Hakuna Kilicho Wazi Bado; Mambo Mengi Hatujayajua Bado - Juu ya Yote Imani

Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
811
349
Ni kama kila kitu bado ni fumbo. Si mwanzo wala si hatima ya mtu, maisha ya mtu bado ni fumbo.

Kuna hatua muhimu za kujivunia katika kuelewa mwanzo na hatima ya mtu. Lakini, hatahivyo juhudi hizo mara zote zimekuja na kasoro nyingi katika kufumbua fumbo la maisha na ulimwengu.

Huwezi kusema maarifa hayo si muhimu. La hasha! Kwa yenyewe ni muhimu katika kuelewa na kufumbua mafumbo ya maisha.

Imani kwa upande mmoja na sayansi kwa upande mwingine, vyote bila kukinzana, vimetajirisha ufahamu wetu kujusu mafumbo ya maisha. Mathalani uhai ni nini. Kifo ni nini. Na uzima ni nini. Imani inatuwezesha kujua hayo na sayansi inatuthibitishia hayo.

Imani inaweza kutupatia majibu yote kuhusu mafumbo ya maisha. Kwa mfano, kwanini kuna magonjwa duniani; au tunatoka wapi tunakwenda wapi. Lakini swali ni Je! Hili linawezekanaje?

Ni muhimu kujifunza. Lakini imani inapita kujifunza; si kujifunza tu - ni nje ya kujifunza. Na hapa ndipo ilipo tofauti ya imani na sayansi.

Kwa hiyo, kama vitu vingi si wazi yaani hatujavijua maana yake si hivyo vitu bali imani. Hapa si kushindwa kwa sayansi kwa sababu sayansi haifanyi kazi kutoka kwa yenyewe isipokuwa kutoka kwa imani.

Hivi tulivyonavyo leo na vile vilivyopo, vyote ni imani. Uvumbuzi sio sayansi, ni imani. Na ugunduzi sio imani, ni sayansi. Lakini ugunduzi na sayansi, hivi viwili havitoki kwa sayansi ila imani.

Ninaweza kuilezea imani kama hali ya juu ya akili. Si dhana, au mawazo wala madhanio. Ni hakika ya mambo na uthabiti katika vitu; ni kipaji.

Habari za maisha ya mtu zimeelezwa kila karne lakini sio na kila mtu. Uvumbuzi umefanyika lakini sio na kila mtu. Uvumbuzi huo umeendelezwa lakini katika utaratibu maalumu.

Hatujui bado, kwa mfano nini hasa husababisha magonjwa ya moyo au mfumo wa fahamu kadiri ya sayansi lakini kadiri ya imani tunaweza kujua.

Kile tunachokijua kuhusu magonjwa kadiri ya sayansi ni asilimia 10 pekee. Huenda hili likakushangaza lakini si kwamba hilo sio muhimu; hakika ni muhimu.

Kwa sayansi, tunajua kuwa ubongo wetu ni asilimia 10 ya ufahamu wote. Pamaja na ukweli huo imethibitika kisayansi kuwa mtu hutumia asilimia 1 mpaka 3 ya ubongo wake wote alionao.

Kuna mambo mawili hapa kutoka kwenye maeleo hayo ya kisayansi. Kwanza ni kile tunachokijua (asilimia 1 hadi 3) ukilinganisha na uwezo wetu wote wa ufahamu (10%). Na pili ni uwezo wetu wa ufahamu tulionao ni 10% ukilinganisha na 90% ambazo hatuna.

Hii ina maanisha kwamba hata ule ufahamu wetu, asilimia 10 tuliopewa, bado hatujaufanyia kazi inavyotakiwa. Kwa nini? Hili ni swali muhimu la kujiuliza.

Lakini kuna jambo muhimu zaidi; nalo ni kuhusu asilimia 90 ambayo hatujapewa kukamilisha asilimia 100 ya ufahamu wote. Hii tunaipataje? Hapa ndipo mafumbo ya maisha yanajitokeza na ndipo hapa tunaona imani.

Maandiko matakatifu yanaeleza kwamba Mungu ndiye afanyae kila kitu. Ni kweli Mungu ndiye afanyae kila kitu. Lakini, hatahivyo kuna shida katika kufafanua Mungu. Labda, swali ni Je! Zipi ni sifa za Mungu? Swali hili linaweza kutusaidia kuelewa maandiko matakatifu yanaposema Mungu ndiye afanyae kila kitu, yana maana gani.

Ninaweza kusema kuwa hakuna mtu awezae kufanya chochote isipokuwa Mungu. Si maendeleo, si tenkolojia; si uvumbuzi, ni Mungu ndiye afanyae hayo yote.

Yote tunayoyajua na ambayo yamethibitika kweli kwetu karne na karne ni Mungu Mwenyewe ndiye amefanya hayo. Hao ambao, kutoka karne na karne tumewashuhudia kuwa sio watu wa kawaida, kwa namna walivyofundisha na kuvumbua, ni Mungu Mwenyewe.

Namna ambavyo Mungu amekuwa nasi kutoka vizazi na vizazi ndilo jambo lisilo wazi kwetu. Hii hatahivyo ni saula la imani. Wale ambao Mungu amewapatia kipaji hiki cha imani, wakaona ukweli huo, walio ndugu zao kwa sababu nyingi: kupenda dunia hawakuzingatia hayo. Hivyo tumepoteza imani na sasa mambo mengi hatuyajui bado.
 
Imani inawezaje kutupatia mafumbo yote ya maisha wakati imani iko based on betting?
 
Wanaojua hawataki wengine wajue shida hata wanaozijua siri wakija hamtawaelewa sababu wengi mmemezwa na mliyofunzwa na kukaririshwa tayari.dini za kigeni na usomi unaombatana na kiitwacho sayansi vimewatia upofu.wenye ujuzi wa kiasili na mawazo kuntu. Wameamua kujinyamazia maana wakitaka kutoa hizo siri. Mwawapoteza mapema. Langu ni hilo
 
Wanaojua hawataki wengine wajue shida hata wanaozijua siri wakija hamtawaelewa sababu wengi mmemezwa na mliyofunzwa na kukaririshwa tayari.dini za kigeni na usomi unaombatana na kiitwacho sayansi vimewatia upofu.wenye ujuzi wa kiasili na mawazo kuntu. Wameamua kujinyamazia maana wakitaka kutoa hizo siri. Mwawapoteza mapema. Langu ni hilo
Ngumu kumeza ngumu kutema..

Sent from my Pro_Max11 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom