Hakuna Kwetu Kwingine...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
1. Hakuna kwetu kwingine, kwanza nawasalimia,

Hakuna kwetu kwingine, ujumbe nawaambia,
Hakuna kwetu kwingine, wa Kijiji naingia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

2. Hakuna kwetu kwingine, hata tukiwa Asia
Hakuna kwetu kwingine, tukiwa na Arabia,
Hakuna kwetu kwingine, Na nchi za Yuropia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

3. Hakuna kwetu kwingine, na siye wa Amerikia,
Hakuna kwetu kwingine, na popote Afrikia,
Hakuna kwetu kwingine, katika hii dunia,
Hakuna kwetu kwingine ila kwetu Tanzania.

4. Hakuna kwetu kwingine, kwetu kwa kupigania
Hakuna kwetu kwingine, kwetu kwa kung’ang’ania,
Hakuna kwetu kwingine, kwetu tusikochukia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

5. Hakuna kwetu kwingine, tunakokushabikia,
Hakuna kwetu kwingine, tunakokuulizia,
Hakuna kwetu kwingine, tunakokufuatilia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

6. Hakuna kwetu kwingine, kwingine kwetu na pia,
Hakuna kwetu kwingine, kwetu tusikogaia,
Hakuna kwetu kwingine, Ni Bongo nawaambia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

7. Hakuna kwetu kwingine, sababu ya kubishia,
Hakuna kwetu kwingine, hivyo twawang’ang’ania,
Hakuna kwetu kwingine, kamwe hatutaachia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

8. Hakuna kwetu kwingine, kwetu kwa kushabikia,
Hakuna kwetu kwingine, kwingine kwa kuchangia,
Hakuna kwetu kwingine, chochote tukipatia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania.

9. Hakuna kwetu kwingine, utawalaye sikia!
Hakuna kwetu kwingine, ukweli tutakwambia,
Hakuna kwetu kwingine, na hata ukichukia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania,

10. Hakuna kwetu kwingine, hata mkitutishia,
Hakuna kwetu kwingine, hofu haitoingia,
Hakuna kwetu kwingine, bado tutawashukia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

11. Hakuna kwetu kwingine, mafisadi mtalia,
Hakuna kwetu kwingine, vikaragosi vyenu pia,

Hakuna kwetu kwingine, hadi mje kukimbia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

12. Hakuna kwetu kwingine, beti zangu zatimia,
Hakuna kwetu kwingine, ni dazeni siyo mia,
Hakuna kwetu kwingine, nafunga na kutulia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Tarumbeta ya Kijiji)
 
Kwetu kwangu ni popote, mambo yakininyookea,
Kwetu mtu si chochote, wezi wanajiibia,
Kwetu sioni lolote, ni jina limebakia,
Ingawa kwetu ni kwetu, kwetu kwangu ni popote.

Kwetu niwe mkimbizi, wageni wawe wenyeji,
Hili hujalimaizi, hebu jaribu kuhoji,
Kwetu ilikuwa enzi, kwa sasa sina uenyeji,
Ingawa kwetu ni kwetu, kwetu kwangu ni popote.

Leo sitasema mengi, kwani si mahali pake,
Jambo moja la msingi, yabidi tubadillike,
Kwetu kweli kwa msingi, tupambane pakomboke,
Ingawa kwetu ni kwetu, kwetu kwangu ni popote.
 
Kwetu kwangu ni popote, mambo yakininyookea,
Kwetu mtu si chochote, wezi wanajiibia,
Kwetu sioni lolote, ni jina limebakia,
Ingawa kwetu ni kwetu, kwetu kwangu ni popote.

Oh Yes! Great Mkuu! Naungana na mchangiaji mwingine kwamba Shaaban Robert hajafa umeondoka mwili tu bali mwawazo yake yanaishi. Mwanakijiji nimemgongea pia like kule juu. Kumbe fasihi na sanaa vikitumiwa vizuri vina nafasi muhimu katika jamii si kama burudani tu bali pia ukombozi. Thanx you guys.
 
Mwanakijiji sikia , maneno yenye hekima
Maisha ni kutulia, popote penye hatima
Mrume acha kulia, vita si lelemama
Mwanajeshi makini; vita kasimamia

Wajitia uhayawani, usiozaliwa nao
Rudi zako mkoani, kijana mtu wa kwao
Tanga ni burudani, maisha kwa raha zao
Mwanajeshi makini, vita kasimamia

Mangula yupo mahiri, ccm ameishika
Mafisadi wamekiri, vilio vimewashika
Namalizia shairi, maneno yangu hakika
Mwanajeshi makini, vita kasimamia
 
Kwetu ni kwako, njia kutayarisha
Kwako ni kwetu, ujio kutamanisha
Kwao ni kwetu, nauli kuchangisha
Kwetu ni kwao, pokezi kuhamasisha

Karibu jisogeze, mgeni wetu kusitirika
Ndani jizoeleze, fungua mema kutiririka
Ahueni ichomoleze, wabaya wote kuathirika
Karibu jisogeze, nyumbani nipa kuridhika

Ujio kuwadia, mashaka kuyaondoa
Ujio kutamania, umati kuukomboa
Ujio kutarajia, wabaya kuunong'onoa
Ujio kuwadia, twahamasika kana'ndoa

Tahadhari kukupatia, dunia haikosi mabaya
Tahadhari kuzingatia, kama ile dozi ya mawaya
Tahadhari imarishia, kunapo dume kupwaya
Tahadhari kukupatia, Mwanakijiji kutotugaya

Beti zaniponyokeka, tahadhari kuendelezesha
Bajaji huchomokea, kushoto kujichomezesha
Bodaboda huchomokea , kulia kujilengezesha
Beti zaniponyokeka, tamati kubembelezesha

Hakuna kwetu kwingine, mgeni unakaribishwa.

Na: Steve Dii (Mwangwi wa Handaki)
 
Nikipandadaladala
Nendapohospitali
Namaumivu makali
Toba!
Naonamisururu
Misururumisururu
Wamejazanawachovu
Wengikupita kiasi
Wenyemimba na wazee
Hatawatoto wa shule
Vibiyongona viwete
Wotewanajambiana
Surazimekunjamana
Sijamuonamtawala!
Kwenyehii misururu
Mienaona kefule
Ninakero ile ile
Swalilangu lile lile
Hivikweli hapa kwetu?
Kwelibabu aliishi hapa?
Aliishimama yangu?
Siaminisiamini.
Babamie siamini
Kwetuniteseke hivi?
 
Mjusi naye ni nani, analalahekaluni,
Muulize ni la nani, hajuikajenga nani!
Kuku naye ana nini, amchekeKanga nini,
Azalisha protini, ulizaalacho nini?

Naye mbwa ana nini, mlinzial'o makini,
Alinda mamilioni, hana kitumfukoni,
Kufuli naye ni nani, kutwakucha mlangoni!
Muulize kilo ndani, hajawahilala ndani!

Nawe kuwadi u nani,uambuliacho nini?
Hukipati cha mezani, chakowaokota chini!
Kaiulize sahani, inaunguakwanini,
Kijiko yumo kundini, hajuitakula lini!

Jiulize wewe nani, nafasiyako ni nini?
Hali hiyo ni kwanini, nchihii ni ya nani?
Jichungue wewe nani, tenawamiliki nini,
Ipi ni nafasi yako, ni mjusihekaluni?

Mkabala wako nini, na zamuyako ni lini,
Wangojea mpaka lini, liniitakuja lini?
Ukingoja hiyo lini, mwanaoangoje nini!
Ipi ni nafasi, ya kufulimlangoni?

Utachokosa ni nini,utapohihoji lini,
Jembe lisilompini, lawezakufaa nini,
Karatasi ni ya nini, iwapohauna peni?
Gari litafaa nini kamahalina injini?

Shuka hufaidi nini,kumfunika fulani,
Zamu yake siku gani,liuchape kitandani,
Mfuko huweka nini, kunachake mle ndani,
Pambo hufaidi nini, litapatamacho lini?

Kiatu u mguuni, wewe utavaalini,
Tinga tinga hupatani, linabarabara gani?
Nalo zamu yake lini,ataliruhusu nani,
Ulitazame kazini, utaumiamoyoni.

