Hakuna laana kubwa kama kuichagua CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna laana kubwa kama kuichagua CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 27, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Kama kuna laana kubwa watanzania itaendelea kuwasakama mpaka mwisho na hakuna matatizo yatakayowaisha hata aje kuhutubia papa Benedicto ni laana ya kuichagua CCM madarakani.

  Najua wapo wasioamini lakini ukweli halisi ni huo kwamba haya matatizo yote mnayoendelea kupiga kelele mara unyanyasaji,ufisadi,albino ni kutokana na laana za ya kuichagua CCM.

  Kama kweli unataka kuondoa laana ya mkosi kwenye familia yako usichague kabisa CCM vinginevyo ndoa zenu zitaota mbawa bila kujua chanzo nini nini kumbe jibu unalo.

   
 2. F

  Falconer JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Asante sweetbaby, Hakika umenikosha leo. Wambie wajue kuwa hiki ni chama uozo kabisa kheri ya chadema mara elfu. CCM ni mzoga kila pakiwa hapakosekani mafisi. Mwisho wakre ndio huu. watanzania amkeni kumekucha.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Nov 28, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  At least we are missing threads of this type, watu wanahangaika usiku na mchana mara EL, geuka huku CHENGE, kidogo RA, mara JK....Mkapa,,,, name it

  Jumla ya yote hayo NI CCM WOTE ....waondoke thats all,

  focus iwe kuijenga Tanzania mpya, kutayarisha vyama vizuri vyenye mawazo mapya ya kizalendo sio hivi tulivyo navyo sasa!

  Tuwakomalie hawa wapinzani wabadilike wasijali matumbo yao wala kuanzisha NGO

  CCM donda ndugu, haliponi jamani
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wishful thinking!
  Wanaosema wengi lakini it is mere lip service.Na waliojitokeza wakipenyezewa rupia maneno ya utata kibao.
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Nov 28, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  wapiga kura wanatuangusha sana, ila kwasababu wasio piga ni wengi kuliko wanaopiga, lazima tufanye mikakati mizito kuwawin hawa waliovumjika moyo kufikia kususa kupiga kura maana wengi wao ni waelewa, wanahitaji somo kidogo tu.
  Mungu tutie nguvu tuweze kukabiliana na hawa CCM Wezi wa kura.
   
 6. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 789
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 80
  Nguvumali, wapiga kura ni wananchi wengi masikini wasiojua kusoma na kuandika , kwanza kwenye kupiga kura wanaletewa mtu wa kuwasaidia kuzipiga hizo kura na sahihi zao ni vidole gumba! what do u expext??hapa hapa Dar kwa mfano wananchi wengi wameridhika na maisha waliyonayo mtu akiwa na mia hamsini ya kula andazi linalouzwa barabarani tandika ameridhika!! unafikiri tutaiondoa ccm madarakani?? kwa kifupi wananchi wako stagnant hawajui kukasirika, in short tunaudhi kuliko maelezo!! angalia uchaguzi wa mitaa uliopita utakubaliana na mimi, mbali na kashfa zote ccm ilizokuwa nazo za ufisadi bado wameshinda kwa kishindo???! saa nyingine nakasirika kuwa mtanzania. yaani sisi wenyewe ni laana na ndiyo maana tutaipitisha ccm tena.
  Binafsi naamini hakuna chama kilicho tayari kwa kushika dola hata hao chadema wenyewe ila kutoa fundisho kwa ccm ni muhimu, yaani kuwanyima kura ili wajirekebishe.
  Lakini bado nasema watanzania wengi hawajui kusoma hivyo tusitegemee critical thinking ya mambo,wakija kudanganywa na miradi ya visima na barabara za kokoto wakati wa kukaribia uchaguzi wanasahau kwamba wana tanzanite arusha, urenium mbeya, gesi, makaa ya mawe, dhahabu, almasi...........ambavyo ni sababu tosha ya wao kutokuwa masikini kama viongozi wengesimamia vizuri.
  Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
   
 7. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi Nguvumali. Ushindi wa CCM unachangiwa pia na wasiopiga kura.

  Toka nimetua hapa bongo, kama mwaka hivi sasa, ninajaribu sana kudodosa wabongo. Wengi wao wamechoshwa na CCM. Hawajasema kama upinzani hauko tayari, ila kwamba hata wakiwachagua upinzani, CCM wataiba hizo kura. Hiyo ndio sababu yao kuu. Mimi binafsi siiamini sana.

  Watanzania chagueni upinzani badala ya CCM. Angalia signature yangu hapo chiini.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Nov 28, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Watanzania vilaza watamchagua Kikwete aendeleze ubabaishaji ikulu kwa awamu nyingine - Tafakari
  huo ni ujumbe maridhawa
   
 9. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ndugu vipi tena umekata tamaa au? na siasa za chadema

  JK hana urais kama tume itakuwa huru..i can assure you...watanzania tuungane tulinde kura zisiibiwe kutakuwa na mabadiliko makubwa sana 2010

  lakini makubwa zaidi 2015 the end of CCM.
   
 10. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  wapiga kura wanatuangusha sana, ila kwasababu wasio piga ni wengi kuliko wanaopiga, lazima tufanye mikakati mizito kuwawin hawa waliovumjika moyo kufikia kususa kupiga kura maana wengi wao ni waelewa, wanahitaji somo kidogo tu.
  Mungu tutie nguvu tuweze kukabiliana na hawa CCM Wezi wa kura.

