuala yabidi zibadilike maana unaanzaje kumushutumu mtu wakati hujampelekea proposal akaikataa!
Pia hata wewe ukitangaza leo viwanja vilivyopimwa sqrm@4000 Kigamboni wateja watamiminika tu.
 
ni
Shida ni jinsi anavyoi represent kwenye public..mkuu makampuni yanayodeal na viwanja yapo mengi kwa nini GSM!?manispaa kila siku zinatangaza mauzo ya viwanja kwanini hajapita uko!?hyo bei ya 4000 isikutishe mkuu hakuna hasara yoyote hapo..kibaha tu hapo viwanja vinauzwa sqm 2000 itakua hyo 4000!?

nimekugongea "like "
 
Kwani ule mpango wa walimu kupanda daladala bure umeishia wapi!! Bashite bhana mtu wa kupenda kiki Sana
 
Deal zote makond ana % yake ndomana ana push kwa nguvu zake zote zifanikiwe

Ova
 
Mkuu kilichopo ni:
Unamjua nani,
Si una nini.

Nasema utadhani mazuri.

Kingine,
Tupunguze ubinafsi- (Umimi)

Wewe una Mali lakini umeing'ang'ania mwenyewe?
Yaani Mali yako kisha Wateja utafute mwenyewe, Hee! Njaa gani hii? Hata Mungu unamkwaza.

Ndio Biashara imeparaganyika lakini japo kwa kusuasua watu wanauza bado na wanunuzi wapo Vilevile.(Telling this from experience and I do have evidence should anyone need)

Tuache Roho mbaya kuona ukimpa Mtu akuhangaikie Kazi yako (Daalali) atafaidika sana.

Ingawa si lazima saaana na hulazimiki ukizingatia kuwa uamuzi ni wako juu ya Mali yako.

Aidha niseme,
Rizki ya Mtu ipo mikononi mwa Mtu.

Mwanadamu anaposhukuru kwa kupata hata kidogo kiasi gani kupitia wewe ndio baraka zinapozidi kufunguliwa na pia rizki zaidi kwako kuongezeka.

Niwie radhi,
Hii yaweza kuwa ukweli wenye ukakasi kiasi.
Lakini, maneno yangu yasiwe sheria.

____________________________________________
PANGA, PANGISHA, UZA, NUNUA N. K :
Nyumba, Ofisi, Viwanja, Mashamba, Dhahabu,
Vito (ghafi), Migodi pamoja na Biashara yoyote.

Usisite kuwasiliana nami :
+255-714-591548.
___________________________________________


Puliizzz.
Naona umepalilia biashara yako vya kutosha,embu nicheck basi tuuze hivi viwanja..0769468965.
 
Back
Top Bottom