Hakuna kitu kinatokea kwa bahati mbaya katika siasa ya Bongo

Umemjua Maalim lini?
Maalim sasa yupo kwenye 70's wewe umeanza mjua enzi zipi?
Tukianza leo kuandika kitabu cha Maalim tukianzia alipikuwa Mwanafunzi wa PSPA UDSM tutajaza page nyingi sana za kitabu.
Huwezi Muelezea Maalim kwa aya mbili tatu. Maalim ni mkakati na ni historia.
Wasalaam
Ninachokwambia ni hiki, Maalimu anatibiwa na SMZ sababu ni stahiki yake na ndio maana hata kipindi kile Maalim amegoma kumpa mkono Shein Huku bara Magu akaja akasema mimi mtu hawezi kuninyima mkono halafu nije nimsainie malipo yake ya kwenda kutibiwa.

Kwa hio wewe kusema Maalim anatibiwa na SMZ wala hio sio habari mpya/iliyokua imefichwa,hio inajulikana hadharani miaka yote.
 
Maalimu kua kitengo hilo sijui lkn akiumwa ni lazima agharamiwe na SMZ sababu yeye alikua ni makamu wa raisi huko Zenji(kipindi cha Shein) na matibabu ni sehemu ya stahiki yake kama makamu wa rais mstaafu.

Kumbe umemjua Maalim juzi hapa kwenye mseto pole sana.
 
Ninachokwambia ni hiki, Maalimu anatibiwa na SMZ sababu ni stahiki yake na ndio maana hata kipindi kile Maalim amegoma kumpa mkono Shein Huku bara Magu akaja akasema mimi mtu hawezi kuninyima mkono halafu nije nimsainie malipo yake ya kwenda kutibiwa.

Kwa hio wewe kusema Maalim anatibiwa na SMZ wala hio sio habari mpya/iliyokua imefichwa,hio inajulikana hadharani miaka yote.

Haya sawa nimekubali maelezo yako.
 
Wanabodi,

Kwanza hakuna kitu kinatokea kwenye siasa kwa bahati mbaya. Kila kitu hupanga na wenye akili "Elites" ambao wengi wao hawapo kabisa kwenye siasa ila ndio wanaamua siasa.

Ukiona siasa ya Mkapa,Kikwete na leo JPM ujue wao wenye siasa yao wameamua kuifinyanga iwe hivyo unavyoiona leo.
Siasa ya ni kama mchezo wa kuigiza "Tamthilia" inayoigizwa jukwaani. Kuna wanaoangalia na kuisgabikia tamthilia ambao ndio sisi wananchi tunaokaa mbele ya jukwaa na mchezo unatuhusu sisi,na waigizaji "stunts" ambao ndio wanasiasa wenyewe wanaoigiza na nyuma ya jukwaa kuna pazia ambako huko ndiko mambo na mipango yote ya tamthilia inakopangwa. Huko nyuma ya pazia ndiko wanapambwa na kufanya mazoezi ya kuigiza na huko ndiko hao "Elites" wapo na ndio wanaamua mchezo uweje huku kila Muigizaji akipewa kipande aigize vipi na kwa namna gani na ili iweje,huku lengo kuu ni kuendelea kubaki milele katika dora huku waigizaji lengo lao ni kuishi kupitia mchezo huo unaolipa vizuri sana.

Na huko nyuma ya pazia ndio wapo "craftsmen" ambao ndio waandishi na waongozaji "masterminds" wa mpango mzima wa igizo.

Tuangazie ishu moja tuu ya vyama vingi msingi wake ambao mpaka leo tunateseka nao sababu bado "Elites" wameushikilia mpango wao huku "stunts" wengi wamezeeka japo wanaendelea kucheza tamthilia huku kazi kubwa ikiwa ni kuwaandaa wachezaji wengine wachanga.

Ndio maana leo utaona mtu kama Cheyo anaomba apewe viti vya ubunge free na ukimuona unaona wazi amechoka kimwili na fikra ila ni mchezaji wa siku nyingi sana na ana ukwasi anajiita "bwana mapesa".

Bosi wa TLP ambaye amewahi kuwa "Naibu Waziri Mkuu". Jamaa ambaye enzi hizo mimi napata akili aliwahi hamasisha tuandamane na mwishoni tukapigwa sisi na kwa macho yangu nikamuona anapanda gari ya RPC kwa kupigiwa saluti. Huyu jamaa yupo kwenye "payroll" nyingi za nchi hii na ni tajiri sema afya tuu mzee wetu huyu.

Vijana wengi "smart" wa walitolewa katika nafasi zao nyeti na kupewa mpunga na kuanzishwa vyama vyao huku wakipewa ruzuku na hao hao wanaowapinga. Yaani unampinga na kumtukana mtu,huyo huyo mtu ndiye anasaini malipo yenu kulipa chama chenu ruzuku kupitia msajiri wa hazina. Huku ujira wa hao "stunts" ukiwa ni ruzuku. Hawa hawana nia ya kushika dora,wao wananufaika na ruzuku na tips za hapa na pale kutoka kwa wale wanaowapinga.

Kwanza ieleweke mchakato wa vyama vingi haukuwa msukumo wetu wa ndani, ulikuwa ni msukumo wa nje maana sisi tuliukataa. Ila wakati huo ili kuendana na masharti ya mabeberu kutoka Bretton Woods ikiwemo WB na IMF chini ya mfumo wa SAP's "Elites" au "think tankers" walifikiri na kuja na mkakati wa siku nyingi wa kuleta vyama na namna ya kuvidhibiti.

Waliandaliwa watu "smart" kutoka vitengo wakapewa "mchanga" kwa lengo la kuanzisha vyama hiyo 1992.

Mtei na Makani ni miongoni mwa watu hao. Mbowe amechukua chama hicho 2000 hakuwahi jua waanzishaji wa chama hicho wana ajenda zao na wana mkono mrefu. Yeye akaja serious akakikuza chama hicho,"Elites" wakaona kijana anavuka grafu wakamchezea shere,wakawavuta vijana wake aliowapika akiwemo Boss wa ACT,alipolambishwa chambi ishu ya Buzwagi akawa hana namna akawa mtumwa wa "Elites". Elites wakawa wakaanza mtumia na wakampa mpunga aanzishe chama chama ndani ya chama. Huyo bosi ACT ana ukwasi wa kuweza kuendesha chama kichanga kusimamamisha mgombea uraisi na kumzungusha nchi kubwa kila kijiji. Hela hiyo aliotoa wapi?.

Mwaka 2015 "Elites" wakapika mpango washindane wao kwa wao. Wakafanikiwa kuwaingiza kingi CDM wakamletea EL. 2015 hapakuwa na upinzani,Chama dora kilikuwa peke yake,walishindana wale wale. 2015 mchawi "CDM" alipewa mwana amlee na akakubali. Mtoto kakua kanyea kambi na karudi kwa baba yake.

EL alikuw na malengo mawili kwanza ajisafishe na pili alitimiza lengo la chama dora kushindana wenyewe.

2020 kuendelea...
Huyo dogo wa visiwani alianza kuandaliwa muda ni mpango wa muda mrefu.
Ishu ya BM kufukuzwa na yenyewe ni trap ni mpango kama ulivyokuwa wa EL mwaka 2015.
Mtoto wa kigoma Mwandiga na yeye anadeni lile lile la kuwamaliza hawa CDM huku yeye akiwa hana mpango wa kushika dora ila kupiga ruzuku. Kazi hiyo bado hajatimiza na ndio maana Maalim amenyakwa visiwani na huku anampanga BM agombee bara.
Lengo lao ni kuwapoka CDM na CUF kitumbua "ruzuku" na kuimaliza CDM.

NATABIRI HAYA BAADA YA OKTOBA
BM ataenda ACT atapunguza kura za CDM. ACT watapewa majimbo na watapata asilimia nyingi za kura kupata ruzuku kutoka visiwani.
BM akimaliza uchaguzi chama chake watamsamehe na watamrudushia uanachama.

ZZK hatagombea uraisi mwaka huu,mpango wake ni 2025 ambapo atakuwa ametimiza lengo la kuiondoa CDM katika "key opposition" ya nchi.

Maalim mwaka huu atapata kura kiduchu sana maana CUF nao wataweka mtu kugawana kura na Huseni atapeta.

Bado tunasafari ndefu sana ya "upinzani" bongo. Aliyebuni mpango wa mwaka 1992 wa namna ya kuendesha siasa ya vyama vingi akili yake itaishi kwa siku nyingi na kwa vizazi vingi. Mpaka pale ambapo tutakuja kufahamu tunataka nini na tukafanya kazi kubwa ya kupata tunachokitaka ndipo tutapata jibu.

Wasaalam.
"Upepo ukipuliza sana uchi wa kuku huonekana"
"Ukiwa na subra utaona mwisho wa kila kitu"

Yule mbobezi nakubaliana nawe kabisa ni sarakasi za lumumba,atarudi kuunga juhudi Kama wenzake.
 
Tatizo wewe unaleta habari then unalazimisha ku-dominate mada kitu ambacho hakina maana.

Umeongelea ACT-Wazalendo nikakuuliza Jack Zoka yuko wapi siku hizi?

Na sio wajibu wangu kujua fulani yupo wapi sio lengo la mjadala.
Pia sijalazimisha mtu akubaliane na mimi,mimi nimeandika mawazo yangu na wewe unaweza andika yako ndio mjadala.
 
Drifter,
Mbowe alikuwa na ajenda seriously lakini alikosa umakini. "Elites outsmarted the guy back in 2015" na hiyi ndio sifa kubwa ya "Elites". Wama "ku-outsmart".
ZZK alipoingia kingi ya kuwa family friend wa JK kupitia mama yake Shida Salum (R.I.P) ndipo "spy chief" wa enzi hizo alipoanza mtumia na ndipo ACT wazalendo ilianza kupikwa.
Mbowe alinusa hii kitu na mkakati ulikuwa mkubwa sana wa kukimaliza CDM.
Pia Mbowe na ile ya "kutokuwa na njaa tumboni" ili msaidia sana.
Njaa ikihamia tumboni nao ni mtego.
Wasalaam
J.Zoka yuko wapi siku hizi?
[/QUOTE]
True angekuwa na njaa angeshamalizwa.
Huwezi ukawa masikini then ukawa mwanasiasa bora ni lzm utauza utu wako kwa vipande.Thus wenzetu leseni za udereva upewa tajiri mtu aliyeshiba
 
Yule ni kama kawa ni agent,tatizo atakalolipata sasa hivi ni kwamba huku mtaani wajuba wote wamemshtukia kwamba yeye ni pandikizi tu.
Waling'atwa na nyoka awarudii kosa,naona mazungumzo yake na CDM yaligonga mwamba anajaribu ACT.Ila ACT wakirudia kosa la cdm 2015 kuyapa mapandikizi leseni za udereva watavunja mioyo ya wanachama wao.
 
Na sio wajibu wangu kujua fulani yupo wapi sio lengo la mjadala.
Pia sijalazimisha mtu akubaliane na mimi,mimi nimeandika mawazo yangu na wewe unaweza andika yako ndio mjadala.
Daah kama humjui huyo mtu then hata kujua ACT ilianzishwa kwa mkono wa kina nani huwezi kuelewa vzr.

Hapo kwny ACT ilianzishwa sijui kwa Zitto kuunganishwa na ndg wa JK walioko huko kitengo toa hio sentensi then weka ACT ilianzishwa na Zitto kwa msaada wa kina Zoka.
 
Kuna msemo ulivuma sana mwaka 2015 kwamba "CCM ina kitabu kikubwa cha MBINU ZA KUSHINDA UCHAGUZI na mpaka mwaka 2015 walikua ndo kwanza wako kurasa ya 3" kwahiyo bado kurasa kibao yaan Wapinzani wa nchi hii wajipange😢😢
Hakuna cha kitabu wala nini. Waweke tume huru na kubadili katiba ndiyo utaijua hiyo nguvu ya hicho kijitabu.
 
Waling'atwa na nyoka awarudii kosa,naona mazungumzo yake na CDM yaligonga mwamba anajaribu ACT.Ila ACT wakirudia kosa la cdm 2015 kuyapa mapandikizi leseni za udereva watavunja mioyo ya wanachama wao.
ACT kule atapata nafasi ya kugombea,nimeona jana Membe kapiga picha na wakina Kabwe na Maalimu,na nikaona Zitto anasema ni lazima Upinzani usimamishe mgombea mmoja kwny urais na majimbo waachiane.

Nikasema Naona maagizo kutoka kwa Agent wanaanza kuyawasilisha mdogo mdogo.

Upumbavu huo uishie huko huko ACT wasiulete Chadema kabisa.
 
mwayena.
Kumwamini mtu hutegemea namna unavyotazama mambo na uelewa.
Siasa ina mengi kuielewa inahitaji usiwe kuku uwe tai.
Hapo Kenya Raisi ajaye 2022 ni Gideon Moi. Usishangae Ridhiwani Kikwete akapata wizara 2020 na akawa bosi wetu 2025.
Comment reserved for future use.
 
Daah kama humjui huyo mtu then hata kujua ACT ilianzishwa kwa mkono wa kina nani huwezi kuelewa vzr.

Hapo kwny ACT ilianzishwa sijui kwa Zitto kuunganishwa na ndg wa JK walioko huko kitengo toa hio sentensi then weka ACT ilianzishwa na Zitto kwa msaada wa kina Zoka.

Ni kweli simjui huyo mtu,ndio namsikia leo kutoka kwako. Hongera kwa kumjua.
 
Umemjua Maalim lini?
Maalim sasa yupo kwenye 70's wewe umeanza mjua enzi zipi?
Tukianza leo kuandika kitabu cha Maalim tukianzia alipikuwa Mwanafunzi wa PSPA UDSM tutajaza page nyingi sana za kitabu.
Huwezi Muelezea Maalim kwa aya mbili tatu. Maalim ni mkakati na ni historia.
Wasalaam
hahah nimefurahi kuona kuna watu wanamjua vizuri maalim ni nani nchi hii.Maalim ni nyoka mmoja hatari sana na ni player muhimu katika siasa za nchi hii
 
Naunga mkono hoja. Ukifikiri kwa undani kikao cha Maalim Seif na Magufuli ikulu Dar es Salaam na haya yanayotokea kwa Membe kujiunga Act utagundua kuwa ACT ni mpango maalum wa kuua nguvu ya CHADEMA.

CHADEMA kuweni makini sana Mie Nina uhakika mkimsimamisha LISSU na mkienda na agenda ya nguvu ya umma mwaka huu huu ushenzi wote uliosukwa na CCM toka miaka ya nyuma unaenda kufa na kuisha rasmi
Lissu atawekewa pingamizi na CCM,Muandae Lissu by 2025.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom