Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Huu ujinga wanaotaka kuufabya utagharimu wengi, haiwezekani nimeacha kazi na michango yangu mbaki nayo nyinyi mpaka niwe babu? Wakitaka kukaa na hela zetu watulipe faida watakayoipata kwenye biashara wanazofanyia hela zetu, mfano kwenye majengo waliyojenga nikitaka frem au chumba wanipe tukatane kwenye hela yangu
 
hahahah... ilianzishwa 2012 ila naona yaliyoazimiwa miaka hiyo hayakutekelezwa... sasa JPM kaingia... yanatekelezwa
 

UPDATES KUHUSU JAMBO HILI 17th June 2016


-Ndugu zangu salamu sana, mimi ni muhanga wa jambo hili

-Niliacha kazi Kwa hiari yangu mwezi wa nne 2016, na nilikuwa napelekewa michango yangu PPF

-Plan yangu ilikuwa nichukue kiinua mgongo changu nilale mbele nianze baishara tu baada ya kuhudumu miaka 3 kama muajiriwa kampuni moja

-Tarehe 13 May 2016 Nilifika PPF Arusha katika jengo lao jipya linalotizamana na hospitali ya AICC, lengo langu ni kupeleka vielelezo vyote muhimu (vya kuacha kazi, barua ya muajiri wangu etc) ili nianze mchakato wa kupata visenti vyangu nisonge mbele. Nilipofika pale ghorofa no 3 ambapo ndipo ofisi za PPF zilipo katika hilo ghorofa nilikutana na mdada mmoja mweupe hivi mnene kiasi yupo kitengo cha mapokezi, nilipompa zile fomu zangu, akazipokea akazikagua akasema ziko sawa LAKINI akasema tena
:"Tumezuiwa tangu May 12 kutoa pesa kwa hili fao la kujitoa",Nikamwambia kwanini?? Mbona sisi wadau hatuna taarifa?? Akasema taarifa zilitolewa katika vyombo vya habari na hivyo hizo pesa ntazipata baada ya miaka 50 (Umri wa kustaafu), na hata nikifa eti familia yangu itaenda kuzidai hizo fedha eti Sheria imeshasainiwa juu ya jambo hili, na sababu kubwa ni kuwa eti wazee huwa wanateseka sana punde wanapostaafu..Alieleza kuwa hiyo ni sheria rasmi imepitishwa na mifuko yoote inapaswa kuanza kutekeleza agizo hilo, akasema wao PPF wameanza na mifuko mingine inajiandaa kufuata.. kwa kweli huyo dada alinipigia blah blaahh nyingi sana zilizonipandisha hasira tu nikaondoka na fomu zangu

Mifuko hii ni hatari sana kwa ustawi wa private sekta, maana mikataba ya hii sekta haitabiriki (leo mradi/shirika lipo kesho halipo, mikataba ni miezi 3-mwaka 1, kila mwaka kuna kurenew mkataba etc), na mbaya zaidi maamuzi ya mifuko hii kuhusu matumizi ya pesa zitokanazo na pesa za wanachama tunaoichangia hatushirikishwi. Maamuzi ni ya top down approach.Inaumiza sana pesa ni yako umeitolea jasho, wanakukata na ukitaka kuichukua ndio unakutana na vigingi kama hivi, na mbaya zaidi hata utakapoipata hiyo pesa hainaga riba zaidi ya yote utakuta imepigwa kodi tena, hivyo makato yanakuhusu achilia mbali value for money kwa wakati huo utakapoipata.

