Hakuna matatizo ya kudumu Ni suala la muda tuu!!

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Kulikuwa na Kijiji kimoja kilipatwa na njaa kali sana, watu walikula mizizi ya miti Kama ulavyo viazi na magimbi. Katikati ya njaa hiyo KIJANA mmoja katika Kijiji hicho alibahatisha kupata mkungu mmoja wa ndizi wenye ndizi 14. Akafurahi sana na akaweka utaratibu wa kula ndizi moja kwa siku, mpaka njaa itakapoondoka..

Alianza kula ndizi moja moja, ndizi zilianza kuisha lakini dalili ya njaa kuisha haikuonekana. Hali hii ilimuhuzunisha sana akawaza mno ataishi vipi baada ya ndizi zote kuisha..

Mwisho akaamua kwamba Kama itatokea njaa kuendelea, Basi ndizi ya mwisho ataenda kuilia juu ya mti mrefu Sana ili akimaliza kula ajirushe chini kwasababu hatoweza kuishi kijijini pale ndani ya box la njaa kali ya kiwango hicho..

Kama ujuavyo aliwazalo mjinga ndilo linalomtokea, ndizi zile zilipukutika na siku zikakimbia Kama usiku wa deni na ndizi ikabakia moja, ili hali njaa ikizidi katika Kijiji kile. Akaamua kutimiza nadhiri yake akaichukua ndizi yake ile moja iliyobaki, na akaenda nayo juu ya mti akaila Kisha ajirushe ili afe...

**----Njaa kwake ilionekana Ni shidaa iliyozidi shida zote, Njaa ilimwambia yeye sio lolote na chochote kwenye dunia hii yenye asali na maziwa.

**------ Njaa kwake ilimfanya asiwaze huzuni atakayowaachia Rafiki zake kutokana na kifo chake..
**-----Njaa hiyo ilimpa ubinafsi hata hakuwaza Kijiji na taifa vinahitaji nguvu zake

Hakufikiria kifo chake kitakuwaje katika Kijiji Kile chenye njaa, watu watakula nini msibani? Je, wachimba kaburi wataweza kuifanya kazi yao vyema ya kuchimba kaburi katika kipindi hicho Cha shambulio la njaa? KIJANA yule hakuwaza kabisa!!

Kijana yule akapanda juu ya mti ule mrefu sana, akamenya ndizi yake taratibu akaila akatupa chini ganda la ndizi, Kisha akasali sala yake ya mwisho.

Baada ya kumaliza kusali akafumbua macho yake ajirushe, kabla ya kujirusha kwa mbali akamuona Bibi kizee anatembea na mkongonjo wake taratibu kuja kwenye eneo la ule mti aliokuwa ameupanda..

Akaamua kusubiri Bibi yule apite ili ajirushe, lakini Bibi yule alipokaribia kwenye ule mti na kuliona ganda la ndizi lililotupwa, akapiga magoti akasali na kumshukuru MUNGU kwa furaha tena kwa uso uliojaa tabasamu lenye kicheko, akalichukua ganda lile na kuanza kulila, alitafuna Kama vile ulavyo mishikaki iliyotengenezwa kwa nyama choma iliyonona..

Yule KIJANA huku akiwa juu ya mti amekodoa macho alijiuliza. Ikiwa Kuna mtu anakula ganda la ndizi nililolitupa! Je, ni sahihi kwangu Mimi mla ndizi kujiua kwasababu ya njaa?

Sijui Ni jibu gani alilolipata KIJANA yule kichwani mwake, lakini alishuka haraka Sana chini ya mti ule na kuelekea geto kwake, Hakufikiria wala kuwaza kujiua Tena kwani aligundua kuwa, pamoja na njaa ile, ila yeye ni BABA LAO...

Wewe ni Nani mpaka unyong'onyezwe na mapito uliyo nayo sasa?

Hata Kama huna kazi, umekosa mkopo chuo kikuu, huna mtoto, Majirani zako wanakusema unavyoshindia ugali dagaa, unatafuta mchumba na hupati, unaishi kwenye nyumba ya kupanga, umefail masomo yako, umefukuzwa kazini, unatafuta kazi na hupati, biashara yako haiendi vizuri,... (n.k)

Wewe ni wa maana sana ni suala la muda tuu, matatizo na magumu unayopitia leo yasikushinde kiasi kwamba ujione huna thamani na huna tumaini lolote kabisa katika maisha yako. Kumbuka MUNGU hupanga kila kitu katika maisha yetu ya hapa duniani na kwa faida yetu ya maisha yetu ya milele..

Matatizo au magumu unayopitia leo yaone kana kwamba yanakuepusha na hatari iliyopo mbele yako, au yanakuandaa kuwa mtu Bora zaidi kesho yako..

Ndugu yangu usile ndizi yako ya mwisho juu ya mti mrefu ili ukimaliza ujirushe, Amini majira hayo unayoyapitia pengine umeandaliwa mazuri zaidi kumzidi hata YUSUFU.

Sikufundishi kufurahia Shida, . shida haifurahishi hata kidogo,
Nakufundisha kuvulimilia shida kwasababu zipo kwa ajili ya Mimi na wewe, Shida huleta Radha ya Maisha ndio maana pilipili zinatuwasha lakini bado hatukomi kuzinunua na kuzila tena!

Shida hutukomaza..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulikuwa na Kijiji kimoja kilipatwa na njaa kali sana, watu walikula mizizi ya miti Kama ulavyo viazi na magimbi. Katikati ya njaa hiyo KIJANA mmoja katika Kijiji hicho alibahatisha kupata mkungu mmoja wa ndizi wenye ndizi 14. Akafurahi sana na akaweka utaratibu wa kula ndizi moja kwa siku, mpaka njaa itakapoondoka..

Alianza kula ndizi moja moja, ndizi zilianza kuisha lakini dalili ya njaa kuisha haikuonekana. Hali hii ilimuhuzunisha sana akawaza mno ataishi vipi baada ya ndizi zote kuisha..

Mwisho akaamua kwamba Kama itatokea njaa kuendelea, Basi ndizi ya mwisho ataenda kuilia juu ya mti mrefu Sana ili akimaliza kula ajirushe chini kwasababu hatoweza kuishi kijijini pale ndani ya box la njaa kali ya kiwango hicho..

Kama ujuavyo aliwazalo mjinga ndilo linalomtokea, ndizi zile zilipukutika na siku zikakimbia Kama usiku wa deni na ndizi ikabakia moja, ili hali njaa ikizidi katika Kijiji kile. Akaamua kutimiza nadhiri yake akaichukua ndizi yake ile moja iliyobaki, na akaenda nayo juu ya mti akaila Kisha ajirushe ili afe...

**----Njaa kwake ilionekana Ni shidaa iliyozidi shida zote, Njaa ilimwambia yeye sio lolote na chochote kwenye dunia hii yenye asali na maziwa.
**------ Njaa kwake ilimfanya asiwaze huzuni atakayowaachia Rafiki zake kutokana na kifo chake..
**-----Njaa hiyo ilimpa ubinafsi hata hakuwaza Kijiji na taifa vinahitaji nguvu zake
Hakufikiria kifo chake kitakuwaje katika Kijiji Kile chenye njaa, watu watakula nini msibani? Je, wachimba kaburi wataweza kuifanya kazi yao vyema ya kuchimba kaburi katika kipindi hicho Cha shambulio la njaa? KIJANA yule hakuwaza kabisaaaaaaaa!!

Kijana yule akapanda juu ya mti ule mrefu sana, akamenya ndizi yake taratibu akaila akatupa chini ganda la ndizi, Kisha akasali sala yake ya mwisho.
Baada ya kumaliza kusali akafumbua macho yake ajirushe, kabla ya kujirusha kwa mbali akamuona Bibi kizee anatembea na mkongonjo wake taratibu kuja kwenye eneo la ule mti aliokuwa ameupanda..

Akaamua kusubiri Bibi yule apite ili ajirushe, lakini Bibi yule alipokaribia kwenye ule mti na kuliona ganda la ndizi lililotupwa, akapiga magoti akasali na kumshukuru MUNGU kwa furaha tena kwa uso uliojaa tabasamu lenye kicheko, akalichukua ganda lile na kuanza kulila, alitafuna Kama vile ulavyo mishikaki iliyotengenezwa kwa nyama choma iliyonona..

Yule KIJANA huku akiwa juu ya mti amekodoa macho alijiuliza. Ikiwa Kuna mtu anakula ganda la ndizi nililolitupa! Je, ni sahihi kwangu Mimi mla ndizi kujiua kwasababu ya njaa?
Sijui Ni jibu gani alilolipata KIJANA yule kichwani mwake, lakini alishuka haraka Sana chini ya mti ule na kuelekea geto kwake, Hakufikiria wala kuwaza kujiua Tena kwani aligundua kuwa, pamoja na njaa ile, ila yeye ni BABA LAO...

Wewe ni Nani mpaka unyong'onyezwe na mapito uliyo nayo sasa?

Hata Kama huna kazi, umekosa mkopo chuo kikuu, huna mtoto, Majirani zako wanakusema unavyoshindia ugali dagaa, unatafuta mchumba na hupati, unaishi kwenye nyumba ya kupanga, umefail masomo yako, umefukuzwa kazini, unatafuta kazi na hupati, biashara yako haiendi vizuri,... (n.k)

Wewe ni wa maana sana ni suala la muda tuu, matatizo na magumu unayopitia leo yasikushinde kiasi kwamba ujione huna thamani na huna tumaini lolote kabisa katika maisha yako. Kumbuka MUNGU hupanga kila kitu katika maisha yetu ya hapa duniani na kwa faida yetu ya maisha yetu ya milele..

Matatizo au magumu unayopitia leo yaone kana kwamba yanakuepusha na hatari iliyopo mbele yako, au yanakuandaa kuwa mtu Bora zaidi kesho yako..

Ndugu yangu usile ndizi yako ya mwisho juu ya mti mrefu ili ukimaliza ujirushe, Amini majira hayo unayoyapitia pengine umeandaliwa mazuri zaidi kumzidi hata YUSUFU..
Sikufundishi kufurahia Shida, . shida haifurahishi hata kidogo,
Nakufundisha kuvulimilia shida kwasababu zipo kwa ajili ya Mimi na wewe, Shida huleta Radha ya Maisha ndio maana pilipili zinatuwasha lakini bado hatukomi kuzinunua na kuzila tena.....!!
Shida hutukomaza..

Sent using Jamii Forums mobile app
Thanks Allah be with you.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Ni rahisi kuandika hapa, ila usiombe yakukute
Kweli kabisa , ila ni muhimu kujipa matumaini katika hali kama hizi kwani ukiamua kubaki kulia , kuhuzunika kwingi na Kukata tamaa hakusaidii kitu bali huongeza matatizo zaidi kwani wakati huo umeamua kukata tamaa Jua bado linaendelea kuchomoza mashariki na kuzama magharibi kama kawaida halisemi ngoja nitulie fulani yupo kwenye hali ya huzuni na Kukata tamaa.
 
Back
Top Bottom