Hakuna haja ya kuchukia waajiri, mwisho wa maovu yote ni 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna haja ya kuchukia waajiri, mwisho wa maovu yote ni 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjomba wa taifa, Aug 3, 2012.

 1. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Licha ya kuwepo vilio vingi vya kudai masilahi ya wafanyakazi kutoka kila kona ya nchi bado serikali imezidi kunyesha jeuri ya kuziba masikio. Hili ndilo tatizo la nchi kuongozwa kwa kauli ya mtu mmoja licha ya kuwa na mihimili mitatu iliyopaswa kujitegemea.

  Majibu haya ya dhihaka na jeuri yanayotolewa na kiongozi mkuu wa nchi mathalan lile la sakata la Madaktari, Walimu, kupigwa kwa Dr. Ulimboka na hata hili la mafao ya wafanyakazi ambalo bado ni kizungumkuti yanasababishwa na kiongozi huyu kujua kuwa hii ni awamu yake ya mwisho na hahitaji tena kupanda jukwaani kunyenyekea wapiga kura. Haya ndiyo malipo ya viongozi wanaoingia madarakani kwa sura ya kondoo.

  Hata hivyo maamuzi haya ya mkuu wa nchi yanakiweka rehani chama chake ya kupata ridhaa ya kuongoza nchi hii awamu ijayo. Na kitu cha kushangaza sijui kwanini wana-CCM wengine wamekuwa wakichekea maamuzi haya ambayo yatakuja kuwagharimu wenyewe kwani mheshimiwa huyu atakuwa Msoga, ama Serengeti akipunga upepo safi huku akila pensheni na mali zote alizozichuma. Ikumbukwe kuwa wananchi wakichukia chama, katika uchaguzi hata mgombea wake asimamishwe na jiwe bado jiwe litapigiwa kura. Ushahidi mdogo tumeuona katika uchaguzi mkuu uliopita, wagombea wengi waliokuwa na sifa walitoswa na wananchi kisa wanatoka chama kisichokubalika.

  Hivyo basi, hakuna haja ya kulumbana na Serikali, kwani kama tumeweza kuvumilia machungu kwa miaka 60 ya Uhuru kwanini tushindwe kuvumilia miaka hii mitatu iliyobaki. Wanyonge tayari wanaomtaji kwa kuwa walimu hawa wanaonyanyaswa leo hii ndio wasimamizi wa zoezi la kupiga kura vituoni na ndio wanaowalea wanafunzi mashuleni ambao wengi wao watakuwa na haki ya kupiga kura uchaguzi ujao.
   
Loading...