Tarehe 9/06/2016 nilienda kwa shughuli zangu jijini Mbeya.Nilipofika Mbeya nikasema ngoja niende tena kujaribu bahati yangu PPF (Ofisi zao zipo mtaa wa Uhindini pembeni kidogo ya PB sheli ya mafuta kabla ya kufika jengo la NMB. Ofisi zao zipo ghorofa la 3 katika hilo ghorofa, hapo nilikutana na mdada mmoja mwembamba hivi na jamaa mmoja anaitwa Mwakiselele (kama sijakosea). Nilipowaeleza shida yangu wakaniambia
"Tumezuiwa kupokea fomu za kujitoa na hakuna malipo juu ya fao hilo mpaka baada ya miaka 50, wakadai wameagizwa hivyo-hivyo wanasubiri tamko rasmi la bodi yao ambayo itakaa tarehe 16/06/2016",Kwa kweli niliumia sana, nikawaza hatma ya senti zangu nikaona tayari hapa nimewafaidisha watu, na watu wanakula jasho langu waziwazi. Jambo la kushangaza ni kuwa ukiwa unapanda ngazi kuelekea ofisini kwao chini kuna bango lao ambalo mpaka leo linaonyesha fao la kujitoa bado lipo.

KWA HIYO NAWEZA KUWATHIBITISHIA WANA JF KUWA SUALA HILI NI SERIOUS NA KWA PPF AMBAKO MIMI NIPO, NI KWELI HAKUNA MALIPO YANAYOTOLEWA KWA SASA JUU YA FAO HILI, HIVYO TUSUBIRI MIAKA 50

========================================================================================


Mbona naona ni ya tangu 2012
 
aisee haya mambo yanatia hasira sana.. nchi za wenzetu wanaojitambua yangekuwa maandamano kabambe kwa ujumla wao especially kundi la wafanyakazi.. hapo vyama vyetu vya wafanyakazi vimelala havina muda na maslahi ya wafanyakazi.. inatia uchungu sera kandamizi kama hizi ambazo ni kichocheo cha umaskini.. i wish another general election ingekuwa next month.. poleni mnaodai chenu
 
aisee haya mambo yanatia hasira sana.. nchi za wenzetu wanaojitambua yangekuwa maandamano kabambe kwa ujumla wao especially kundi la wafanyakazi.. hapo vyama vyetu vya wafanyakazi vimelala havina muda na maslahi ya wafanyakazi.. inatia uchungu sera kandamizi kama hizi ambazo ni kichocheo cha umaskini.. i wish another general election ingekuwa next month.. poleni mnaodai chenu
Hivi hii insu nilisikia inapelekwa bungeni ndiyo imepita au ni vipi? Au kwa kuwa wapinzani hawapo, du hatari kabisa sijui tutaponea wapi hii mfuko ni wezi, inatakiwa kila mtu atoke na chake, walio karibu na hii mambo hebu fafanueni, wanataka kutupiga ile mbaya, nasikitika Sana kwani mimi ni muhanga wa hili fao nilitaka nijitoe sasa hari kama ni hii hatari. Nimeishiwa hadi maneno ya kuandika.
 
Unajua hili suala si la leo wala jana, it seems awamu ya 4 waliliona na athari zake na vilio wakaliacha pending, so it was a dormant ishu way back 2011, sasa hii awamu ya papara wameliparamia kwa shabaha maalumu wanayoijua wao pasipo kulifanyia review yakinifu
 
Kwenye gazeti la leo la jambo leo Kuna habari inahusu mfuko mmoja wa kijamii wa PSPF, kwamba uko hoi kifedha, wakaenda mbali zaidi wakasema umeathiliwa na uchaguzi wa mwaka jana, unahangaika kuwalipa wastaafu, sasa kwa Hali hii wanaodai fao la kujitoa lazima wazinguliwe, nafikiri SSRA inatumia njia hii kurescue situation ya mifuko hii ina hari mbaya kifedha, kwa hiyo inalazimisha watu wasijitoe ili watengeneze pesa kwanza, yaani inauma ile mbaya kwa sisi walala hoi, ukifukuzwa kazi basi uende unahangaika, hata kuazisha kamradi ushindwe huku unafedha yako wamekalia watu fulani, na vitu wanavyojitete havina maana kwani wanasema mtu akijitoa anaenda kuishi maisha magumu lakini hawajatupa utafiti waliofanya na kufuatilia watu walio jitoa kwenye hiyo mifuko, wanafanya kazi kwa hisia , ili tukubaliane na matakwa yao, yaani mimi binafsi nimeshitushwa na hii mambo.
 
Back
Top Bottom