Chivundu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2012
- 7,176
- 5,285
Wanabodi,
Kwanza hakuna kitu kinatokea kwenye siasa kwa bahati mbaya. Kila kitu hupanga na wenye akili "Elites" ambao wengi wao hawapo kabisa kwenye siasa ila ndio wanaamua siasa.
Ukiona siasa ya Mkapa,Kikwete na leo JPM ujue wao wenye siasa yao wameamua kuifinyanga iwe hivyo unavyoiona leo.
Siasa ya ni kama mchezo wa kuigiza "Tamthilia" inayoigizwa jukwaani. Kuna wanaoangalia na kuisgabikia tamthilia ambao ndio sisi wananchi tunaokaa mbele ya jukwaa na mchezo unatuhusu sisi,na waigizaji "stunts" ambao ndio wanasiasa wenyewe wanaoigiza na nyuma ya jukwaa kuna pazia ambako huko ndiko mambo na mipango yote ya tamthilia inakopangwa. Huko nyuma ya pazia ndiko wanapambwa na kufanya mazoezi ya kuigiza na huko ndiko hao "Elites" wapo na ndio wanaamua mchezo uweje huku kila Muigizaji akipewa kipande aigize vipi na kwa namna gani na ili iweje,huku lengo kuu ni kuendelea kubaki milele katika dora huku waigizaji lengo lao ni kuishi kupitia mchezo huo unaolipa vizuri sana.
Na huko nyuma ya pazia ndio wapo "craftsmen" ambao ndio waandishi na waongozaji "masterminds" wa mpango mzima wa igizo.
Tuangazie ishu moja tuu ya vyama vingi msingi wake ambao mpaka leo tunateseka nao sababu bado "Elites" wameushikilia mpango wao huku "stunts" wengi wamezeeka japo wanaendelea kucheza tamthilia huku kazi kubwa ikiwa ni kuwaandaa wachezaji wengine wachanga.
Ndio maana leo utaona mtu kama Cheyo anaomba apewe viti vya ubunge free na ukimuona unaona wazi amechoka kimwili na fikra ila ni mchezaji wa siku nyingi sana na ana ukwasi anajiita "bwana mapesa".
Bosi wa TLP ambaye amewahi kuwa "Naibu Waziri Mkuu". Jamaa ambaye enzi hizo mimi napata akili aliwahi hamasisha tuandamane na mwishoni tukapigwa sisi na kwa macho yangu nikamuona anapanda gari ya RPC kwa kupigiwa saluti. Huyu jamaa yupo kwenye "payroll" nyingi za nchi hii na ni tajiri sema afya tuu mzee wetu huyu.
Vijana wengi "smart" wa walitolewa katika nafasi zao nyeti na kupewa mpunga na kuanzishwa vyama vyao huku wakipewa ruzuku na hao hao wanaowapinga. Yaani unampinga na kumtukana mtu,huyo huyo mtu ndiye anasaini malipo yenu kulipa chama chenu ruzuku kupitia msajiri wa hazina. Huku ujira wa hao "stunts" ukiwa ni ruzuku. Hawa hawana nia ya kushika dora,wao wananufaika na ruzuku na tips za hapa na pale kutoka kwa wale wanaowapinga.
Kwanza ieleweke mchakato wa vyama vingi haukuwa msukumo wetu wa ndani, ulikuwa ni msukumo wa nje maana sisi tuliukataa. Ila wakati huo ili kuendana na masharti ya mabeberu kutoka Bretton Woods ikiwemo WB na IMF chini ya mfumo wa SAP's "Elites" au "think tankers" walifikiri na kuja na mkakati wa siku nyingi wa kuleta vyama na namna ya kuvidhibiti.
Waliandaliwa watu "smart" kutoka vitengo wakapewa "mchanga" kwa lengo la kuanzisha vyama hiyo 1992.
Mtei na Makani ni miongoni mwa watu hao. Mbowe amechukua chama hicho 2000 hakuwahi jua waanzishaji wa chama hicho wana ajenda zao na wana mkono mrefu. Yeye akaja serious akakikuza chama hicho,"Elites" wakaona kijana anavuka grafu wakamchezea shere,wakawavuta vijana wake aliowapika akiwemo Boss wa ACT,alipolambishwa chambi ishu ya Buzwagi akawa hana namna akawa mtumwa wa "Elites". Elites wakawa wakaanza mtumia na wakampa mpunga aanzishe chama chama ndani ya chama. Huyo bosi ACT ana ukwasi wa kuweza kuendesha chama kichanga kusimamamisha mgombea uraisi na kumzungusha nchi kubwa kila kijiji. Hela hiyo aliotoa wapi?.
Mwaka 2015 "Elites" wakapika mpango washindane wao kwa wao. Wakafanikiwa kuwaingiza kingi CDM wakamletea EL. 2015 hapakuwa na upinzani,Chama dora kilikuwa peke yake,walishindana wale wale. 2015 mchawi "CDM" alipewa mwana amlee na akakubali. Mtoto kakua kanyea kambi na karudi kwa baba yake.
EL alikuwa na malengo mawili kwanza ajisafishe na pili alitimiza lengo la chama dora kushindana wenyewe. EL kwa sasa ni "msafi" na hafuatwi na nzi tena na unaishi "uzee mwema".
Tragedy of miscalculation inabaki kuitafuna CDM. Wakati kamati kuu inampitisha EL kuwa mgombea wao "mzee ruksa" alisema "wamekwisha" lakini sikio la kufa wakakomaa kumpiga jiki EL huku wakifurahia bilioni tisa alizokuja nazo wakijua ni zake,kumbe mwenzao alipewa huo "mpunga" na "Elites" na yeye hakuweka hata mia mbovu ya kwake.
2020 kuendelea...
Huyo dogo wa visiwani alianza kuandaliwa muda ni mpango wa muda mrefu toka enzi za Ben.
Ishu ya BM kufukuzwa na yenyewe ni trap ni mpango kama ulivyokuwa wa EL mwaka 2015.
Mtoto wa kigoma Mwandiga na yeye anadeni lile lile la kuwamaliza hawa CDM huku yeye akiwa hana mpango wa kushika dora ila kupiga ruzuku. Kazi hiyo bado hajatimiza na ndio maana Maalim amenyakwa visiwani na huku anampanga BM agombee bara.
Lengo lao ni kuwapoka CDM na CUF kitumbua "ruzuku" na kuimaliza CDM.
NATABIRI HAYA BAADA YA OKTOBA
BM ataenda ACT atapunguza kura za CDM. ACT watapewa majimbo na watapata asilimia nyingi za kura kupata ruzuku kutoka visiwani.
BM akimaliza uchaguzi chama chake watamsamehe na watamrudushia uanachama.
ZZK hatagombea uraisi mwaka huu,mpango wake ni 2025 ambapo atakuwa ametimiza lengo la kuiondoa CDM katika "key opposition" ya nchi.
Maalim mwaka huu atapata kura kiduchu sana maana CUF nao wataweka mtu kugawana kura na Huseni atapeta.
Bado tunasafari ndefu sana ya "upinzani" bongo. Aliyebuni mpango wa mwaka 1992 wa namna ya kuendesha siasa ya vyama vingi akili yake itaishi kwa siku nyingi na kwa vizazi vingi. Mpaka pale ambapo tutakuja kufahamu tunataka nini na tukafanya kazi kubwa ya kupata tunachokitaka ndipo tutapata jibu.
Wasaalam.
"Upepo ukipuliza sana uchi wa kuku huonekana"
"Ukiwa na subra utaona mwisho wa kila kitu"