Hakuna haja ya upinzani watanzania wote wanampenda Rais Magufuli

mzee wa kubet

Member
Dec 3, 2017
6
45
Ndugu zangu,

Kwa sasa ni wakati wa muda muafaka kwa nchi kurudi mfumo wa chama kimoja, mfumo huu utaipa mafanikio makubwa nchi yetu kiuchumi kwani utamfanya Rais wetu afanye kazi bila bughudha na kuleta maendeleo ya kweli.Hili la chama kimoja silisemi mimi tu bali watanzania wote wameamua kuwa CCM ya Magufuli yatosha.

Hii inathibitishwa na matokeo ya Uchaguzi mdogo wa udiwani ambapo CCM ya Magufuli ilipata ushindi wa kishindo zaidi ya asilimia 90, wimbi kubwa la viongozi wa vyama vya upinzani ambao kila kukicha wanahamia CCM, uungwaji mkubwa mkono na wananchi ambao hutoa sifa kede kede kwake na kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yake ya kisiasa.

Kwa hali hii ilivyo nina kila sababu ya kusema hakuna haja ya Upinzani kwa sasa kwani yote waliyokuwa wanapigania MH Magufuli anayafanya kwa kasi kubwa.

Rai yangu kwa wapinzani wachache waliobaki tuungane kumuunga mkono my Rais kwa sasa.
 
Naminipo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
506
1,000

Siyo kweli? Ulikuwepo wakati mfumo wa vyama vingi unaanzishwa? Kwanini mfumo wa sasa ulipitishwa hata kama matokeo ya maoni yalikuwa yakipendelea chama kimoja? Kama kiongozi wa sasa amefunika kama unavyotaka kutuaminisha kuna sababu gani ya kuhangaika hata kubafili mfumo? Ok ikitokea kiongozi ws sasa akamaliza mihula yake kisha akaja ambae hafikii viwango tutarudi tena kwenye mfumo wa vyama vingi? Mfumo uliopo uendelee, vyama vitakuwa dhaifu au imara kwa nyakati mbalimbali na ndiyo maisha yenyewe.
 
usatrumpjr

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
2,243
2,000
Kwn upinzani unamfanya magufuli asijenge nchi inamaana wapinzani wanambugzi jamaa?
 
mtana76

JF-Expert Member
May 31, 2015
502
500
Kweli naamini % kubwa ya Watanzania ni mbumbumbu. Elimu ya kufahamu haki zao na umuhimu wa Upanzania inahitajika haraka sana
 
Menyainganyi

JF-Expert Member
Mar 12, 2013
1,172
2,000
Mzee (kijana) wa Kubet..,

Jina lako linasadifu uwezo wa akili yako .. Akili yako ni kama "sponge" . .
Sponji ikiwekwa ktk kimiminika chochote kile, huwa lina tabia ya kunyonya kimiminika hicho ..., bila kujali kama kimiminika hicho ni kisafi ama kichafu ...

Hebu tujiulize swali la msingi..., mfumo wa VYAMA VINGI vya siasa ni kwa ajili ya FAIDA ya watanzania au wanasiasa wachache wa Tanzania .. ?

Jee, kuna faida ya mfumo wa vyama vingi vya siasa , na faida hizo ni zipi ..?

Ni kitu gani hicho alichofanya MTU MMOJA....JPM ..., kwa miaka hii miwili tuu ..., kustahili SIFA ya kuua MFUMO WA VYAMA VINGI vya siasa Tanzania ... ?!
Hebu tujibu kijana wa Kubet ..

Kwa hiyo, inawezekana kabisa pia (Kwa akili za vijana wa kubet wa ccm), kufuta mfumo wetu wa kutoa haki, yaani MAHAKAMA zetu kwa kuwa tumempata Raisi mpenda watu, aliyetokomeza RUSHWA WIZI UMASKINI,mtenda Haki, MSEMA KWELI nae ni mpenzi sana wa mungu ... ?!

Kwamba huyu Raisi JPM anatosha sasa..., nae aendelee kutawala milele..., na hatuhitaji kupiga kura tena ...?!
 
simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
14,942
2,000
Yes,sanamu ya shaba ya Magu iwekwe Dodoma tuisujidie kila jumapili. Magu oyee umetunyosha kweli kweli.
 
Avatar

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
10,827
2,000
Upinzani uendelee kuwepo kuamsha hali ya kiongozi tawala wa sasa,

Pia tusibeze uungaji mkono wa vitu vya tija kwa wananchi wa Tz kwa ujumla wake, na uponzani hisiwe kambi ya kashifu na kukosoa kwa ajili ya maslahi binafsi..

Sina imani na hawa wanao hama hama
 
Abuu Said

JF-Expert Member
Jul 5, 2015
2,849
2,000
Upinzani sio adui wa Serikali, upinzani upo kui pressurize serikali itende mema na kuleta mafanikio kwa Taifa kwa hiyo uache upinzani uendelee kwa faida ya Serikali na Taifa
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,871
2,000
Kama namwelewa hivi mleta mada. Nimeelewa kwamba kwa namna mambo yanavyoenda na jinsi wenyewe wnavyotaka iwe ni kwamba kila mtu aunge mkono na kukubaliana kinachofanywa na serikali hata kama sio sawa. na kwamba hata iweje upinzani hautakiwi hapa Tanzania kwa sababu wote wanalazimishwa kuunga mkono....kwa sababu hiyo hakuna haja ya vyama vya siasa (sarcastically) na kwa sababu hiyo hakuna haja ya mawazo mbadala.....impliedly; hakuna haja ya chaguzi wala uchaguzi Mkuu wa 2020
 
mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,907
2,000
Ndugu zangu,

Kwa sasa ni wakati wa muda muafaka kwa nchi kurudi mfumo wa chama kimoja, mfumo huu utaipa mafanikio makubwa nchi yetu kiuchumi kwani utamfanya Rais wetu afanye kazi bila bughudha na kuleta maendeleo ya kweli.Hili la chama kimoja silisemi mimi tu bali watanzania wote wameamua kuwa CCM ya Magufuli yatosha.

Hii inathibitishwa na matokeo ya Uchaguzi mdogo wa udiwani ambapo CCM ya Magufuli ilipata ushindi wa kishindo zaidi ya asilimia 90, wimbi kubwa la viongozi wa vyama vya upinzani ambao kila kukicha wanahamia CCM, uungwaji mkubwa mkono na wananchi ambao hutoa sifa kede kede kwake na kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yake ya kisiasa.

Kwa hali hii ilivyo nina kila sababu ya kusema hakuna haja ya Upinzani kwa sasa kwani yote waliyokuwa wanapigania MH Magufuli anayafanya kwa kasi kubwa.

Rai yangu kwa wapinzani wachache waliobaki tuungane kumuunga mkono my Rais kwa sasa.
Hivi kumbe kuna vichwa vya aina nyingi hivi
 
mtu chake

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
21,441
2,000
Kama namwelewa hivi mleta mada. Nimeelewa kwamba kwa namna mambo yanavyoenda na jinsi wenyewe wnavyotaka iwe ni kwamba kila mtu aunge mkono na kukubaliana kinachofanywa na serikali hata kama sio sawa. na kwamba hata iweje upinzani hautakiwi hapa Tanzania kwa sababu wote wanalazimishwa kuunga mkono....kwa sababu hiyo hakuna haja ya vyama vya siasa (sarcastically) na kwa sababu hiyo hakuna haja ya mawazo mbadala.....impliedly; hakuna haja ya chaguzi wala uchaguzi Mkuu wa 2020
Nami nimeelewa hivyo, na ninapenda iwe hivyo, maana hkn namna
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom