Hakuna moto wa umeme bali umeme ni chanzo kikubwa cha moto

Anko Drew

Member
Jun 9, 2021
15
41
Moto umegawanyika katika madaraja makuu matano (5);

1. Daraja A
-Huu ni moto utokanao na vitu vyenye asili ya mimea mf. Karatasi, mbao, nguo n.k

2. Daraja B
-Huu ni moto utokanao na vimiminika vinavyowaka, ambao wengi huuita moto wa mafuta.

3. Daraja C
-Huu ni moto utokanao na gesi inayowaka. Hivyo milipuko yote itokanayo na gesi, moto huo tunauweka kwenye daraja C

4. Daraja D
-Kwenye moto huu, viunguavyo ni vile vitu vyenye asili ya madini kama vile chuma n.k

5. Daraja F au K
-Moto huu ni ule unaosababishwa na Mafuta ya kupikia yanapochemka sana na endapo yanapata chanzo kidogo cha moto huweza kuwaka.
 
Back
Top Bottom