mzee wa kubet
Member
- Dec 3, 2017
- 6
- 14
Ndugu zangu,
Kwa sasa ni wakati wa muda muafaka kwa nchi kurudi mfumo wa chama kimoja, mfumo huu utaipa mafanikio makubwa nchi yetu kiuchumi kwani utamfanya Rais wetu afanye kazi bila bughudha na kuleta maendeleo ya kweli.Hili la chama kimoja silisemi mimi tu bali watanzania wote wameamua kuwa CCM ya Magufuli yatosha.
Hii inathibitishwa na matokeo ya Uchaguzi mdogo wa udiwani ambapo CCM ya Magufuli ilipata ushindi wa kishindo zaidi ya asilimia 90, wimbi kubwa la viongozi wa vyama vya upinzani ambao kila kukicha wanahamia CCM, uungwaji mkubwa mkono na wananchi ambao hutoa sifa kede kede kwake na kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yake ya kisiasa.
Kwa hali hii ilivyo nina kila sababu ya kusema hakuna haja ya Upinzani kwa sasa kwani yote waliyokuwa wanapigania MH Magufuli anayafanya kwa kasi kubwa.
Rai yangu kwa wapinzani wachache waliobaki tuungane kumuunga mkono my Rais kwa sasa.