Hakuna kidumucho milele-the law of impermanence

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,679
2,000
Matatizo mengi sana kwenye jamii yangeepukika kama tungeilewa vema hii kanuni ya impermanence, kwamba kila kitu kinapita na hakuna kitakachodumu milele!

Tunapokuwa na mapenzi yaliyopitiliza kwa baadhi ya vitu tunajijengea ugonjwa mbaya sana utakaokuja kutuumiza na kuleta madhara makubwa mara vile vitu vikitutoka au vikikoma kuwa vyeti kwa sababu yoyote ile.

Tujifunze kuikubali hii kanuni ili vile vyote tunavyovimiliki siku vikiondoka tusiumie sana na yasiwepo madhara, watu wamejiuwa au wameuwa au kuwaumiza wengine kwasababu tu ya mapenzi, watoto wamejeruhiwa kwasababu wamepoteza au kuharibu chombo au kifaa cha nyumbani, wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.

Hatuna umiliki wa kudumu kwenye chochote kile utafika wakati vinakoma kuwa vyetu na vitatuondoka kwa njia tofauti kama wizi, kuharibika, kupotea nk. kwa jinsi hii tutaponya majeraha mengi na kupunguza athari nyingi pindi vikomapo kuwa katika milki yetu.
 

HARUFU

Platinum Member
Jan 21, 2014
28,302
2,000
matatizo mengi sana kwenye jamii yangeepukika kama tungeilewa vema hii kanuni ya impermanence, kwamba kila kitu kinapita na hakuna kitakachodumu milele! tunapokuwa na mapenzi yaliyopitiliza kwa baadhi ya vitu tunajijengea ugonjwa mbaya sana utakaokuja kutuumiza na kuleta madhara makubwa mara vile vitu vikitutoka au vikikoma kuwa vyeti kwa sababu yoyote ile. tujifunze kuikubali hii kanuni ili vile vyote tunavyovimiliki siku vikiondoka tusiumie sana na yasiwepo madhara, watu wamejiuwa au wameuwa au kuwaumiza wengine kwasababu tu ya mapenzi, watoto wamejeruhiwa kwasababu wamepoteza au kuharibu chombo au kifaa cha nyumbani, wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu. hatuna umiliki wa kudumu kwenye chochote kile utafika wakati vinakoma kuwa vyetu na vitatuondoka kwa njia tofauti kama wizi, kuharibika, kupotea nk. kwa jinsi hii tutaponya majeraha mengi na kupunguza athari nyingi pindi vikomapo kuwa katika milki yetu

Ni kweli mkuu hujakosea na sisi binadamu tunajisahau sana hapa duniani na kujiona kama tutakuwepo milele kumbe ni mapito tu.

Ujumbe umefika
 

patience96

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
1,327
1,500
Ni kweli mkuu hujakosea na sisi binadamu tunajisahau sana hapa duniani na kujiona kama tutakuwepo milele kumbe ni mapito tu.

Ujumbe umefika

Mkuu, bila kujisahau japo kiasi, hatungeweza kufanya jambo lolote la maendeleo hapa duniani. Maana muda mwingi tungekuwa tunafikiria kufa tu.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,679
2,000
Mkuu, bila kujisahau japo kiasi, hatungeweza kufanya jambo lolote la maendeleo hapa duniani. Maana muda mwingi tungekuwa tunafikiria kufa tu.

tukiwa hai tufanye yale yatupasayo kufanya lakini tusiwe attached na vile tunavyovipata kwenye mchakato wa mafanikio ya kimaisha, tuvilinde tuvitunze lakini tuwe na roho ya kujua kwamba havitakuwepo milele
 

Konya

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
918
250
na hapa ndipo binadamu walio wengi tunapojisahau, hakuna kitakachodumu au kitakachoishi milele kwenye hii dunia, hata uhai wako, itafika mahali utakoma.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,679
2,000
Unaweza kunisaidia maana ya "kila kitu"?
Halafu ukishanisaidia hilo unisaidie kama kuna anaejua "kila kitu"

Mtoa mada amenichanganya!

Eiyer Nothing last forever! tunapongelea 'kila kitu' yaani 'every-thing' manake kuna 'no-thing' je umenipata au ndo nimezidi kukuchanganya?
 

rubwe

Senior Member
Feb 12, 2013
107
195
matatizo mengi sana kwenye jamii yangeepukika kama tungeilewa vema hii kanuni ya impermanence, kwamba kila kitu kinapita na hakuna kitakachodumu milele! tunapokuwa na mapenzi yaliyopitiliza kwa baadhi ya vitu j tunajijengea ugonjwa mbaya sana utakaokuja kutuumiza na kuleta madhara makubwa mara vile vitu vikitutoka au vikikoma kuwa vyeti kwa sababu yoyote ile. tujifunze kuikubali hii kanuni ili vile vyote tunavyovimiliki siku vikiondoka tusiumie sana na yasiwepo madhara, watu wamejiuwa au wameuwa au kuwaumiza wengine kwasababu tu ya mapenzi, watoto wamejeruhiwa kwasababu wamepoteza au kuharibu chombo au kifaa cha nyumbani, wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu. hatuna umiliki wa kudumu kwenye chochote kile utafika wakati vinakoma kuwa vyetu na vitatuondoka kwa njia tofauti kama wizi, kuharibika, kupotea nk. kwa jinsi hii tutaponya majeraha mengi na kupunguza athari nyingi pindi vikomapo kuwa katika milki yetu
Ahsante kwa ujumbe mzuri na ni somo linaloweza kutuondolea stress baadae manake ya kesho hatuyajui
 

Kisima

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
3,807
2,000
Lakini mkuu mshana jr hii mada umeigeneralize sana! nijuavyo mimi mwanzo/sifa kuu ya kumiriki kitu kizuri ni sharti ukipende sana then unakomaa kuhakikisha kwamba unaikipata!
Sasa ukinzani unakuja pale ambapo inatokea ghafla kitu hicho kinatoweka ktk uhalali wa kukimiriki wakati ndo kwaanza mahaba nacho hayajafikia hata robo ya kuridhika na kusherehekea kupatikana kwacho.... Hapo ndo mtu hupatwa na msongo wa mawazo ktk kutoweka kwake!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom