Elections 2015 Hakuna kifungu cha sheria kinachomruhusu mpiga kura kukaa nje ya mita 200 toka kituoni akilinda kura

we ulieandika huu uzi una akili fupi sana hata kama chuo kikuu, kwa hayo mawazo yko bs bdo huna akili. hebu jifikirie tena afu urudi hapa.
 
Ipo sheria ya nchi inayozuia watu kukusanyika bila ya kibali, yaani kilichokatazwa ni baada ya kupiga kura kukaa kikundi mahali kwa maana ya kukusanyika hili haliruhusiwi na hiyo sheria ipo ya kuzuia kukusanyika kama huwa mnakusanyika kundi kubwa la watu mahali pamoja na hakuna kinachotokea ni kwamba wameamua kutowafwatilia tu rejea zamani wazururaji hovyo walivyokuwa wanakamatwa au watu wasiokuwa na kazi maalumu!

Na hii ni Dunia nzima kila nchi ina hizi sheria za kuzuia mikusanyiko ya watu bila ya kibali maalumu kutoka kwa wahusika, hivyo siyo jambo geni!

Ebu Mnaojua Sheria mtumie ujuzi wenu kuwaelimisha hawa Vijana wa Ukawa kabla hatujawapoteza maana wanadhani sheria za Uchaguzi zinazifanya Sheria za Maandamano/Mikusanyiko kuwa Inactive
 
Kinachopigwa mkwara ni kukusanyika watu. Kulipo na mkusanyiko kunakuwa na mob saikoloji ambayo ni rahisi kuanzisha vurugu. Mfano mmekusanyika mita 200, harafu mtu mmoja kwa makusudi kabisa anawaambia humo ndani wanachakachua kura sasa hivi, swali je mtabaki mita 200 ama mtavamia kutuo na kufurumusha sandaku za kura?

Ukawa, mnafahamu mtashindwa ila mnajenga mazingira ya fujo.
 
Kinachopigwa mkwara ni kukusanyika watu. Kulipo na mkusanyiko kunakuwa na mob saikoloji ambayo ni rahisi kuanzisha vurugu. Mfano mmekusanyika mita 200, harafu mtu mmoja kwa makusudi kabisa anawaambia humo ndani wanachakachua kura sasa hivi, swali je mtabaki mita 200 ama mtavamia kutuo na kufurumusha sandaku za kura?

Ukawa, mnafahamu mtashindwa ila mnajenga mazingira ya fujo.
 
Haiwahusu waangalizi hao na wala haihusu silaha! Bila ulinzi wa kura uchaguzi uliopita Sio Lema wala Mnyika wala Wenje wala Sugu wala Mdee wala Msigwa na wengine ambao wangalikuwa wabunge. Kwa uwepo wa watu walio mita mia moja wizi ulishindikana na utangazaji ukaahirishwa hadi muda wa majeruhi! Ikawa haiwezekani kuchakachua na kutangaza! Mradi CCM walisema kuwa hata kwa goli la mkono watashinda, ni jukumu letu kufanya kila tuliwezalo kuzuia hilo pasipo kuvunja sheria. Tutakaa umbali ambao sheria inaruhusu. Hatukubali.
Kipindi cha uchaguzi wa lema polisi waliwaachia watu kusimama ndani ya mita 100 karibu na ofisi za halmashauri na wananchi walitishia kumduhuru lema.ndio unachokitaka hiki?
 
Mh Mbowe na viongozi wengine wamekuwa wakiwahamasisha wapiga kura kulinda kura zao siku ya uchaguzi kwa kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura.
Tume ya Taifa ya uchaguzi,NEC, na Rais kikwete wameendelea kusisitiza kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha sheria,na watakaofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Sasa kama ni kinyume cha sheria kwa nini vyombo vya ulinzi na usalama hususani Polisi wasiwachukulie hatua viongozi wa UKAWA wanaowahamasisha wafuasi wao kulinda kura kwa kigezo cha uchochezi wa uvunjifu wa amani? vinginevyo naona ni kuwatisha tu wapiga kura maana hakuna sheria itakayovunjwa kwa kukaa mita 200 na hivyo hakuna kesi kwa wote watakaokaidi amri hiyo, CCM iache woga maana wamekazania sana hiyo hoja utafikiri hao walinda kura wa UKAWA watakuwa eneo hilo na silaha za kivita.
 
Tanzania tuna utamaduni wa kukusanyika vijiweni kupiga stori au kujadili mambo mbalimbali ya kijamii au matukio, fursa kama hii walioikosa katika nchi zao wameibukia kupindua serikali zao ama kukosa amani,kwa watanzania hii ni njia ya kukuza kujenga amani na utulivu kwani hapo vijiweni watu hutoa madukuduku yao yote kwa mazungumzo aidha ya mabishano au jazba na hatimae huelekea makwao kulala,ukizuia hali hiyo utazusha jingine kubwa zaidi na lenye hasara kama vile kuuwana,vita nk.Utaratibu huu ni mzuri uendelezwe kukuza mshikamano na umoja wetu,tulumbane sana vijiweni yaishie hapo,ukizuia malumbano,mabishano,vijiwe ,watu watapigana na hatimaye nchi haitakalika .
 
Kuna kura za thermos na hotpot! Hayo yalifanyika Arumeru kwa Nasari. Ndio maana ja,aa wameng'ang'ania hilo ili wacheze Uruguai au kata funua.
 
Nenda kakae kituo cha kipigia kura uione kazi,

Huyo Mbowe akishapiga kura ataingia mitini, hutomuona karibu ya kituo.

Wajinga Ndiyo Waliwao.
 
Mbona watu wanasema kura zinaibwa. Mbona wanasema tusilinde. Mbona wanazusha vitu mbalimbali. Kama leo nimeona picha ikimuonesha Mbowe kashika kiroba nikaju imetengenezwa. Je sio dhambi ? kufikiri tu kabla ya kutenda ni dhambi. Kuna hawa watu wa IT masaki. Sijui kweli sijui. Mbinu za kuiba kura ndio zimeshaiva hivyo. Leo nimemuona mtu mzima akiongea na kusema sheria ipo lakini kwa mazingira tuliyonayo tukae mbali na vituo. Je mazingira tuliyonayo ni yapi? Hilo ni suala nyeti la kujiuliza. Kweli mtu mzima unaongea hayo maneno mbele ya watu milioni 45.

Mbinu inayotumika hapa ni kubwa sana. Kuwanunua mawakala na viongozi kadhaa wa taasisi fulani ili kuharibu uchaguzi. Mimi nasikitika sana kumuona mtu mzima akijipanga mbele ya wanahabari huku nikimtazama najua kabisa alikuwa anatumika
 
Nimeona hiyo habari na zaidi anaposema kubalini matokeo ,na kifuatie kuyarekebisha yaliotokea kwa uchaguzi ujao !! Nilishangaa na kufikiri sana na kuona sio bure ,ipo namna ,maana huu si uchaguzi wa mwanzo ,

sasa watu wakae tu wadhulumiwe wakubali ? watu wajitarishe kuiba kura waangaliwe tu ! Hii nchi sasa inaelekea kubaya.

Na sio nchi inaelekea kubaya bali inapelekwa kubaya ,na itaelekea huko ,ule wakati wa piga tajama umepitwa na wakati ,Tume ya UCHAGUZI ni lazima ifahamu kuwa hii sio vita ya Lowasa na CCM,mbowe na CCm Seif sharifu na CCm bali hii ni vita kati ya wananchi na CCM.

Wananchi wameshaisha kusema hata likiwekwa jiwe watalichagua jiwe na sio CCM ,kwa maana hiyo watu wapo tayari kwa lolote ,kufa ni second chache tu na haswa ukipigwa risasi hata hujui kama umekufa ,wajeshi wanalielewa funzo hilo.

Kama Tume inalazimishwa na CCM basi wajiondoe tu kwenye tume kwa kupinga shinikizo la serikali ya CCM kwani wananchi hawatokubali na sio Chadema au CUF au wengine.
 
MAZOEA YA KUWEPO UMBALI WA MITA 200 AU 300 KUTOKAKITUO CHA KUPIGIA KURA

Kumekuwepo na mazoea kwamba, baada ya kupiga kura wafuasiwa vyama hubakia na kukaa kwenye maeneo ya kupigia kuraumbali wa mita 100 au 200 au 300.Jambo hili ni kinyume na Sheria za Uchaguzi. Kwani, katikakifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343kinasema nanukuu

“Hakuna mtu atakayefanya Mkutano siku ya kupiga kura au;ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika uchaguziunaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita miambili yajingo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleoau nembo nyingine inayoonesha kuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”

Mwisho wa kunukuu.

Aidha, kifungu cha 103 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali zaMitaa, Sura ya 292 kinasema, Nanukuu:

“hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigajikura katika uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa naumma ndani ya umbali wa mita mia tatu ya mlango wowote wakuingilia katika jengo, atavaa au kuonyesha kadi, upendeleo au 4nembo yoyote inayoashiria kumuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”Mwisho wa kunukuu.

Kifungu cha 5 cha Sheria ya Adhabu, Sura Na. 16 kinaelezamaana ya njia ya Umma.

Nanukuu:

“Public way includes any highway, market place, square, street,bridge or other way which is lawfully used by the public”

Mwisho wa kunukuu.

Vifungu vya Sheria zote kwa pamoja havisemi wala kutoa fursa aunafasi kwa wananchi kukusanyika bali zinapiga marufuku nakukataza uvaaji wa sare, au nembo au alama za Vyama vya Siasasiku ya kupiga kura kwa umbali kati ya mita 200 na 300.

Hivyo basi ieleweke kwamba umbali huo wa mita 200 mpaka 300sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio chakulinda kura.

Aidha, uzoefu unaonesha kwamba, katika kampenizinazoendelea, pale ambapo wafuasi wa vyama tofautiwanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa nasehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafamajeruhi na uharibifu mali.


Source: http://www.nec.go.tz/uploads/documents/en/1444402411-MAELEKEZO YA TUME SIKU YA UCHAGUZI.pdf
 
Nenda kakae kituo cha kipigia kura uione kazi,

Huyo Mbowe akishapiga kura ataingia mitini, hutomuona karibu ya kituo.

Wajinga Ndiyo Waliwao.

Bibie kesho nikitoka Al-jumaa nitapita kuja kula Pilau ya kuku, naomba uniwekee sahani 2 nitakuja na kaka yangu
 
Kipindi cha uchaguzi wa lema polisi waliwaachia watu kusimama ndani ya mita 100 karibu na ofisi za halmashauri na wananchi walitishia kumduhuru lema.ndio unachokitaka hiki?
Unaongea kitu nisichokijua samahani!
 
Back
Top Bottom