The Collector
New Member
- Nov 3, 2010
- 3
- 0
Sasa tunakaribia mwisho wa matokeo na ni dakika yoyote toka sasa tutapewa ratiba ya kumwapisha JK, sio mbaya sana kwasababu amejiona yupo katika nafasi gani ndani ya mioyo ya watanzania, amejiona amefulia kwa kiasi gani, hii ni changamoto kubwa sana kwa CCM, inaweza ikasaidia wao kuwa na matimizo ya kweli ya ahadi zao angalau kwa asilimia ndogo.
Lakini kwa upande mwingine wapinzani, hasa chadema tumeweza kuonesha mwamko wa hali ya juu sana, nafikiri hili liliwatishia sana ccm amani yao katika uchaguzi huu, na vile vile natoa wito kwa wanachadema wote kuwa jamani 2015 sio mbali sana kama wengi tuonavyo, ni siku chache sana na hivyo tusilale kabisa mpaka kieleweke 2015 na ninaomba vijana wote wapenda maendeleo wajitokeze kwenye mchakato wa kugombea nafasi mbalimbali ili kuleta changamoto zaidi za kimaendeleo, tumekuwa shuhuda sisi wenyewe katika uchaguzi huu jinsi gani vijana wamekuwa na changamoto kubwa kwa wazee waliokuwa wamelowea madarakani, hii ni ishara nzuri sana ya mabadiliko ndani ya nchi yetu.
HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!