Hakuna mbunifu wa kibiashara anayeweza 'kubrand' chipsi mayai?

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Umuofia kwenu,

Tukiwa kwenye mazungumzo yasiyo rasmi na wafanyakazi wenzangu hapa kwenye box, tumejikuta tukiulizana masuala kadha wa kadha ya kujisogeza mbele ktk kusaidiana kukuza pato la nchi kupitia biashara..

Kama inavyofahamika, kutokana na maisha ya kimjini mjini, tumekuwa tukipata misosi maeneo ya viwanja pamoja na snacks za hapa na pale ambazo kiukweli ni inteneshno levo by name tu ila hakuna la ajabu kihivyo, achilia mbali KFC, chukulia mfano hizi burger, hamburg, pizza na nyinginezo za Mac Donald.

Huyu Mac kumbukumbu zinasema alianza kuuza hamburg ktk fast food yake kama kamgahawa ka babakyuu tu miaka hiyo..

"McDonald's is an American hamburger and fast food restaurant chain. It was founded in 1940 as a barbecue restaurant operated by Richard and Maurice McDonald, in San Bernardino, California".

Leo tunavyoongea hapa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya msosi huko duniani.. Ni ubunifu tu!

Nisiwachoshe, nimetumia mfano wa Mac Donald kuleta kwenye dunia ya tatu huku mavumbini ambako nako kuna kaubunifu ka msosi special ambao pengine tunauchukulia poa. Chipsi mayai au Kiepe yai (zege)..

Nimefurahi kuona intaneti inaufahamu huu ubunifu kuwa umeasisiwa Tanzania, Afrika Mashariki. Yaani taarifa zilizowekwa mtandaoni zinaitambua hivyo. Naamini ni kweli maana ktk nchi za wenzetu sijawahi 'kuona' chipsi yai kama popular dish..

Chipsi mayai (Swahili for "chips and eggs") is a common food found in Tanzania, East Africa.

In its most basic form, chipsi mayai is a simple potato-egg omelette. In Tanzania it is also called Zege. It is available in most regions of Tanzania, from the most remote villages to large towns. Food stands both indoors and on streets make them to order, and while potatoes are usually not prepared until late morning in Tanzania, those who are able to find it earlier in the day can have it as a breakfast meal.


Sasa tumejiuliza; Je, hatuwezi kumpata Mac Donald wetu hapa akajaribu kuipa thamani Chipsi Yai ili iwe internationally recognized dish na tukawa na 'Mac Donald' yetu itakayouza msosi wa aina hiyo?

Utofauti wake na ubunifu wa kuchanganya mayai kwenye chips ndio selling point... Sijui nimeeleweka?

Vielelezo: Chipsi mayai - Wikipedia

McDonald's - Wikipedia

Chips Mayai: Bidhaa pekee iliyogunduliwa Tanzania tangu tupate Uhuru!

Nakaribisha uumbaji zaidi wa wazo hili..
 
Hata mimi nilikuwa sijui zege nchi nyingi hawalijui

Utashangaa wataibuka wachina na kuja na brand
 
Hata mimi nilikuwa sijui zege nchi nyingi hawalijui
Utashangaa wataibuka wachina na kuja na brand
Uko sahihi Boss, wachina watatupiga bao nasi tumeshangaa.. Wanaoweza kutekeleza wachukulie hii serious..
Sio lazima nifanye mimi kama ambavyo Mphamvu kanipendekeza... Maana hata aliyestate law of flotation siye aliyetengeneza Meli..
 
Wazo zuri na nipo tayari kwa utekelezaji nahitaji partner tubadilishane mawazo
 
Homework nzuri sana hii kwa wahitimu wa SUA somo la Food Processing.
AMKENI WAHITIMU WA SUA!
 
Jitokeze makinika akugeuze Accacia. Atakulima kodi mpaka utashika kichwa.
Watanzania wana idea nyingi sana za kupata hela nzuri ila Tanzania inatubana kuendelea
 
Ngoja niende kujazilizia nyama wikipedia

"Zege (Chipsi Yai) has contributed to childhood pregnants by 99 percent being the number one female teenagers food choice. It is said that eating Chips Yai increases Hips and therefore making females look sexier.
 
Swala ni kwamba
1) Je waweza kuzihifadhi kwa muda gani bila uharibika zikiwa "packed"??
2) Na Utaweka "Preservatives" gani za kufanya isiharibike haraka??
3) Je hizo "Preservatives" hazitoharibu ladha ya Chipsi??
 
Swala ni kwamba
1) Je waweza kuzihifadhi kwa muda gani bila uharibika zikiwa "packed"??
2) Na Utaweka "Preservatives" gani za kufanya isiharibike haraka??
3) Je hizo "Preservatives" hazitoharibu ladha ya Chipsi??
kwani KFC wanauzaje chipsi kuku zao na yale mazagazaga mengine like wali n burger? Na ukiangalia bidhaa zote hizo ni perishable..suala hapa sio kuhifadhi kwa muda mrefu ila ishu ni kuifanya iwe na taste nzuri na ya kuvutia kwa walaji (branding),ili watu wakija kwenye migahawa yako basi wanapata kitu moto kabisa, wanakula, wanajiramba zao vidole hlf wanasepa huku wakikuachia misimbazi kadhaa.
 
Back
Top Bottom