Mpiga kura ana'ni, namchaguliwa nini,
Mheshimiwa ni nani,mdharauliwa nani?
Jama sifanye utani, mwenzenunimo kizani,
Jibu lifikirieni, mliwekematendoni.

Hivi inzi na kunguni, naniamcheke nani,
Huyu ala jalalani, yule alamaungoni,
Wanachokula cha nani,wanachochangia nini?
Mbona wote hayawani, aliye borani nani?

Pete na kidole nani,alonunua ni nani,
Pete hufaidi nini, raha yakidole nini,
Wa ndani hupata nini, wa njeakosa nini,
Fikirini si utani, nafasiyako ni nini?
Hapa ndipo kituoni,nimepagawa kichwani,
Narejea darasani, nendamambo kubaini,
Nijue nami ni nani, niambiweni kwanini,
Nitarejea ugani, nijuewenzangu nani.
 
Chako ni chako jamani, hata kama maskini
Kikiwemo mfukoni, au uchimbie chini,
Kiwe cha kubwa thamani, au bei magirini,
Ni chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Nyumba ya kwako ni yako, hata iwe msituni,
Ya kwake siyo ya kwako, hata iwe ni peponi,
Ya kuazima si yako, hata kama ghorofani,
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Kilicho chako cha kwako, hata watu wakucheke
Kidogo bado ni chako, wala usidanganyike,
Usiachie cha kwako, hata lije libeneke,
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima

Mwizi kaingia ndani, kwenye nyumba ya kwako,
Utahamia uani, eti ni yake si yako?
Au wende kwa jirani, useme nyumba si yako?
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Nyoka umkute ndani, kwenye uvungu chumbani,
Utahamia jikoni, umuache kitandani?
Hutamtoa jamani, na kumpiga kichwani?
NI chako hicho ni chako, cha kwako si cha kuazima.

Cha kwako bado cha kwako, hata kibovu watani,
Kizima kisicho chako, wakitamani kwa nini?
Tengeneza kilo chako, ujivunie moyoni,
NI chako hicho ni chako, cha kwako si cha kuazima.
 
Kumbe kweli! Mtu chake apendacho,hakina hila machoni,huridhika kuwa nacho,japo hakina thamani!
 
...

12. Hakuna kwetu kwingine, beti zangu zatimia,
Hakuna kwetu kwingine, ni dazeni siyo mia,
Hakuna kwetu kwingine, nafunga na kutulia,
Hakuna kwetu kwingine, ila kwetu Tanzania

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Tarumbeta ya Kijiji)

Kama tangu mapema mngefanya AFRICANIZATION ningekuelewa
 
Mwanakijiji nimekukubali mkuu. Kazi nzuri.

Chako ni chako jamani, hata kama maskini
Kikiwemo mfukoni, au uchimbie chini,
Kiwe cha kubwa thamani, au bei magirini,
Ni chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Nyumba ya kwako ni yako, hata iwe msituni,
Ya kwake siyo ya kwako, hata iwe ni peponi,
Ya kuazima si yako, hata kama ghorofani,
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Kilicho chako cha kwako, hata watu wakucheke
Kidogo bado ni chako, wala usidanganyike,
Usiachie cha kwako, hata lije libeneke,
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima

Mwizi kaingia ndani, kwenye nyumba ya kwako,
Utahamia uani, eti ni yake si yako?
Au wende kwa jirani, useme nyumba si yako?
NI chako hicho ni chako, chako si cha kuazima.

Nyoka umkute ndani, kwenye uvungu chumbani,
Utahamia jikoni, umuache kitandani?
Hutamtoa jamani, na kumpiga kichwani?
NI chako hicho ni chako, cha kwako si cha kuazima.

Cha kwako bado cha kwako, hata kibovu watani,
Kizima kisicho chako, wakitamani kwa nini?
Tengeneza kilo chako, ujivunie moyoni,
NI chako hicho ni chako, cha kwako si cha kuazima.
 
Bravo Mzee Mwanakijiji!!

Last edited by a moderator:

Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom