Hakuna kitu kinakera kama kufanya kazi na mpenda sifa

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,120
Habari!

Je,umewahi kufanya kazi na mtu mpenda sifa? Hawa maofisini tunawaita kazi kunoga, jeshini tunawaita majeshi kumbwitu, au majeshi K.

Hawa watu huwa ni wapenda sifa, usiombe wawe juu yako halafu amekuja boss wa juu kuwatembelea.

Hawa watu wako tayari wakuroge ili wao ndio wawe na kauli, hii hutokea wanapoona umekuwa na cheo kikubwa zaidi yao mko katika kazi moja.

Hawa watu sifa wanazipenda kuliko hata Pesa. Wako tayari kufanya kazi yoyote ilimradi tu itawapa sifa hata kama haiwahusu au haina malipo.

Hapa kazini tunaye mmoja, anaboa sana.
 
Wapo wadada watatu hapa kwangu,yani bosi akizungumza kitu hata hakichekeshi wanacheeka ili mradi aone wana muunga mkono,yani kujichekesha vitu hata havichekeshi wakimuona bosi, mara utasikia tukuchemshie chai, mara utasikia kuna vitafunio tukuchukulie bosi, dah kwakweli wanayaweza.
 
Alikuwepo mmoja hapa ofisini, akajifanya anajua saaana sheria za kupiga mstari daftari la mahudhurio (Kabla ya haka kaking'amuzi)

Tulikuwa kila mwezi tunaiba daftari :D :D :D
Umenikumbusha bwana mdogo m'moja. Hawa watoto wa miaka ya 1997 wanatakiwa watafutiwe maeneo ya kazi ambapo watakuwa na rika zao na si kuwekwa kitengo na waliowazidi umri au kupewa cheo kuwazidi.

Kimsingi, hawa madogo wanapenda sana kuonekana wanajua na hawanaga adabu. Wanaona vyeo na sifa zao ndio muhimu kuliko adabu na umri.

Kuna dogo tulikuwa nae kampuni moja hapa mjini Dar. Dogo tulikuwa nae kitengo cha Marketing and sales. Dogo ameingia kazini hata miezi sita hana ameshaanza kutupanda vichwani.

Mara aje aanzishe mijadala kuhusu kuchelewa kwamba kwann watu wanachelewa, mara oooh yaani mimi nikipewa cheo cha kuwasimamia hapa ndani sijui kama kuna mtu atabakia.....nitawanyoosha.

Me siku moja nikamtolea uvivu. Nikamwambia kwanza wewe ni mtoto mdogo sana kutufokea au kutupangia sisi tukiokuzidi kiumri na pia hata experience ya kazi na maisha.

Halafu pili nikamkumbusha dogo kuwa maisha hayaendi hivyo, hutakiwi kujiona wewe ndie mjuaji na mwerevu kushinda kila mtu yoyote mahala ulipo, kuna kesho na keshokutwa. Hizi kampuni tunaajiriwa na kuacha kazi, hazina guarantee yakuwapo milele. Dogo akawa analeta dharau na kuziba masikio kila tunapomuweka sawa.

Fitina nyingi sana alikuwa anafanya ikiwemo kuwageuka wenzake anapokwenda kwa wateja au kuzungumza na menejiment. Alisababisha supervisor kusimamishwa kazi baada ya kutoa siri kuwa jamaa kuna hela ya mteja kapiga. Na pia aliharibu kwa kushinikiza uongozi watuwekee ile finger check in sensor ya kuconfirm ujio wa kazini.

Haya yote na mengineyo yakapelekea watu baadhi kusimamishwa kazi na wengine kuondoka wenyewe. Dogo akavimba sana kichwa kama makonda, kwa kuongea kauli za kipuuzi na tambo za kijinga mbele za watu. Nikasema haina shida muda ndio mwalimu mzuri.

Basi nakumbuka wazee kunasiku tukalimwa barua kwa sababu ambazo kimsingi ni geresha ila lengo ni kupunguza watu maaan tulivyomaliza mkataba tu huku nyuma wakaja madogo wapya kibao.

Basi wazee wa jiji tukatafuta green pasture somewhere else, maisha yakaendelea MUNGU akabarikia tukarudi kuwa vema.

Sasa hapo juzi kati baada ya hii shuruba ya corona, kuna bi dada tulikuwa nae ofisini akanicall tukaongea kwa kirefu sana akinipa picha ya matukio baada ya mimi na wenzangu kadhaa kusepa.

Kampuni ilisitisha mkataba na kampuni kubwa na hatimae ikasitisha mikataba na kila mtu na raia wakarejea uraiani. Bwana mdogo anahaha. Nilimkuta duka la nguo ana hang na viduku wenzake, ameniona ananiletea salamu za kinafiki nikamjibu kama simjui nikaachana nae takataka kabisa.

Dogo yupo benchi sasa hivi hata utokee mchongo hapa nilipo naanzaje mwita au kumfanyia mpango maana najua ni mtaka sifa. Kuna watu wanajizibia baraka kwa matabia yao wanayotoka nayo kwao badala ya kujiheshimu wanajikuta wao ni wajuaji.
 
Kama unachapa kazi no sawa chapa kazi kwa habari zako. Sio uchapakazi wako unaanza sasa kuingilia na mambo ya watu wengine....
Kama internal system and control ya organisation ipo vizuri haiwezekani kuchapa kazi bila kuingiliana. Cashier hawezi bila accountant, accountant hawezi bila manager, manager hawezi bila afisa masoko n.k yaani mtakerana tu. Inatakiwa kama ni kazi wote mpige, kama ni wavivu wote muwe wavivu ndo mambo yataenda. kinyume na hapo yule aliye na tabia tofauti ataonekana anaingilia yasiyomuhusu.
 
Umenikumbusha bwana mdogo m'moja. Hawa watoto wa miaka ya 1997 wanatakiwa watafutiwe maeneo ya kazi ambapo watakuwa na rika zao na si kuwekwa kitengo na waliowazidi umri au kupewa cheo kuwazidi.

Kimsingi, hawa madogo wanapenda sana kuonekana wanajua na hawanaga adabu. Wanaona vyeo na sifa zao ndio muhimu kuliko adabu na umri.

Kuna dogo tulikuwa nae kampuni moja hapa mjini Dar. Dogo tulikuwa nae kitengo cha Marketing and sales. Dogo ameingia kazini hata miezi sita hana ameshaanza kutupanda vichwani.

Mara aje aanzishe mijadala kuhusu kuchelewa kwamba kwann watu wanachelewa, mara oooh yaani mimi nikipewa cheo cha kuwasimamia hapa ndani sijui kama kuna mtu atabakia.....nitawanyoosha.

Me siku moja nikamtolea uvivu. Nikamwambia kwanza wewe ni mtoto mdogo sana kutufokea au kutupangia sisi tukiokuzidi kiumri na pia hata experience ya kazi na maisha.

Halafu pili nikamkumbusha dogo kuwa maisha hayaendi hivyo, hutakiwi kujiona wewe ndie mjuaji na mwerevu kushinda kila mtu yoyote mahala ulipo, kuna kesho na keshokutwa. Hizi kampuni tunaajiriwa na kuacha kazi, hazina guarantee yakuwapo milele. Dogo akawa analeta dharau na kuziba masikio kila tunapomuweka sawa.

Fitina nyingi sana alikuwa anafanya ikiwemo kuwageuka wenzake anapokwenda kwa wateja au kuzungumza na menejiment. Alisababisha supervisor kusimamishwa kazi baada ya kutoa siri kuwa jamaa kuna hela ya mteja kapiga. Na pia aliharibu kwa kushinikiza uongozi watuwekee ile finger check in sensor ya kuconfirm ujio wa kazini.

Haya yote na mengineyo yakapelekea watu baadhi kusimamishwa kazi na wengine kuondoka wenyewe. Dogo akavimba sana kichwa kama makonda, kwa kuongea kauli za kipuuzi na tambo za kijinga mbele za watu. Nikasema haina shida muda ndio mwalimu mzuri.

Basi nakumbuka wazee kunasiku tukalimwa barua kwa sababu ambazo kimsingi ni geresha ila lengo ni kupunguza watu maaan tulivyomaliza mkataba tu huku nyuma wakaja madogo wapya kibao......

Basi wazee wa jiji tukatafuta green pasture somewhere else, maisha yakaendelea MUNGU akabarikia tukarudi kuwa vema.

Sasa hapo juzi kati baada ya hii shuruba ya corona, kuna bi dada tulikuwa nae ofisini akanicall tukaongea kwa kirefu sana akinipa picha ya matukio baada ya mimi na wenzangu kadhaa kusepa.

Kampuni ilisitisha mkataba na kampuni kubwa na hatimae ikasitisha mikataba na kila mtu na raia wakarejea uraiani. Bwana mdogo anahaha..... Nilimkuta duka la nguo ana hang na viduku wenzake, ameniona ananiletea salamu za kinafiki nikamjibu kama simjui nikaachana nae takataka kabisa.

Dogo yupo benchi sasa hivi hata utokee mchongo hapa nilipo naanzaje mwita au kumfanyia mpango maana najua ni mtaka sifa. Kuna watu wanajizibia baraka kwa matabia yao wanayotoka nayo kwao badala ya kujiheshimu wanajikuta wao ni wajuaji.....
Hakuwa na busara. Hilo ndo kosa lake.
 
Back
Top Bottom