Hakuna kama mh. J.Kikwete

pcman

JF-Expert Member
Oct 9, 2008
742
186
Ni raisi pekee:
1.Aliye mpole na asiye na papara katika mambo yake
2.mwenye huruma na utu, hakusi kuhudhuria misiba muhimu, kutuma salamu za rambirambi, kutembelea wagonjwa, n.k
3.Anayeweza kukuita ikulu na ukaenda bila woga
4.Anayependwa na wana CCM hatakushinda tena nafasi ya uenyekiti
5.Asiye mchoyo, na ndio maana katika safari zake nyingi za kututafutia maendeleo huwa anaambata na watu wengi.
6.Anayependa kupata hekima kutoka kwa wazee wa dar na hivyo kuiendesha nchi ipasavyo, kama wazee wanavyo mshauri
7............
8................
 
katika hayo kajitahidi...........
7:kaboresha miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami sehemu nyingi mikoani
8:ni raisi pekee niliewahi kumsikia akiwahoji live,r.p.c,dc,na watendaji mbali mbali wa serikali juu ya utendaji wao,mbele ya mamia ya wananchi
9:kaboresha upatikanaji rahisi wa maji safi na salama sehemu nyingi mikoani
10:ni mwana c.c.m pekee anaelinde heshima ya chama isiharibike,wengine bla bla nyingi sana!na nivyema wanachama wote wangeiga mfano wake
11:kaboresha sehemu kubwa ya ulinzi na usalama wa taifa,kwani matukio ya wizi wa kutumia silaha za moto yamepungua kiasi kikubwa sana
12:ni raisi ambae wa tanzania wengi watamkumbuka baada ya muda wake kuisha kwa busara zake,uvumilivu wake,utendaji kazi zake,ukweli wake,kupenda kwake ushirikiano,na kwa uzoefu wangu binafsi ni raisi ambae hajivuni na anaishi kama mtu wa kawaida tu.
 
Yaani we kibuyu kweli!
Kwa hiyo mwombe agombee kipindi cha tatu basi.
Nionavyo mimi huo ni wajibu wake,kwa hiyo wewe unataka asicheke,au wananchi wasiende ikulu!

Ndio tatizo la shibe hilo,ukishiba sana halafu huna kazi ya kufanya,ndio madhara yake haya.

Anyway,uwezo wako wa kufikiria ndio umeishia hapo ndugu yangu.
Pole sana.
 
weka ushabiki wa vyama pembeni na kubali ukweli!!
je aliezungumza member mtoa hii mada katika mtiririko wake ni ya kweli ama???????????
 
Mpenda UFISADI, na kupandisha garama za maisha kwa kila mtanzania, elimu na afya duni. Rais aliyepoteza mwelekeo wa taifa hili kwa ujumla. Hakustahili kuwepo katika nafasi hii ya urais.
 
weka ushabiki wa vyama pembeni na kubali ukweli!!
je aliezungumza member mtoa hii mada katika mtiririko wake ni ya kweli ama???????????

Mkuu tuliza akili kwanza. Hoja hapa ni je,yote hayo uliyoyasema,sio wajibu wake? Kwa akili yako wewe unaona ni favour,katufanyia? Yeye kwa nafasi na kipindi chake anawajibu wa kutenda yote hayo uliyosema.Ushabiki wa vyama umeuOna wapi sasa. Na unawezaje kujua nina mapenzi na chama gani? Kuwa great thinker mkuu.

Lakini mbona hujasema mengine aliyoahidi kufanya na bado hajafanya,na ni wazi hatayafanya hadi anaondoka madarakai.
Hakuuna mtu amekataa kama hajafanya hayo uliyosema,ila ukae unajua huo ni wajibu wake kikatiba. Na sisi wananchi tunasubiri atimize ahadi zote alizotuahidi tukampa kura zetu. Na vipi mbona hujasema jinsi anavyoshughulikia maswala ya ufisadi na udini vinavyotishia ustawi wa taifa letu.
 
Kweli hakuna kama yeye...........anashangaa nanasi ya Ghana wakati marehemu mama yake kazaliwa Kiwangwa

Rais-JKakikagua-shamba-la-mananasi.jpg
 
Acheni ushamba hashangai mananasi anayafananisha na ya kiwangwa.......kuhusu ahadi wewe baba yako aliyekuzaa ameahidi mangapi na hajayatekeleza???
 
Ni raisi pekee:
1.Aliye mpole na asiye na papara katika mambo yake
2.mwenye huruma na utu, hakusi kuhudhuria misiba muhimu, kutuma salamu za rambirambi, kutembelea wagonjwa, n.k
3.Anayeweza kukuita ikulu na ukaenda bila woga
4.Anayependwa na wana CCM hatakushinda tena nafasi ya uenyekiti
5.Asiye mchoyo, na ndio maana katika safari zake nyingi za kututafutia maendeleo huwa anaambata na watu wengi.
6.Anayependa kupata hekima kutoka kwa wazee wa dar na hivyo kuiendesha nchi ipasavyo, kama wazee wanavyo mshauri
7............
8................

1.Ni kweli ni mpole asiye na papara na mambo,na ndio maana yaende tu yanavyotaka. Mfumuko wa bei uende tu unavyotaka,udini uende unavyotaka,ufisadi uende tu unavyotaka,makundi ktk chama yaende tu yanavyotaka nk..nk..

2.Kwa kuwa yeye sio binadamu wa kawaida,so kitendo cha kuhudhuria misiba,rambirambi na kutembelea wagonjwa ni favour ya pekee anayotufanyia sisi kama waja wake!

3.Kwa kuwa ikulu ni peponi ambapo binadamu wa kawaida huwezi kwenda ni hadi ufe. Lakini pia kwa kuwa ikulu hakwenda kutokana na kura yako na yangu,hivyo hatuna haki ya kufika huko hata kama tuna shida gani.

4.Kwa kuwa hakuna makundi ktk chama.Na vile vile hakuna vipeperushi vilivyokuwa vinahimiza wanachama wa mkutano mkuu 'wampunguzie majukumu rais wetu'.Pia haijawahi kutokea mwenyekiti akaongezewa muda wa kukiongoza chama,hii imetokea kwake pekee. Ndio maana tunasema hakuna kama yeye!

5.Katika hili nakuunga mkono100%.Ndio maana hata unaamini kuwa maendeleo ya wananchi yatatoka nje ya nchi,hivyo hakuna haja ya kutumia muda wake mwingi nyumbani kuhimiza na kusimamia shughuli za maendeleo ya wananchi.Mimi nashauri,uandaliwe utaratibu wa wananchi wote kwenda huko kuchota maendeleo yetu.

6.Kweli huyu ni wa kwanza,hakuna rais mwingine aliyewahi kukaa na wazee.Kitendo cha kuhutubia taifa na wazee wa Dar es Salaam ni cha pekee na cha kupigiwa mfano.Maana wazee wanapata nafasi ya kushauriana naye,wanamuuliza maswali anayajibu na bahati nzuri wazee wetu hawa wengi sio wa chama.Mambo burudani kweli!

7....

8........

Na mengine mengi sana,yasiyoweza kuhesabika!
 
Ni raisi pekee:
1.Aliye mpole na asiye na papara katika mambo yake
2.mwenye huruma na utu, hakusi kuhudhuria misiba muhimu, kutuma salamu za rambirambi, kutembelea wagonjwa, n.k
3.Anayeweza kukuita ikulu na ukaenda bila woga
4.Anayependwa na wana CCM hatakushinda tena nafasi ya uenyekiti
5.Asiye mchoyo, na ndio maana katika safari zake nyingi za kututafutia maendeleo huwa anaambata na watu wengi.
6.Anayependa kupata hekima kutoka kwa wazee wa dar na hivyo kuiendesha nchi ipasavyo, kama wazee wanavyo mshauri
7............
8................

katika hayo kajitahidi...........
7:kaboresha miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami sehemu nyingi mikoani
8:ni raisi pekee niliewahi kumsikia akiwahoji live,r.p.c,dc,na watendaji mbali mbali wa serikali juu ya utendaji wao,mbele ya mamia ya wananchi
9:kaboresha upatikanaji rahisi wa maji safi na salama sehemu nyingi mikoani
10:ni mwana c.c.m pekee anaelinde heshima ya chama isiharibike,wengine bla bla nyingi sana!na nivyema wanachama wote wangeiga mfano wake
11:kaboresha sehemu kubwa ya ulinzi na usalama wa taifa,kwani matukio ya wizi wa kutumia silaha za moto yamepungua kiasi kikubwa sana
12:ni raisi ambae wa tanzania wengi watamkumbuka baada ya muda wake kuisha kwa busara zake,uvumilivu wake,utendaji kazi zake,ukweli wake,kupenda kwake ushirikiano,na kwa uzoefu wangu binafsi ni raisi ambae hajivuni na anaishi kama mtu wa kawaida tu.
Ni Rais gani ambaye hakufanya haya? Ni nini kinachomfanya Kikwete aonekane special, tofauti na wenzake ambao walifanya hayohayo anayoyafanya huyu na kuipelekea nchi kuwa masikini kama ilivyo?
 
Acheni ushamba hashangai mananasi anayafananisha na ya kiwangwa.......kuhusu ahadi wewe baba yako aliyekuzaa ameahidi mangapi na hajayatekeleza???

Ndugu yangu tuliza akili. Mbona unapenda sana kukisia mambo. Ukizoea hivyo utaanza hata kukisia maisha yako. Wewe umejuaje kama baba ameahidi mangapi na hajatekeleza? Kama mzee alikuahidi mengi halafu ameshindwa kukutekelezea,huyo ni wewe tu.Si kila mzee ameshindwa kutimiza ahadi alizomwahidi mwanae.Nikwambie kitu ndugu yangu,kama wewe ni mzazi mzuri huna sababu ya kuahidi vitu usivyokuwa na uwezo wa kuvitekeleza.Na hapo ndipo utakuwa unakosea,na heshima yako ndio basi tena.Kwanini uwe mzee mwongo mwongo?
 
Back
Top Bottom