Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,787
Matatizo mengi sana kwenye jamii yangeepukika kama tungeilewa vema hii kanuni ya impermanence, kwamba kila kitu kinapita na hakuna kitakachodumu milele!
Tunapokuwa na mapenzi yaliyopitiliza kwa baadhi ya vitu tunajijengea ugonjwa mbaya sana utakaokuja kutuumiza na kuleta madhara makubwa mara vile vitu vikitutoka au vikikoma kuwa vyeti kwa sababu yoyote ile.
Tujifunze kuikubali hii kanuni ili vile vyote tunavyovimiliki siku vikiondoka tusiumie sana na yasiwepo madhara, watu wamejiuwa au wameuwa au kuwaumiza wengine kwasababu tu ya mapenzi, watoto wamejeruhiwa kwasababu wamepoteza au kuharibu chombo au kifaa cha nyumbani, wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.
Hatuna umiliki wa kudumu kwenye chochote kile utafika wakati vinakoma kuwa vyetu na vitatuondoka kwa njia tofauti kama wizi, kuharibika, kupotea nk. kwa jinsi hii tutaponya majeraha mengi na kupunguza athari nyingi pindi vikomapo kuwa katika milki yetu.