Hakuna maslahi binafsi bali uzalendo kwa chama na taifa letu.

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Ipo dhana imejengeka sana humu mitandaoni hasa kutoka vijana wa upinzani kwamba kinachowasukuma vijana wa CCM kulitetea taifa lao ni kusaka vyeo na pesa tsh 7000 hii ni dhana ya hovyo isiohitaji kufumbiwa macho.
Mimi nakitetea chama lakini ukweli ni kwamba nafanya hivi huku nikiwa mwanachama mwenye kadi ya chama kwa mapenzi yangu nikiishi mikoani na wala sifahamiki na kiongozi yeyote yule ndani ya chama huku nikitumia ID mficho ambayo hata huyo kiongozi hawezi kutambua mimi ni nani.
Ukitizama makala za Yeriko zilizokua zikimuhusu Lowasa kabla hajahama CCM makala ambazo zilimpinga na kumuona Lowasa hafai na ukilinganisha makala anazozitoa sasa zenye kumpamba kwa kila nakshi mtu yuleyule.
Mwenye akili anapaswa kujiuliza je ni kichocheo gani kimeweza kumsukuma kijana kama huyu kuiweka heshima na utu wake rehani hata kubadilisha makala na kuanza kumsifia mtu yuleyule ambaye mwanzo alimwita hafai?
Ni yapi maslahi binafsi wanayapata vijana wa mithili yake ambao wameonekana kutetereka kimsimamo ghafla na kuanza kumtetea Lowasa ambaye mwanzo walimpinga hadharani?
Ni kijana yupi alipaswa kuhisiwa vibaya kwa kupata malipo kati ya vijana wa aina hii ukilinganisha na vijana wa CCM?
Ni vema kuanzia sasa ikafahamika ni uzalendo kwa chama na taifa letu ndio unaotusukuma na si pesa ama cheo kama inavyo zushwa humu mitandaoni.
Na pia lazima ikafahamika nje cha vyama vya siasa kigezo pekee cha kua mtumishi wa uma ni taaluma na si kadi ya chama.
 
Back
Top Bottom