Elections 2015 Hakuna kifungu cha sheria kinachomruhusu mpiga kura kukaa nje ya mita 200 toka kituoni akilinda kura

Ukawa wapuuzi kweli
Sasa unalinda kura ukiwa nje wakati kura zinahesabiwa ndani
Upuuzi mtupu
Na uharo
Huu

Kwan hamna mawakala?

".......mtu akikuambia upige kura na ulinde kura ..mwambie mzee njoo tulinde wrote..."
Kanali kinana

Mwambie Kinana tembo wetu jamani... Atuonee huruma bana
 
Kura lazma zilindwe otherwise bora kusiwe na uchaguzi. anaepinga kulinda kura huyo atakua kahamia Tz mwaka huu.
 
je, hivyo vituo havijazungukwa na nyumba au makazi ya watu?

kuzaliwa siku moja, kufa siku moja!

haki haiombwi, haki inatafutwa.
 
Nani kasema ukawa ndo wanaweza ibiwa kura tu? Hata ccm wanaweza ibiwa vilevile, ukawa ccm act wote tulinde kura zetu,
 
Wala hakuna sheria inayokataza , kifungu cha 104(1) cha sheria ya uchaguzi sura ya 343 kinasema : " mtu yeyote haruhusiwi kufanya mkutano siku ya uchaguzi au ndani ya majengo ambako upigaji kura unaendelea au sehemu yoyote ndani ya mita 200 ya jengo hilo akiwa amevaa au kuonyesha bango , picha au nembo kwa ajili ya kumpigia debe mgombea kwenye uchaguzi huo " mwisho wa kunukuu , wala haijakatazwa kulinda kura ukiwa nje ya eneo hilo .
 
MAZOEA YA KUWEPO UMBALI WA MITA 200 AU 300 KUTOKAKITUO CHA KUPIGIA KURA

Kumekuwepo na mazoea kwamba, baada ya kupiga kura wafuasiwa vyama hubakia na kukaa kwenye maeneo ya kupigia kuraumbali wa mita 100 au 200 au 300.Jambo hili ni kinyume na Sheria za Uchaguzi. Kwani, katikakifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343kinasema nanukuu

“Hakuna mtu atakayefanya Mkutano siku ya kupiga kura au;ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika uchaguziunaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita miambili yajingo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleoau nembo nyingine inayoonesha kuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”

Mwisho wa kunukuu.

Aidha, kifungu cha 103 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali zaMitaa, Sura ya 292 kinasema, Nanukuu:

“hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigajikura katika uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa naumma ndani ya umbali wa mita mia tatu ya mlango wowote wakuingilia katika jengo, atavaa au kuonyesha kadi, upendeleo au 4nembo yoyote inayoashiria kumuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”Mwisho wa kunukuu.

Kifungu cha 5 cha Sheria ya Adhabu, Sura Na. 16 kinaelezamaana ya njia ya Umma.

Nanukuu:

“Public way includes any highway, market place, square, street,bridge or other way which is lawfully used by the public”

Mwisho wa kunukuu.

Vifungu vya Sheria zote kwa pamoja havisemi wala kutoa fursa aunafasi kwa wananchi kukusanyika bali zinapiga marufuku nakukataza uvaaji wa sare, au nembo au alama za Vyama vya Siasasiku ya kupiga kura kwa umbali kati ya mita 200 na 300.

Hivyo basi ieleweke kwamba umbali huo wa mita 200 mpaka 300sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio chakulinda kura.

Aidha, uzoefu unaonesha kwamba, katika kampenizinazoendelea, pale ambapo wafuasi wa vyama tofautiwanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa nasehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafamajeruhi na uharibifu mali.


Source: http://www.nec.go.tz/uploads/documents/en/1444402411-MAELEKEZO YA TUME SIKU YA UCHAGUZI.pdf

katika sheria zote hizo hakuna inayozuia wananchi kukaa umbali wa mita 200 wakisubiri matokeo au kulinda kura hakuna.
 
Wee unajiita Mr,chin Mara zote nakwambia kichwani sijui umejaza nini,unashindwa hata kujua sheria ambayo inakupa haki? Kuwa mbali 200m ,hata wwe unayo haki kisheria ,nakushauri rudi drs la 1 Mr,chin!
 
Au kwamba tume imefunga radio majimbo yote kwamba kila yakitoka yatawatangazia wapiga kura wa jimbo ilo matokeo. na nini umuhimu wa kutangaza matokeo kama wahusika mmewafukuza wakae majumbani mwao? Hiyo waliona wapi duniani wapiga kura wanamaliza kuiga kura wanatimliwa kwenda kulala majumbani mwao? Kwani wakikusanyika na kupiga story sheria ipi inakataza? Maana Katiba inaruhusu watu kwenda mahali popote wanakotaka mradi hawavunji sheria ya nchi.

Ni kweli kabisa hakuna sheria inayomtimua mwananchi kufanya anachotaka kufanya.Maana sheria inajitukuza kwenye kosa tu,lakini kama hakuna kosa sheria si kitu tena.
 
Ukifanya fujo utakua umevunja sheria za nchi ambazo Polisi ambao ndio wanao hakikisha na au enforce USALAMA WA RAIA watakushughulikia na kukuweka mahali pema Keko. Don't worry, wewe anzisha fujo tu na subiri uone mkono wa Serikali utakavyo kufunza adabu huku Lowassa akiwa amejituliza nyumbani kwake.

Sheria hiiihii ambayo inaanza na kuvunjwa na vingoz wa juu wa ccm
 
Hebu angalia hao Ukawa waliotakiwa kuwa watetezi wa katiba ya wananchi wanavyofanya sasa hivi. Unawaamini kweli hawa jamaa, wakati wao wenyewe ndio vinara wa kuvunja katiba zao?

Kama ni kuvunja katiba zao, vyama vyote vimevunja lakini kwa kiwango tofauti. Kwa jinsi unavyoandika nakuona ni mtu mwenye "good reasoning", kutokana na hilo naamini unaelewa nani aliikataa katiba ya wananchi. Kama ulifanikiwa kupitia vifungu vichache vya rasimu ya katiba ya wananchi naamini utaichukia CCM kwa kuikataa ile rasimu na kuleta kile walichokiita katiba pendekezwa ambayo ni kwa manufaa ya CCM tena kwaajili ya "wenyewe wenye nayo" nikiamini wewe humo katika hao "wenye nayo".

Kwa kuikataa tume huru ya uchaguzi na mambo mengine ya msingi kwa watanzania, unaweza kuelewa kwanini watu wenye uelewa wanaichukia CCM, samahani kama wewe unaipenda lakini nazungumzia wale wanaoichukia. Hili la kwamba UKAWA wanavunja katiba yao (zaidi ya kumpitisha Lowassa bila uchaguzi), sijui unaweza kulielezea japo kwa ufupi?
 
Nipe kifungu kinachomkataza raia wa Tanzania kukaa mita 200 akifurahia mandhari inayozunguka eneo alilopigia kura
 
Nani kasema ukawa ndo wanaweza ibiwa kura tu? Hata ccm wanaweza ibiwa vilevile, ukawa ccm act wote tulinde kura zetu,


Wewe mgeni tz historia inaonesha jinsi upinzani wanavyoibiwa kura.....mrema hata kura yake hakuiona mnyika nk
 
Wasomi Wetu Wananishangaza Sana, Unakutwa Mtu Anajiita Mwanasheria Wakati Hata Baadh Ya Sheria Hazijui, Nina Mashaka Sana Kama Waafrika Tutaacha Uzembe Wa Kujisomea Maandiko Mbalimbali,
Sheria INARUHUSU MTU KUENDELEA NA SHUGHULI ZAKE ZA KAWAIDA KWA UMBALI WA MITA 200 KUTOKEA KITUO CHA KUPGA KURA ,NA SI KUKUSANYIKA PALE KULINDA KURA, ANAYERUHUSIWA KUKAA PALE KITUON KULINDA NA KUHAKIKI KURA NI WAKALA WA CHAMA HUSIKA,;

MAON; natoa wito TAKUKURU wasambaze maafisa wao kila kituo cha kupgia kura na wakae ndani, maana hata mkikaa kundi nje eti mnalinda kura haisaidii kama wakala wenu ana matatizo chungu nzima, ada ya watoto ,kodi, madeni, alafu apatiwe milion 10, kubadili matokeo, tena anahamishiwa kwa mpesa hapo chumbani sijui kama anaweza kukataa, na mtakaokuwa mita 200 ndo nashangaa mtajuaje hyo, nakushauri mbowe tumia akili hyo,

Hapo kwenye bold... HIVI KULINDA KURA SIYO SEHEMU YA SHUGHURI MBALIMBALI ZA MTU ANAZORUHUSIWA KUZIFANYA UMBALI WA MITA 200 TOKA KITUO CHA KUPIGIA KURA...??? If not, then niambie hizo shughri ,mbalimbali ni zipi..
 
hata wewe sheria pia hujui,kuendelea na shughuli nyingne anaweza kutia ndani ulindaji wa kura, ukiachana na tendo la upigaji kura,huwezi kukaa mita 200 ukisubiri kupiga kura wakati ulishapiga...
Mimi ntakaa mita 200 nikiendelea na shughuli nyingne a.k.a kulinda kura
 
Unakumbuka kile kilichotaka kufanyika Nyamagana na Ubungo katika uchaguzi wa 2010 na kikazuiwa na waliokuwa wanalinda kura?. Kama kura zisingelindwa majimbo haya yangeenda CCM kama yalivyoenda majimbo ya Magu na
Shinyanga mjini. Tutainda kura zetu ndani ya sheria!!!!
 
Hiyo ELIMU ELIMU ELIMU. ya Lowassa ingeanzia hapo chamani kwanza maanake kuna viongozi wengi mbumbumbu na wanaaminika kwa wafuasi wao ambao ni zaidi ya mataahira.

Nashauri vyombo vya ulinzi na usalama wawepo kadhaa kwenye kila kituo kuhakikisha hakuna nungunungu wanaokusanyika hata umbali huo.
 
Back
Top Bottom