Hakuna kutaja majina mpaka uhakiki, je waliotajwa majina nani kawahakiki?

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Wadau juzi Mwenyekiti wa Baraza la Madawa ya Kulevywa Nchini Mh.Waziri Mkuu Majaliwa wakati akizindua Baraza hilo alisema no marufuku kumtaja MTU jina mpaka Ahakikiwe.Swali langu ni je wale ambao Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.Makonda aliwataja Walihakikiwa? Na kama ndio nani aliwahakiki? Na kama hawakuhakikiwa ilikuwaje wakatajwa majina yao?Je Sheria inasemaje kumtaja MTU bila uhakiki? Adhabu yake Kwa alitenda kosa hilo ni nini?
 
Katazo la kutotaja hadi pale itakapo hakikiwa, limeanza kufanya kazi kuanzia pale siku waziri Mkuu alipo tamka.
Au kwa lugha nyepesi ni kwamba, yaliopita si ndwele
 
Watajitetea kwamba katazo limeanza kufanya kazi baada ya PM kwahiyo nyinyi wengine kafieni mbele.

Hapa nakumbuka sheria yao ya namna wanufaika wa mkopo wanavyotakiwa kuilipa bodi, hiyo sheria imemgusa hata aliyemaliza miaka minane nyuma, na TLS wapo tu.
 
Wadau juzi Mwenyekiti wa Baraza la Madawa ya Kulevywa Nchini Mh.Waziri Mkuu Majaliwa wakati akizindua Baraza hilo alisema no marufuku kumtaja MTU jina mpaka Ahakikiwe.Swali langu ni je wale ambao Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.Makonda aliwataja Walihakikiwa? Na kama ndio nani aliwahakiki? Na kama hawakuhakikiwa ilikuwaje wakatajwa majina yao?Je Sheria inasemaje kumtaja MTU bila uhakiki? Adhabu yake Kwa alitenda kosa hilo ni nini?
Kukaribisha rushwa tu na vita ishakoma hii
 
Back
Top Bottom