Hakuna mfanyakazi kuhama mpaka kulipwa kwanza – Rais Magufuli

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amepiga marufuku uhamisho wa wafanyakazi bila kuwalipa stahiki zao huku akisema kumekuwa na utaratibu wa kuwahamisha wafanyakazi bila kuzingatia taratibu za malipo ya uhamisho.

MEI13.jpg


Rais Magufuli amepiga Marufuku hiyo Jumatatu hii, alipokuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chuo Cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Rais Magufuli alisema “Sasa niwaombe wafanyakazi, yoyote akihamishwa hakuna kuhama mpaka uwe umelipwa pesa ya uhamisho, kuanzia juu mpaka chini yeyote atakaye kuhamisha mwambie nipe hela yangu ya uhamisho ninapoenda akishindwa usihame kaa hapo hapo ufanye kazi.”
 
Teh wazee wa rishafo walikua wamezidi, kila siku vitisho kuhamisha kuhamisha haya wahamishe na cheque mkononi
 
Back
Top Bottom