Hakuna kitu kibaya duniani kama umasikini!

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,155
11,461
Rejea kichwa cha habari kinajitosheleza.

Kwanza umasikini ukiisha kukudaka, pamoja na kwamba unakutesa kwa kukunyima mahitaji yako yooote ya muhimu kama kukosa mahali bora pa kulala, kuangaika na njaa, kiu, mavazi, jua lako, mvua yako, vumbi lako, huna unachomiliki hata mwili sio mali yako wakati wowote unaweza kushambuliwa na kuharibiwa na vibaka, wezi, wabakaji, nk.

Nje ya hapo, huthaminiki katika jamii na matokeo yake unakuwa shamba la kupandikiza tabia zote mbaya kama uongo, usengenyaji, wizi, umalaya, fitina, uchawi, udokozi, n.k. Unakuwa ndo chanzo cha kupata na kusambaza magonjwa, harufu mbaya, kutumiwa na makundi ya uhalifu wa madawa ya kulevya, kutumiwa kutetea kundi fulani la uhalifu kwa kupewa kipande cha mkate (hata bure kwa kulazimishwa), kudhurumiwa haki zako hata kama uliridhishwa mali au una madai fulani unadai hakuna wa kukusaidia na kupelekea kudhurumiwa.

Unakuwa ni nyumba ya kuingiwa na kila aina ya roho chafu (kwa mujibu wa imani). Mbaya zaidi umasikini ukikuingia na kuvuka mipaka unajikuta unaupenda na hutaki kuutoka hata kama mazingira yatatengenezwa kukutoa au kupewa msaada utakataa huo msaada au kuutumia vibaya au kupokonywa kwasababu hata akili na ufahamu huna!

Unaweza ukawa huna sifa zote nilizoziorodhesha hapo juu lakini ukiwa na mojawapo ni dalili tosha ya umasikini kuanza kukunyemelea. Hivi ndivyo wanavyokuona (matajiri) na wale waliobahatika kuukwepa au kuushinda umasikini katika jamii zetu tunazoishi. Pia hivyo ndivyo Wazungu wanavyotuona Waafrika.

Wakati ukijitambua una sifa za umasikini ukianza kupambana nao, pambana nao kimya kimya kwa maana yule unayetaka akusaidie kukutoa hana msaada wowote na anakuogopa na kukukimbia kiaina usije ukamuambukiza. Kwahiyo pambana na hali yako!

NILIKUWA SEHEMU NATAFAKARI BAADA YA KUSHIBA MIHOGO NA MAJI YA KUFUNGA YA KANDORO
 
bwana mdogo masikini ana jeuri sana afu huwa anaanza kuonyesha dalili pole pole

ukiwa darasani afu mpiga kelele, we ni masikini mtarajiwa.

nywele zikikuota bila mpangilio, we ni masikini mtarajiwa.

unalala saa 10 usiku kwa kukesha kuangalia movie afu unaamka saa 7 mchana kwa uchovu wa movie, we ni masikini mtarajiwa.

kila mwanamke/mme unataka kuwa naye, we ni masikini mtarajiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom