Hakuna kitu kizuri duniani kama kusikia ushauri kutoka hata kwa wale ambao unawadharau

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,873
Israeli siku zote habipiwi na ukimbipu tu anapiga hapo hapo.

Nasisitiza tena kwamba " hakuna kitu kizuri duniani kama kusikia ushauri kutoka hata kwa wale ambao unawadharau ".

Maisha ni 50 / 50 ila kikubwa ni kusali sana na kufanya toba mno ili hata Israeli akikupigia huna cha kulaumu ukifika Mbinguni Kuume kwa Baba Mungu.

Tuwe na Kiasi na umakini mno hasa tunapokuwa hapa duniani na Wanadamu tujenge tabia ya kuwatembelea sana Wagonjwa huko Mahospitalini ili na Wao waweze kufarijika na kuona tupo nao katika shida na raha.

Masikitiko yetu / Furaha zetu hapa duniani ziwe ni darasa tosha kutufanya tuwe na Hekima na Busara kuliko kutufanya tuwe Jeuri na Wakaidi halafu mwishoni tukaja kujuta.

Haya yote nimeyaota muda huu huu tu wa mchana ambapo nililala kidogo kwa Saa 1 na nusu nikasema si vibaya nikishea nanyi nilichokiota kwani nahisi kitatufaa wengi wetu.

Akhsanteni.
 
Ahsante kwa maneno haya mkuu

Akhsante sana Mkuu kwani sijawahi kuota hivi na mpaka nikaogopa na kuona si kitu cha kawaida hivyo siyo vibaya pia nikishea nanyi kwani yawezekana hii ndoto ikawa ni msaada kwa wengi hasa hasa wale wenzetu ambao hupenda Kuwadharau Watu wanaowashauri mambo mema na hata yenye msaada mkubwa wa Kiuhai / Kimaisha Kwao.
 
Back
Top Bottom