Hakuna jambo gumu katika Siasa

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,098
2,000
Baada ya Uchaguzi kumalizika na matokeo ya jumla kuonyesha ccm wameshinda kwa asilimia kubwa zaidi kwa kujumlisha na maeneo waliyopita kwa Mapingamizi je ni kweli kuna cha kujivunia?

Wapo wanaccm wasioamini kuwa chama kinaanguka kwa kasi sana tukiangalia Takwimu za hivi karibuni kwa mfano÷
Urais 2005 Ccm ilipata 86%
Miaka mitano tu mbele 61%
Kwa mgombea aliyekuwa na ushawishi zaidi ccm.

Serikali za mitaa 2009 ccm ilivuna 96%
Mwaka 2014 ukiondoa sehemu zenye mapingamizi inaweza kufika 70%.
Sasa ukiangalia hizo takwimu vizuri ni wazi kabisa kuna hatari 2015 kwa ccm kudidimia zaidi kwani wananchi waliowengi wataona kumbe hata bila ccm maisha yapo tu. Ule woga unatoweka kwa kasi zaidi.

Urais 86 - 61 = 24%
Mitaa 96 - 70 = 26%

Mh. Kikwete mwaka 2011 aliita CC ya CCM na kuwataka kutafuta jibu la kwa nn hali imekuwa hivi.
Mpaka leo hakuna majibu.

Kuondoka ccm 2015 si muujiza tena inawezekana hata wao viongozi wanajua hilo.

Ukiiguza tu hiyo 61% - 12% tu inakuwa habari ingine.
 

Attachments

kkarumekenge

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,710
2,000
Ni mnafiki pekee ambaye haoni kufa kwa CCM 2015 na hata wakiponea chupuchupu 2015, 2020 watang'oka tu!
 

Pesambilli

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
283
225
CCM haifi na haitakuja kufa kamwe.
CCM itakufa tu mkuu. Hapo unajidanganya. Mwanafalisafa na Mwanahistoria nguli wa Ujerumani katika karne ya 19 Karl Marx anataja kanuni moja mhimu sana ya Kihistoria kuwa "Hapa duniani kila kitu kiko kwenye mwendo wa mabadiliko, kitu pekee kisichoweza kubadilika ni mabadiliko yenyewe". Kwa hiyo, kusema CCM haiwezi kufa ni upofu na kujidanganya. Hata Wakoloni walikuwa wanadai wataishi milele kwenye makoloni yao. Lkn leo hatunao tena
 

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,098
2,000
Brazil ilitingisha sana ila ikajikuta taratibu inakufa sasa ni ya 9 kisoka sasa ccm hawawez kukubali kirahis kuwa ndo kwaheri ya kuonana zama za " Ushindi wa Kishindo" zinapotea
 

HIPSON

Member
Mar 19, 2012
61
0
Pesambili una uhakika kuwa hatuna wakoloni? inaonesha bado ni mdogo wa kufikiri; tunalishwa kwa mrija hivi na kuchukuliwa rasilimali zetu kijanja halafu unakula maharage na kushiba eti una uhuru????? uhuru uko wapi hapa??? Mtwara walitaka kujitutumua kwa kutaka uhuru wa kuamua matumizi ya rasilimali yao, wooote kwa mashinikizo ya wakoloni mamboleo tuliwapinga bila hata kufikiri!. Hiyo CCM ikipata mkono wa wakoloni itabaki tu, utake usitake weweweeeeeeee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom