Hakuna haja ya Uchaguzi 2010! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna haja ya Uchaguzi 2010!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Dec 4, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kwa nini tufanye uchaguzi mkuu huku hatuna fedha za kujifanyia uchaguzi?

  Kwa nini tufanye uchaguzi ambao utajaa rushwa na takrima na umeshaongeza vitendo vya hujuma na ufisadi?

  Kwa nini tuwe na uchaguzi huku tunajua wazi matokeo yatakuwaje kabla hata ya kwenda kupiga kura?

  Kwa nini tusiongeze muda tuwape Wabunge na Rais muda wa miaka 10 kabla ya uchaguzi mkuu, ili kuondokana na upuuzi tulioujengea mapambo kwa jina la Demokrasia?
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Itakuwa watanzania tumepiga hatua ya mabali sana kuona na kuchukua hatua hiyo!
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Inasemekana Abraham Lincoln alihonga pombe wakati wa uchaguzi wake. Je, na Marekani nayo ingesogeza muda wake? Jibu ni hapana. It takes time to perfect a system. Hivyo, we have to bear the load now...in order for a better future ahead. Give it 25 years...(another 5 elections) mpaka watu wajue umuhimu wa uchaguzi...then we will see the fruits. Tatizo kwa sasa ni tuna watu walio maskini kupita kiasi ambao wako tayari kuuza haki yao, kwa sababu hawaoni faida yake. On the other hand...hii inaweza ikawa moja ya sababu ambazo inafanya ccm isilete maendeleo. Maana maendeleo = end of it rulership...
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Uchaguzi ujao Rais hatabadilika labda utokee muujiza au kwa mapenzi ya Mungu. Bunge litabadilika sana. Kwangu mimi hii ni hatua kubwa kuelekea kuing'oa CCM madarakani. Tusiiache nafasi hii ipite. Udhaifu wa Rais tulienae kwa sasa ukitumika vizuri mabadiliko yatakuwepo.
   
 5. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mtu siko zote mjinga kwenda kurudi lazima ataijua njia
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naungana na wewe kabisa maana hakuna haja ya kufanya uchaguzi kabisa maana mambo ni yale yale kila siku
   
 7. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kakudanganya nani kuwa fedha za kufanyia uchaguzi mkuu hazipo? Hazijawahi kukosekana na haitakaa itokee! Parking za magari zitahamia barabarani, watu watakufa njaa, watakosa maji ya kunywa na kuogea, watoto watakaa chini ya miti bila walimu na madawa hospitalini hayatapatikana. Ila uchaguzi mkuu lazima utafanyika bila upungufu wa fedha.

  Rushwa na takrima, hujuma na ufisadi ndio utawala wa leo. Bila hivyo kuwepo, unazungumzia uchaguzi mkuu wa nchi gani? Utawala gani?

  Ni njia mojawapo nzuri ya watu wetu ndani ya chama kupisha madili yao kwa kisingizio cha ufadhili wa uchaguzi na hivyo kujitengenezea utajiri. Oops, hiyo ni sababu ya ndani mno, kwa nje ni ili tuweze kusimama na kutangaza demokrasia na uhuru wa kuchagua licha ya kujua kimsingi ni kiinimacho.

  Ni muda mrefu mno, iwapo tutapata rais wa hovyo itamchukua muda mrefu mno kuachia. Kama unavyojua hatuna utaratibu wa kumwondoa rais madarakani kabla ya muda wake kuisha, hata kama akishindwa majukumu yake. Wala hakuna sababu ya kuliweka kwenye katiba kwa sasa (maana so far marais wana uwezo, itakapoonekana dalili ya vyama vingine kuchukua nchi tutabadilisha katiba).
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  BIG UP BIG MAN !!
  Ninakubaliana nawe 100%, na sababu inayonifanya nifikiriye na nikubaliane nawe ni pale ambapo upinzani tulionao ama kwa kuhujumiwa, bahati mbaya au makusudi bado haujafikia mahali pa kuweza kupambana na wenye mtaji wa uchaguzi (ccm).

  Kwa maoni haya ingekuwa vyema kama vyama vya upinzani vingekubaliana kuwe kuna a certain monitoring system say kila baada ya miaka mitatu kama wako tayari kujipima na chama tawala.Kwaani kinachoendelea sasa hivi ni kwenda kwenye mechi wakati unakuwa unajua kwamba utashindwa, hii kwa watu makini haileti maana.

  Japo kuna tatizo la ahadi zilizotolewa wakati wa first speech ya JK kwamba atashirikiana na kuvilea vyama vya upinzani, kitu ambacho mpaka sasa hivi hakina ushahidi wowote kama kiko applied.
   
 9. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  This discussion might end up being just as useless if we dont recognize the problem at hand. Tatizo sio Uchaguzi, bali ni jinsi uchaguzi unavyoendeshwa. Huwezi kusema tufute uchaguzi. Kuwa na uchaguzi ni essential katika community yeyote. Solution ya tatizo lolote inaanza kwa kuelewa tatizo. Tatizo ni rushwa na takrima. Hili sio tatizo pekee la Tanzania...bali ni tatizo linalosumbua nchi nyingi maskini. The question can be re-phrased to: How do you offer democratic elections to poor people? Sub-questions: Kwa nini mtu anapokea rushwa? Kwa nini bunge letu limeruhusu takrima? Kusema tufute uchaguzi ni kutoelewa maana na kazi ya uchaguzi. Kuelewa hilo inabidi urudi katika basic question la kwa nini tunahitaji serikali/kutawaliwa? Katika jibu lake utakuta basically its for a functionable community. Kwa hiyo kama individuals tuliokuwa forced kuishi pamoja (katika jamii) - lazima tuwe na system ya kuweza kuishi pamoja. Hii ndo basis ya kuwa na serikali/au system fulani ya uongozi. Pia katika jamii yeyote lazima kuwe na conflicts za vision. Mfano mimi nataka kuwe na huduma bure ya afya, wewe unataka huduma bure ya shule. Uchaguzi ndo njia pekee iliyovumbuliwa ya kusaidia ku-solve such a conflict bila kufanya kundi moja lione kuwa limeonewa. Na democracy ni njia inayotumika ku-legitimize the outcome. Watu wengi huwa hawaelewi maana ya demokrasia. Hivyo...kuwa na uchaguzi ni lazima. Swali ni jinsi ya kuboresha huo uchaguzi. Hopefully the discussion will head into this direction, badala kuonyesha kufa moyo na kutaka kuvunja foundations za jamii - yaani kuwa na Uchaguzi wa Viongozi.
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  kumbe tuendelee tu na sirikali iliyopo kwa kipindi kingine bila uchaguzi? ila mawazo yako ni kama sahihi vile
  rais ni yule yule na viongozi ni wale wale hakuna mabadiliko na pesa za uchaguzi hatuna
   
 11. M

  Mwedi Member

  #11
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh,kama kweli vile,mana mshindi anajulikana,chama kinajulikana,kwa nini pesa za eletion zisitumike kufanyia mambo mengine ya maendeleo?mana chaguzi za Afrika duh,aibu,full changa la macho,mwisho wake hukawii kusikia(wakishaibiana kura) basi tuunde serikali ya mseto.
   
 12. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  tatizo ni kwamba hata tusipofanya uchaguzi hizo hela ambazo hatutomia kwenye gharama za uchaguzi bado hazitatumika kwenye malengo ya kuendeleza jamii yetu.
   
 13. K

  Kinyikani Member

  #13
  Dec 5, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapana maana yoyote kufanya Uchaguzi kwa hapa Tanzania NEC haitoruhusu kuwa na uchaguzi huru na waki NEC ipo kwa ajili ya CCM tu sasa yanini kufanya uchaguzi ni just kuwapa CCM mwanya wa kutesa watu tu.
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180

  Mtoto,

  Ikiwa leo hii Chama kilichoko madarakani hakitaki kutoa nafasi sawa hata kurekebisha Katiba ambayo itakuwa shirikishi, je kuna maana gani ya kuwa na uchaguzi na kupoteza fedha?

  Ikiwa wawakilishi wa Wananchi wamekaa katika nafasi zao miaka nenda rudi lakini Mtanzania hapigi hatua za maendeleo na haionekani kuwa kuna ulazima wa kumbadilisha Mwakilishi huyo ili kuleta maendeleo na si kubailisha sura tuu, je kuna maana gani ya kufanya uchaguzi?

  Ikiwa Serikali na Chama kilichoko madarakani, kimamua kuwa chenyewe ndio mwanzo na mwisho na yeyote atakayekikosoa Chama au Serikali ni msaliti, mhaini hata karibu kuwa gaidi, je kuna maana gani ya kufanya uchaguzi na kutumia pesa nyingi hizo eti kutimililza Katiba na Demokrasia ambayo inashikiliwa Kidikteta?
   
 15. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acheni fikra nyepesinyepesi kama hizi!!!!!!!!!!!!!!!!

  nani aliyewaroga kuamini kuwa uchaguzi ni kupiga kura?

  nani aliyeaaminisha kuwa uchaguzi una maana kama tu kuna uwezekano wa kupata rais mpya?

  uchaguzi n mchakato mrefu. mwisho wa uchaguzi uliopiyta ndio uliokuwa mwanzo wa uchaguzi ujao. ndio maana wansiasa wanapoamiwa "uchaguzi umekwisha " hwaelewe unawaambia nini!

  uchaguzi hutoa fursa za kupambanisha hja za maendeleo na kyapa nafasi majukwaani mwazo mbadala kwa maendeleo yetu. huwafanya wanasiasa wasilale wakijua wanaweza kuondoshwa. angalia bunge la sasa. angalia serikali ya sasa, licha ya kujua kuna uchaguzi, tunaambiwa kuna wabungw hawajawahi kuongea bungeni tangu 2005 hadi leo (mfano marehenmu ng'itu hadi mauti yanamkuta alikuwa hajawahi kusema wa la kuuliza chochote bungeni utadhani alikuwa wa "viti maalum" au wa "kuteuliwa kwa kazi maalum" kumbe wa jimbo la uchaguzi la ruangwa kule umasikini ulipoota mizizi!) sas fikiria bila uchaguzi wangesinzia nambna gani waha?

  mimi tayari nimeishatangaza zma ya kuwania ubunge kwenye jimbo la uchaguzi, tayari matumaini yanachipua, hadi hapa pekee, mamjaona faida ya kuandaa uchaguzi?

  gharama maana yake nini? kuna gharama kubwa zaidi ya kuwahakikishia afisadi nchi kwa iaka mingine mitano! bora uchaguzi japo hauondoi lakini unapunguza uhakika wa kukamata uamu wa nchi kwa baadhi ya afisadi.

  Mungu libariki jimbo ninalotaka kugombea, bariki na tanzania yote
   
 16. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yote uliyosema ni sahihi. Ni matatizo yaliyopo. Lakini narudia tena....kufuta uchaguzi ni kumnyima mwananchi haki yake ya msingi ya kuchagua uongozi wa jamii. Refer to my earlier post for further elaboration of this point.
  Kwa hiyo sasa...cha msingi ni kujadili mikakati ya kupambana na haya matatizo uliyoyaandika.
  Tatizo la wawakilishi.
  Je, Mwananchi wa kawaida anaelewa kazi ya mwakilishi wake? Na kama jibu ni hapana. Sisi kama waelewaji, tulitatuaje hili tatizo? Kumbuka, Tanzania haina upinzani. Hawa wanajiita wapinzani - ni li-lebal tu wamejipa. Sijaona upinzani usio na mikakati wazi juu ya policy ya chama tawala. Mpaka leo, sijasikia upinzani umetoa ripoti, au a feasible policy ya tatizo la umeme Tanzania. Sijaona upinzani umetoa a different policy kwenye swala la foreign investment. Upinzani hawajui kazi yao. Wao ni kuita watu mafisadi tu! Uliza pesa wanayo-pocket wao! Zitto akikaa kwenye vikao vya kamati ya Nishati, anapokea Tsh 200,000 kila siku. Muulize pesa anayopokea as Waziri kivuli wa sijui wizara gani inaenda wapi? Muulize million 40 atakayopokea 2010 itaenda wapi? nk, nk, nk. Ni ujinga/siasi tu zinavyoendelea. Anyway...lets return to our discussion. Kwa hiyo ni muhimu kwa mwananchi kutambua kazi za mwakilishi wake kwa kusudi la kuweza kumpima kama ni mfanyakazi kweli! Mwananchi yeyote asiyejua kazi ya mwakilishi ni MJINGA. Kuitwa mjinga sio tusi, bali ni kutojua kitu (ignorance). Kwa hyio ni lazima tuufute huu ujinga.

  Swala la Chama tawala kutotaka kutoa nafasi ya kubadilisha katiba, ni haki yake. Solution, andika Katiba mpya, sambaza kwa wananchi eleza tofauti yake na umuhimu wake, na wape option ya kuchagua wawakilishi watakao badilisha hiyo katiba. CCM haiwezi kubadilisha katiba kama imekaa kui-favour yenyewe. Kama unasubiri CCM ifanye hivyo...utasubiri mpaka kufa.

  "Adui wa taifa ni Umaskini, Maradhi na UJINGA" - JKN. Out of these three, the worst is UJINGA. Na ndo huo unaotumaliza hivi leo. Lakini kizuri ni kwamba, ujinga unafutika. Kwa hiyo, solution ni kupambana na huu ujinga kwa kusudi la kumwezesha mwananchi wa kawaida ku-make an informed choice katika UCHAGUZI. Je tutapambanaje na ujinga? That is the next question....
   
 17. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #17
  Dec 8, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kishoka,

  Maneno yako ni sawa na muziki mtamu masikinoni mwangu, tatizo ni kwamba, ni Watanzania wangapi wenye "ubavu" wa kukataa kushiriki kwenye uchaguzi huo mkuu wa 2010 utakaosheheni kila aina ya hila, ghilba na ufisadi?

  Nawashangaa Watanzania, hawakistuka jinsi "wenye nchi" walivyoiba kura kwa kutumia "sayansi na teke linalokujia"! Nashangaa sana! Inakuwaje, ati kwenye kituo kizima kura zote z'ende SISIEMU, hata yule kinara wa upinzani naye kura yake 'ende SISIEMU? Nashangaa sana! Yaani kituo kinatoa matokeo, SIEIEMU 500, UPINZANI 0! Duuu!

  Kama hawakuliona hili 2005, basi, 2010 hawataliona!

  HAKUNA DEMOKRASIA TANZANIA!

  Tuna "kiinimacho" cha "DOMOKRASIA". Kila mtu ajali ya kwake, ya Taifa ayaweka kando!

  Toba Yarabi! Tunusuruuuuu!


  ./Mwana wa Haki
   
 18. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pesa zote za uchaguzi ujao kutoka vyama vyote nchini na tume ya uchaguzi na zote ambazo zingetumika kufanya logistics.. police, UWT, etc

  Zitumike kujenga chuo kikuu cha matibabu ya binadamu (full equipped) kule kwetu sumbawanga..ili hospitali hiyo iwe ya kimataifa rais na mawaziri wanatibiwa hapo

  huo ungekuwa uamuzi wa kizalendo sanaaa kweli
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Dec 8, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280

  Asante kwa kusema hilo, umenena kijasiri

  swali viko wapi vyama vya upinzani kuhakikisha hili linatokea SIO NCHI YA CCM HII!!!!!!!!!

  VYAMA VYA UPINZANI VILITAKIWA KUPIGANIA HILI KWANZA HATA KUKATAA UCHAGUZI, KATIBA IKIBADILISHWA WANA UHAKIKA WA KUWA SEHEMU YA SERIKALI

  LAKINI WAPI!!! ANGALIA VYAMA VYETU MASKINI...VINAWAZA KUMSIMAMISHA MGOMBEA URAIS!!! SOMETHING WRONG SOMEWHERE!
   
 20. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mmeanza kuandaa akili za watu ili mkishindwa na huo ubunge msingizie mmezulumiwa.

  Mmeanza wakati mwenendo wa vyama vya upinzani mnauona wenyewe.Haya
   
Loading...