  CCM haifai tena kupewa nafasi ya kushika dola tatizo wasomi wengi wanaganga njaa, heri wananchi wasiojua kusoma na kuandika maana siku wakijua watabadilika.

  wasomi wanajua ubaya wa CCM lakini kusema ukweli kuhusu hilo ni mwiko. Zaidi tunaona wengi wanahangaika kujiunga na CCM ili mambo yao yanyoke.

  Wananchi wengi kutokana na uelewa wao mdogo wamedaganyika sana na propaganda za CCM.

  Mabadiliko yanakuja
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  sisiemu baibai 2010
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kila mtu anataka mabadiliko. Sio siri CCM kina wezi, ingawa ni wachache lakini ndio wenye influence kwenye chama, na ndio wenye nguvu, lakini swali linakuja nani aje badala ya CCM?

  So fara upinzani wanaonekana kuwa bado hawajajipanga. Na inaonekana tayari mafisadi wameanza kutumia janja ya kuwatingisha na kuwanunua, tumeshaanza kusikia migogoro chadema, NCCR ndio imekufa, CUF bado ina nguvu zanzibar bara ni kama haina kitu.

  Bado kuna asilimia kubwa ya watu wanaweza kuwapigia kura mafisadi kwa kuhongwa pilau, khanga, sukari au hata bia. Kuna wengine bado wakataa kuwapigia kura opposition kwa kuwa tu opposition ni opposition.
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kuota mchana sio dhambi
   
 14. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sisi tulio vijijini tunatarajia nyie mlio dsm mtuonyeshe njia maana magazeti mnasoma, na wengi ni wasomi; lakini nimeshangaa takwimu za waliojiandikisha na kupiga kura dsm katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Hivi kweli mnatarajia mageuzi yaanzie vijijini? Mmetuangusha. Katika kata yangu tumepata wenyeviti wa vijiji 2 wa CUF na ccm mmoja, kata ya jirani tumepata vijiji 2 Chedema na ccm kimoja. Tungepata hivyo dsm tungekuwa tunazungumza mengine.
  Mijini mmekata tamaa, mageuzi atayaongoza nani kutokea kijijini? Wakeup!
   
 15. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hizi fikra ndiyo sikubaliani nazo. Hivi unadhani hakuna anayeweza kuongoza ila CCM tu? Hata wewe unaweza ali mradi dhamira yako iwe ni kuwatumikia wananchi. Nakuhakikishia ukiwa na dhamira safi utaona wananchi wanakuunga mkono na kila kitu kitaenda vizuri.
  Unafikiri kwa nini watu wanakwepa kodi? Ni kwa sababu hawana uhakika kodi zao zinatumiwaje!
  Kwa nini watu wanapiga kelele za ufisadi na kutowaamini viongozi wao? Ni kwa sababu viongozi wamewageuka wananchi na kuanza kuwatafuna!

  Wewe ukijiepusha na mambo hayo, utaweza kutuongoza tu. Nchi hii ni tajiri sana, huhitaji miujiza kuwatoa wananchi katika umaskini!!!!
   
 16. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wewe wakikusikia House negro wa kibogo utakiona
   
 17. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe 100 kwa 100. kazi kweli ipo wasiopiga kura wako wengi sana, kuna dada mmoja nilimpa lifti akaniambia kuwa hapigi kura tena kwani hana imani na system. Nilichofanya nilihakikisha kuwa nampa lifti kila siku halafu nikawa nampa somo, juzi kaniambia kuwa atapiga kura
   
 18. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hakuna laana yoyote, CCM ni nambari one na chama mama.
   
 19. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2009
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kukiwa na tume huru ni rahisi CCM kuondoka Zanzibar na Zanzibar kupata maendeleo lakini sio Bara! Ukitathmini matokeo ya chaguzi za serikali za mitaa, utatambua kuwa CCM inachukiwa JF tu sio na wananchi ambao imewafanya maskini wa kutupwa! Wabara mtaendelea kuumia mpaka mtakapotambua CCM ndio wanaofanya mahoheha wa kutupwa mpaka wakina mama wazazi wodini Temeke walale sakafu na wamlize Naomi Campbell!
   
 20. M

  Molembe JF-Expert Member

  #20
  Jun 10, 2014
  Joined: Dec 25, 2012
  Messages: 7,759
  Likes Received: 4,266
  Trophy Points: 280
  Ccm ni chama chenye laana hivyo kukichagua ni kuchagua laana miaka 53 nchi imeliwa imebaki mifupa, watanzania wanaishi kwenye umasikini uliopindukia pamoja na nchi kuwa na rasilimali nyingi ambazo zingetumika kunufaisha wananchi husika.
  Huduma za kijamii ni mbovu
  Elimu ambayo ingetumika kumkomboa mwananchi wameiua makusudi ili waendelee kututawala
  Rushwa imekithiri masikini hana haki hata watoto wa masikini wameishia kuwa walimu maana kwingine hupati kazi bila rushwa na kujuana,
  Kibaya zaidi deni la Taifa linapaa hivi hiyo mikopo inafanya kazi au mnakopa mje kulipana posho
  NAKULILIA NCHI YANGU.
   
Loading...