Hakuna kusita, Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi ivunjwe

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
maggid_0.jpg



Hakuna kusita, Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi ivunjwe











Maggid Mjengwa

7 Sep 2011
Toleo na 202










TUMESOMA kuwa, wanafunzi wapatao 14,000 wenye sifa za kujiunga na masomo ya elimu ya juu wamekosa sifa za kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Hii ni taarifa ya kusikitisha na inaonyesha kuwa wakati umefika kwa bodi hiyo kuvunjwa, na badala yake wanafunzi wenye sifa za kujiunga na masomo ya elimu ya juu wasaidiwe kupata mikopo kutoka kwenye mamlaka itakayotoa mikopo hiyo . Na katika hilo, Serikali iwe mdhamini mkuu wa chombo kitakachoundwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi na kuifuatilia kwenye malipo.
Ikumbukwe kuwa katika hotuba yake ya kukizindua rasmi Chuo Kikuu cha Dodoma Novemba 25, 2010, Rais Jakaya Kikwete aliahidi mambo makubwa mawili kama ifuatavyo, nanukuu:

Moja: “Kuhusu mikopo ya elimu ya juu napenda kuwahakikishia wazazi na wanafunzi kuwa tutaendelea kuongeza fedha katika mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike. Tumefanya hivyo katika miaka mitano iliyopita na tutafanya hivyo siku za usoni. Serikali iliongeza fedha za mikopo kutoka shilingi bilioni 56.1 mwaka 2005/06 hadi kuwa shilingi 237 bilioni mwaka 2010/11 na wanafunzi waliopatiwa mikopo hiyo wameongezeka kutoka 16,345 hadi 69,921. Haya ni mafanikio makubwa na naahidi kuwa tutafanya vizuri zaidi ili tuwafikie wanafunzi wengi zaidi.

Pili: Pia tutautazama upya mfumo mzima wa utoaji wa mikopo ikiwepo na utendaji kazi wa Bodi ya Mikopo kwa nia ya kuuboresha na kuleta ufanisi zaidi. Mawazo ya wadau wakiwemo wamiliki wa vyuo, wahadhiri na wanafunzi, yatasaidia sana”.
Na katika kutekeleza ahadi hiyo ya Pili, Rais Kikwete aliteua Tume ya wataalam 11 kufanya mapitio ya mfumo na uendeshaji wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini kwa lengo la kuimarisha utoaji wa mikopo hiyo. Tume ilitakiwa kufanyakazi kwa siku 60, kuanzia Februari 14, 2011 na kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi Aprili 15, 2011.
Mpaka kufikia sasa, ripoti husika juu ya kupata namna bora ya kutoa mikopo haijawekwa hadharani. Na tunakumbuka, kuwa Rais aliomba pia mawazo ya wadau. Kuna tuliotoa mawazo yetu. Na hapa tunayaweka tena wazi ili wahusika wayasome na kuona kama kuna ya kuyafanyia kazi.
Nilipata kuandika kuwa suala la wanafunzi wa vyuo vikuu kugoma sasa limekuwa ni la kila mara. Kwa sasa migomo vyuo vikuu si habari mpya; bali ni suala la lini utakuja mgomo mwingine baada ya mmoja kuhahirishwa au kuzimwa, kwa nguvu za dola. Ndio, kwa jinsi tunavyoenenda, hakuna dalili za migomo kumalizika bali ni kuzimwa na kuanza tena.
Suluhisho la muda mrefu linawezekana, kinachotakikana ni dhamira halisi ya kisiasa. Kwamba tuangalie upya utaratibu wa kulipia gharama za masomo kwa vyuo vikuu ili watoto wa makabwela waweze kupata fursa ya kusoma.
Tukubali kuwa hakuna tena kinachoitwa kuchangia elimu ya vyuo vikuu. Wakati umebadilika, gharama za kumhudumia mwanafunzi wa chuo kikuu ni kubwa mno. Mzigo huo hawezi kuachiwa mzazi, hauwezi kuachiwa Serikali pekee. Ni mzigo wa mwanafunzi mwenyewe, lakini asaidiwe kuubeba kwa kukopeshwa fedha za kugharamia elimu yake.
Mwanafunzi wa chuo kikuu ni mtu mzima, anapaswa kuwajibika kulipa deni la elimu itayomsaidia maishani mwake. Kinachotakiwa ni kufanya mawili yafuatayo;
Mosi, Serikali iandae utaratibu utakaoiwezesha kukopa fedha ili kulipia tuisheni ya mwanafunzi wa chuo kikuu. Tuisheni hapa ina maana gharama ambazo chuo husika kinahitaji kulipwa ili kiweze kutoa mafunzo stahili kwa mwanafunzi. Kwa mantiki hii, mwanafunzi hatalizimika kulipia gharama hizi isipokuwa zitalipwa na Serikali kutokana na mapato yatokanayo na kodi.
Pili, Serikali ivunje Bodi ya Mikopo na badala yake iunde chombo cha kukopesha wanafunzi ili wagharamie mahitaji yao ya msingi ya kila mwezi wa masomo ikiwamo malazi,chakula, usafiri na vitabu. Kiitengwe kiwango maalumu ambacho itakubalika kuwa kinamtosha mwanafunzi kulipia gharama hizo.
Mwanafunzi aliyepata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu atakuwa na hiyari ya kuingia mkataba wa kukopeshwa kila mwezi na chombo hicho au la, kwa maana ya kuamua kujilipia kwa msaada wa wazazi au ndugu na jamaa zake.
Mwanafunzi atakuwa anaomba fedha za kila muhula wa masomo na kuzipata kwa kila mwezi kupitia akaunti yake. Na ili afuzu kupata mkopo huo kwa muhula unaofuatia,mwanafunzi huyo atahitajika kuonyesha ripoti ya kiakedemia itakayothibitishwa kuwa amefaulu kwa kiwango kitakachokubaliwa kwa masomo ya muhula uliopita ili aweze kuendelea kukopesheka.
Mwanafunzi huyo atalazimika kuanza kulipa deni lake mara tu akipata ajira baada ya kumaliza masomo yake. Deni hilo litalipwa kwa kukatwa katika kila mshahara wa mwezi. Chombo hicho cha kuwakopesha wanafunzi kitatunza kumbukumbu za mwanafunzi na kitakuwa kikifanya kazi kwa mujibu wa sheria na kupewa uwezo wa kuwafuatilia wadaiwa wake na hata kuwafungulia mashtaka kama watashindwa kutimiza masharti ya mikopo hiyo.
Tukichukua muda wetu kuifanyia kazi kwa kina hoja yangu hii, basi, naamini inaweza kuwa muharobaini wa kuondokana na kinachoitwa migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu. Hii ni kwa sababu, kuna nchi tayari zenye mfumo kama huu na ambazo msamiati wa mwanafunzi kugoma haupo tena kwenye jamii zao.
Ni utaratibu utakaowapunguzia wazazi kero na hata chuki kwa Serikali yao kwa kuwabebesha mzigo wa kusomesha hata vijana wa vyuo vikuu ambao kimsingi ni watu wazima. Na hapa ndipo mchango wa Wabunge wetu unahitajika katika kuzifanyia kazi hoja za wananchi zenye kulenga kuwasaidia watoto wa makabwela, wanyonge wa nchi hii.
Watanzania hatupendi kuonyeshwa picha za kwenye runinga na magazetini jinsi wanafunzi wetu wakilazimishwa kufunga virago kurudi makwao. Huko nyuma kuna tuliowaona wakirudishwa kwa kuwa hawakuwa na sifa za kupata mikopo.
Kwamba hawakufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kama ni wavulana, na daraja la kwanza au la pili kama ni wasichana. Hakika ilitushangaza wengi wetu, kuwa vijana wetu wale waliondolewa vyuoni kwa mujibu wa sheria iliyounda Bodi ya Mikopo ingawa waliofungishwa virago walistahili kubaki chuoni na kupata mikopo ya bodi.
Na hapa ndipo tunapoona umuhimu wa kuwa na utaratibu mpya,maana huu wa sasa hautufai ikiwamo uwepo wa Bodi ya Mikopo. Kwa niaba yetu wananchi, waheshimiwa wabunge wetu wahoji; Je ni kwanini baadhi ya wanafunzi wenye sifa za kujiunga na masomo ya elimu ya juu wananyimwa nafasi hizo na kupangiwa madaraja ya kufaulu ili wapate udhamini wa serikali? Je, hatuoni kuwa jambo hili linaimarisha matabaka katika jamii na kwamba litazidi kuongeza pengo kati ya masikini na tajiri?
Iweje leo, miaka 50 baada ya uhuru wetu, kijana wa Kitanzania mwenye sifa ya kusoma elimu ya juu asipate nafasi hiyo kwa vile tu amefaulu kwa daraja la pili na amechagua kusomea biashara, uchumi, utawala, michezo na masomo mengine yasiyo ya sayansi au fani ya ualimu? Matabaka haya ni ya nini? Kila eneo la mafunzo katika chuo kikuu lina umuhimu wake kitaifa na kimataifa na ndio maana ya kufundishwa chuo kikuu.
Ndio, mfumo tulionao sasa una kasoro. Bila kuufanyia marekebisho, migomo vyuo vikuu itakuwa ni jambo la lini unakuja mwingine. Hali hii ikiendelea ina athari kubwa ya kiuchumi na kijamii kwa taifa letu. Tusiache iwe hivyo. Nahitimisha.
 
LIpo wazi mawazo yao wamekurupuka kwamba ufaulu wa daraja la 1 na 2 hakikuwa kigezo kwa mwaka 2011/12 kukopeshwa bali ni UHITAJI & VIPAUMBELE hata kama huna sifa ya ufaulu katika daraja la kwanza na pili unanufaika na mkopo, je hii ni Msingi Madhubuti wa kuwapata wataalam wanaostahiki?
 
Hii serikali inaongozwa na muhuni{jk}uctegemee mabadiliko yoyote.
 
Back
Top Bottom