Hakuna haja ya kuwa na alama za wenda kwa miguu Tanzania

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wana JF, mara nyingi nimekuwa nikishuhudia jinsi madereva wetu wasivyofuata alama za wenda kwa miguu. Siku moja nilishuhudia kiwete mmoja akivuka kwenye alama za wenda kwa miguu halafu gari lililokuwa likipita likawa linapiga honi na lilikuwa katika speed kali.

Siku nyingine niliona mtoto akipita na gari lilikuwa likija speed na dereva hakupunguza mwendo na badala yake akaanza kupiga honi na kumshutua huyo mtoto akababaika nusura amgonge.

Siku nyingine ilikuwa mama mzee alitaka kuvuka na gari lilikuwa likipita kwa speed. Nilichofanya nilimshika huyo mama mkono na kumvuta asipite na hilo gari likapita speed. Nisingefanya hivyo, ni wazi angegongwa. Hivi kwenye mafunzo ya udereva hawa madereva huwa wanafundishwa nini?

Sehemu zingine unamkuta polisi wa trafiki amesimama kwenye alama za wenda kwa miguu na kuzuia magari yasimame na kama hayupo, hayawezi kusimama. Hivi tatizo ni nini? Ni madereva wachache sana ambao wanaheshimu na wakifika sehemu ya wenda kwa miguu na kama kuna watu wanasubiri magari yasimame ili wapite, wanasimama na kuwaruhusu wapite.

Madereva wengine ni kama wenda wazimu, hawajali. Hivi kutakuja siku labda za huko usoni tutaheshimu alama za barabarani au ndiyo hiyo imepita? Binafsi sioni sababu ya kuwa na alama ambazo hazifuatwi au zinafuatwa tu pale dereva anapotaka kupakia wanaovuka barabara!
 
- Hatuna Barabara (Vichochoro vinageuzwa njia za Magari!)
- Hatuna Madereva (Leseni unaletewa Nyumbani)!
- Hatuna Sheria za Barabarani (Kama zipo who cares?)
- Asilimia 90 ya Magari Mabofu

Kila Mtu ni kivyake tu - Life goes On - Obladi Oblada
 
Back
Top Bottom