Tetesi: Hakuna Kuiendeleza M-Pesa MasterCard.

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,504
646
Inasemekana kwamba kwa sasa M-Pesa MasterCard inapoExpire hakuna tena kuiendeleza kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, na hii ni baada ya kujaribu kuiendeleza Card yangu iliyoExpire baada ya mwezi wa tisa kuisha, na majibu yalikuwa hivi, "your card has been un-suspended successfully" lakini nilipojaribu kuweka hela majibu yaliyokuja ni kwamba "Your Card is expired"

Nikachukua hatua ya kuwasiliana na huduma kwa wateja nikaambiwa hivi,

"Pole sana kwa hilo. Tunapenda kukufahamisha kwamba kadi ikiisha muda wake hauwezi kuiendeleza bali unatakiwa ufungue kadi mpya na kama kadi ya zamani ilikua ina hela unatakiwa kuzihamisha zote. ^OM"

Kuna swali niliuliza lakini mtoa huduma bado hajasoma meseji.

Sasa naomba kuuliza;

Kama mtu alifanya manunuzi mtandaoni lakini mzigo haukufika na muuzaji akataka kumrudishia hela itakuwaje? Je utaipataje hela yako na wakati kadi ime expire?

Sent from my cupboard using mug
 
Ukifanya manunuzi mtandaoni na muuzaji akanya refund hiyokadi itapokea hela bila shida.Ila unatakiwa usitengeneze kadi nyingine kabla ya kukamilisha miamala yako inayoendelea.Nilishawahi kupokea refund kwa kadi iliyoexpire ila sikutengeneza nyingine mpaka baada ya kupata refund.
 
Asante kwa ushauri, ila kuhusu kutotengeneza kadi nyingine itakuwa ngumu maana buyer protection waliweka siku tisini ambapo zilizobaki ni kama miezi miwili na kitu, hivyo naweza lala njaa mkuu. Ni afadhali nitengeneze nyingine ili niendelee kuitumia wakati huo kabla Covid-20 haijaingia.

Sent from my cupboard using mug
 
Ila mkuu si unajaza Expire date ya Card? Na ukitengeneza Card unapewa expire date. Ni jukumu la website unayonunua kujua Card yako ina expire lini ili malipo yawe refunded kwenye njia nyengine ya Kulipia.
Niliwahi kufuatilia hiyo kitu kwa upande wa AliExpress tu, na kwa maelezo yao walisema card iliyotumika kufanya manunuzi ndiyo tu itakayopokea refund na wala si vyinginevyo.
Sasa sijui kwa makampuni mengine wao wana msimamo upi.

Sent from my cupboard using mug
 
Inasemekana kwamba kwa sasa M-Pesa MasterCard inapoExpire hakuna tena kuiendeleza kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, na hii ni baada ya kujaribu kuiendeleza Card yangu iliyoExpire baada ya mwezi wa tisa kuisha, na majibu yalikuwa hivi, "your card has been un-suspended successfully" lakini nilipojaribu kuweka hela majibu yaliyokuja ni kwamba "Your Card is expired"

Nikachukua hatua ya kuwasiliana na huduma kwa wateja nikaambiwa hivi,

"Pole sana kwa hilo. Tunapenda kukufahamisha kwamba kadi ikiisha muda wake hauwezi kuiendeleza bali unatakiwa ufungue kadi mpya na kama kadi ya zamani ilikua ina hela unatakiwa kuzihamisha zote. ^OM"

Kuna swali niliuliza lakini mtoa huduma bado hajasoma meseji.

Sasa naomba kuuliza;

Kama mtu alifanya manunuzi mtandaoni lakini mzigo haukufika na muuzaji akataka kumrudishia hela itakuwaje? Je utaipataje hela yako na wakati kadi ime expire?

Sent from my cupboard using mug
Ikitokea kadi ime expire na una refund unawajulisha voda kadi yako ya zamani pesa ikirudishwa wanakuwekea kwenye account mpya. Pia wamefanya kadi iki expire hakuna ku renew kwa sababu za kiusalama kwani kusimamia kadi moja kwa moja ni gharama kubwa ndio maana wanakushauri usiweke pesa kama hufanyi manunuzi. Maana yake wanachozingatia ni usalama wa pesa yako wakati wa muamala na sio vinginevyo.
 
Unapofanya malipo kupitia kadi yako na ikatokea kuhitaji kurudishiwa hela lakini kadi ime expire, hakuna kampuni ambayo itarudisha hela yako kwenye kadi mpya, itarudisha hela yako kwenye kadi ya zamani. Wewe unatakiwa uwataarifu walio ishu hio kadi kuhusu hio refund, wao ndio watakaoihamisha kwenda kwenye kadi mpya.
 
Hayo ndiyo maneno nilikuwa nataka sasa. Tayari nishatengeneza kadi mpya na kuifanyia manunuzi.
IMG_20201002_200144.jpg

Sent from my cupboard using mug
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom