Hakuna Maendeleo Bila Kubadilika

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Tulifundishwa kuwa maendeleo ni mabadiliko toka hali duni kwenda iliyo bora maana yake ni mabadiliko kutoka mbinu hafifu kwenda mbinu zilizo bora, kutoka uzalishaji duni kwenda kwenye uzalishaji bora, kutoka teknolojia duni kwenda teknolojia ya juu, kutoka utendaji mbovu kwenda kwenye utendaji makini, kutoka kwenye uzembe kwenda kwenye bidii, kutoka kwenye kuiga na kwenda kwenye ubunifu, n.k.

Kama tunataka kusonga mbele kuna mambo ya kuyatenda mara moja. Bahati nzuri mengine tayari yameanza kufanywa na serikali iliyopo lakini mengi bado. Haya ni lazima yafanyike kama hatua ya awali:

1) Usimamiaji mzuri wa matumizi ya mapato ya serikali - linafanyiwa kazi

2) Uimarishaji wa misingi ya demokrasia na kuheshimu uhuru wa raia ili wananchi waungane kwa lengo moja la kujenga nchi yao. Uchafu ule uliofanyika Zanzibar utafutiwe suluhisho haraka

3) Usimamiaji mzuri wa ukusanyaji kodi za serikali kwa njia rafiki

4) Kuhakikisha kuna watu wenye uwezo na ubunifu TRA ili kuepukana na mawazo duni kuwa ukiweka kodi nyingi na kubwa ndiyo mapato ya serikali yanaongezeka. Kodi utititiri na kubwa zinadidimiza uwekezaji na ukuaji wa uchumi. Nchi kama Dubai, Hong Kong zimeendelea haraka kutokana na kuwa na kodi ndogo. Kodi ndogo kwa Tanzania kutaifanya Tanzania kuwa kuwa mahali pa kufanyia manunuzi kwa nchi nyingi majirani zetu

5) Serikali izungumze na waagizaji wakubwa wa bidhaa toka mataifa ya kigeni iwaulize ni lini wataanza kuzalisha Tanzania bidhaa hizo hizo wanazoagiza toka nje. Iwasaidie waagizaji hao wa bidhaa toka nje ili wawe wazalishaji

6) Wazalishaji wa ndani ambao uzalishaji wao ni mdogo waitwe wazungumze na serikali ili kujua ni nini kinawazuia kuwa wazalishaji wakubwa. Kama tatizo ni mtaji wasaidiwa kupata mitaji kwa serikali kuwekeza katika makampuni hayo na baadaye wafanyakazi na wananchi wengine wanunue hisa za serikali. Kama tatizo ni soko, kwa bidhaa ambazo serikali ina uwezo wa kuzitumia, serikali inunue bidhaa kutoka kwa wazalishaji wa ndani

7) Serikali na taasisi zake zote, walazimishwe kununua mahitaji yao kutoka kwa wazalishaji wa ndani isipokuwa pale tu ambapo hazipatikani. Wazalishaji wa ndani wasaidiwe katika kuongeza ubora wa bidhaa zao

8) Rais na wote wenye mamlaka waepuke kabisa teuzi za nafasi mbalimbali kama zawadi kwa misimamo ya kisiasa au urafiki na undugu uliopo baina yao

9) Serikali ijenge mifumo imara ya kitasisi inayoweza kusimamia kila jambo ili utendaji kazi kwa misingi ya uadilifu na weledi uwepo wakati wote bila ya kujali nani amekuwa kiongozi mkuu
10) Serikali ijenge mahusiano mazuri na jamii ya kimataifa ikiwemo wahisani wetu wa miaka mingi. Bado tunawahitaji ili tuweze kujitegemea kwa haraka, la muhimu ni kutambua kuwa kila msaada tunaopewa utuelekeze kwenye kujitegemea kuliko kutufanya kuwa watu wa kusaidiwa milele

10) Msingi wa yote ni Katiba nzuri. Rasimu ya katiba ya Warioba, yenye mapendekezo yenye hekima toka kwa wananchi iwekewe utaratibu wa kujadiliwa upya baada ya kuchakachuliwa na watu wachache wasio na nia njema na Taifa letu.

11) Watanzania tuache kuangalia na kuhamasisha tu mabadiliko ndani ya serikali, nasi katika maisha yetu kuna mengi tunastahili kuyabadilisha. Katika maisha yetu ukiona una tatizo na hupati suluhisho usiamini kuwa hakuna suluhisho bali wewe umeshindwa kuliona suluhisho.
 
Safi sana, lakin ujue kipengele namba 8 ndo silaha kuu kabisa ya chama tawala lakin pia ndo chimbuko la matatizo ya nchi hii.
 
Back
Top Bottom