Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,751
Niliwahi kufika Kaole Bagamoyo kule kwenye makumbusho... Pale kuna kaburi moja maarufu sana... Wamezikwa watu wawili kwa pamoja mke na mume ambao walipendana sana kiasi kwamba walikufa pamoja...
Roho ndio nishati ya mwili, yaani ndio pumzi ya uzima kwenye mwili... Bila roho mwili ni mfu na haukawii kuharibika... Kati ya hivi vitu viwili, roho na mwili kuna kitu cha tatu ambacho ni nafsi ama utambulisho... Nafsi ni matokeo ya muunganiko wa roho na mwili... Nafsi ndio software ya uhai inayobeba muktadha na miamala yote kwenye mwili wenye roho kuanzia, kuweka kumbukumbu, kupanga jambo, kutoa maamuzi, hisia nk nk.... Nje ya nafsi kwenye utenganisho wa mwili na roho hakuna kinachoendelea
Kwenye vitabu vya kiimani, kwenye kipengele cha mahusiano na ndoa hasa kwa wakristo.. Kuna maneno yanasema... NITAKUPENDA HADI KIFO KITAKAPOTUTENGANISHA....
Mapenzi ni hisia... Hisia huzaliwa, hukua, huzeeka na hatimaye hukoma kuwa yaani hufa.. Yaani hisia zikifa wawili hutengana na kuachana... Lakini kama bado wako hai kuna wakati hukumbukana, ndio maana baadhi hurudiana...
Hii ni tofauti kabisa kwenye KIFO... Mwisho wa mawasiliano yenu kihisia ama kindugu ni kifo... Roho zinapofikia ukomo wake mwilini na kusema hakuna mawasiliano tena... Kila moja huchukua njia yake kwenye vast galaxy... Ulimwengu mpana usio na kikomo....
Hii inathibitishwa pia kwenye mambo ya kiimani kwamba hata huko mbinguni, peponi au jehanum hakuna featuring wala mawasiliano yoyote... Kila roho inasimama yenyewe
Codes zote za kifamilia, kirafiki, ndugu na mahusiano mengine yoyote yale hukatika na kukoma kuwa pale ufu unapotamalaki... Reincarnation pia inatoa ithibati zinazofanana na hizo... Simulizi zote za reincarnation sio kati ya roho na roho bali kati ya mwili wenye roho na roho na kinyume chake...
Simulizi za ndoto za kutokewa na marehemu ni kati ya mwili wenye roho na roho... Hakuna hata siku moja mtu alishawahi kutokewa ndotoni na wapendwa wote wawili kwa wakati mmoja mfano wazazi na wakakwambia kwa pamoja huko waliko kukoje ama kuna nini...
Mara nyingi kama si zote utatokewa na mmoja tuu tena katika vague image kwakuwa yeye si mtu kamili tena... Kiubinadamu tu na katika bali ya kuoneshana upendo mtaahidiana kupendana milele lakini kiuhalisia ni kudanganyana live kwakuwa mwisho wa mawasiliano yenu ni KIFO... Baada ya hapo hakuna kitu tena....