Hakuna Fao la Kujitoa NSSF duniani kote - Ramadhan Dau

Mimi nimeshangazwa sana na hatua ya serikali kuruhusu mfuko mmoja kutoa fao la kujitoa.Naona labda serikali imefanya hivyo kwa kujua kwamba imeshafilisi hii mifuko mingine sasa inaona labda watu wakitaka kuchukua pesa zao itakuwa noma.Hii serikali hamna jambo lolote zuri inaweza kufanya,kwani haina uchungu na wananchi wake,wako kimaslahi zaidi.
 
Nimemsikiliza kwakweli nimepatwa na hasira sana, mbaya zaidi anaongea akijichekesha chekesha.
Anadai utaratibu unatakakiwa ukifukuzwa kazi utafute kazi pengine uendelee kuchangia!

hizo kazi za kujuana kama wewe huna undungu na Riz one hupati kazi
tena asitupandishe hasira
Kwanini hawakufanya hivi mapema waje wabadilishe sasa tena ghfla bila kujadiliana na wahusika wanaokuwa affected na hili jambo??
 
Hamna kitu kibaya kujiona wewe ni bora kuliko binadamu wengine na mawazo mazuri zaidi ya binadamu wengine wote waliowahi kuishi katika ulimwengu huu. Kauli ya huyu Mkurugenzi inadhihirisha kuwa yeye ni bora zaidi na mawazo yake ni bora zaidi ya wengine. Issue inayohusu maslahi ya watu (individuals) lazima iamuliwa na watu (individuals) kwa umoja wao na ndo maana issue kama ya katiba ya Jamhuri tumeruhusiwa kila mtu kutoa maoni yake mbali na kwamba wapo wanasheria waliobobea kwenye mambo ya katiba na sheria lakini hawajaachiwa wao watutungie katiba. Na katika suara zima la Fao la kujitoa ni juu ya wahusika (contributors/members) wa mifuko kuamua namna inavyofaa kuchukua fao lao pindi wanapokuwa hawana kazi. Kauli kama ya Ramadhan ni kauli ya kipuuzi ya kuingilia uhuru wa mtu binafsi kwa maslahi ya kikundi kidogo katika jamii, jambo hili halikubaliki!

Haingii akilini mtu mwenye PHD akasema eti ukiacha/kuachishwa/mkataba kuisha utafute kazi sehemu nyingine uendelee kuchangia. Huyu mtu nadiriki kusema si mtanzania na kama ni mtanzania basi hayajui maisha ya watanzania na atakuwa msaliti mkubwa katika taifa hili tajiri la watu masikini, simuhukumu kwa lolote kwa kuwa nami si wa haki aliye na haki atamhukumu. Ramadhan hata kama utafumba macho na kuziba masikio bado nafsi yako inakuhukumu kwa maneno ya kejeli na ya dharau kwa watu wasio na hatia. Nani asiyejua kuwa pesa za mifuko ya jamii serikali/ mifuko yenyewe mmeziwekeza kwenye miradi ya muda mrefu kiasi kwamba inaelekea kufilisika na hiki ndicho chanzo cha kutunga sheria ya fao la kutojitoa ambayo nayo imepitishwa bila kujadiliwa bungeni kwenye schedule of amendements? Nani asiyejua ukweli huu? Leo hii unakurupuka eti duniani kote hakuna fao la kujitoa? I doubt you might be mentally insane or forced by your lower eagle!

Ramadhan na wote wenye mitazamo sawa na Ramadhani mkumbuke vyeo mlivyonavyo ni dhamana ya muda tu ambapo sisi ndio tunawalipa mishara, ipo siku we will bring you down on our floor na ndipo nanyi mtapata kujua kuwa ubinadamu ni zaidi ya cheo na mali zisizokuwa za haki. Tutapigania haki zetu si kwa upanga au mabavu, vitisho na sheria kandamizi kama mnavyofanya bali kwa kumtumainia yule aliye wa haki naye atatupigania. Hakika Ramadhani na watu wenye mtazamo kama wako kizazi chenu hakitapita bila kushuudia adhabu ya unyanyasaji na dhuluma mlizowatendea watanzania katika taifa lao!
 
Huyu anaakili ya kuchoma makanisa tu. Dau na Shekhe Ponda akili zao zinafanana.
 
wewe uko wapi? wangapi wanaozeeka siku hizi! hata CCM wana motto yao CHUKUA CHAKO MAPEMA kwani hawaajijui watakuwa wapi in the next few years to come.....

Kitakusaidia nini? wakati bado una nguvu zako na unaweza kufanya kazi. Kumbuka hizo fedha zinawekwa pale utapokuwa umeishiwa na nguvu na madhara ya kupewa mapema yameonekana ndio maana kwa upande wangu naona ni bora inavyofanywa sasa kwani ukiwa hauna nguvu huna haja ya kuwa Matonya.
 
Swali la kizushi, hivi sisi tunaishi kwa ajili yetu au kwajili ya watu wengine?? Maana kila kukiwa na upuuzi fulani lazima wafanye comparison na wengine......kwanini sie ndio tuwafanye wao waige toka kwetu?? Pia kama ni kuangalia wengine wanafanyaje, basi linapokuja suala la RUSHWA basi na wenyewe wajiuzulu ili kuendana na huo mfumo wa kimataifa kama wengine, mbona kwenye ufisadi na wizi hua hawajilinganishi na nchi nyingine ambapo viongozi husika hujiuzulu pale wanapokumbwa na kashfa????
 
Jamani hivi mtu katoka mgodini(mwanafunzi), alikuwa anakatwa nssf naye asubiri miaka 60?

Mgodini wanafukuza na kuajiri kila siku,hao wachimbaji waliofukuzwa watapata lini mafao yao?

Je makampuni ya madini yana uwezekano wa kuendesha mgodi kwa miaka tajwa na nssf?

Kuna viongozi wanakuwa hawajui mazingira halisi ya wafanyakazi,na wakiendelea namsimamo wao ya RSA yatatokea TZ.

Nimesikiliza kutoka magazetini ya Clouds radio power breakfast (leo) mswada umewasilishwa serikalini na mwanasheria mkuu na unaonyesha fao la kujitoa limeruhusiwa PPF na mifuko mingine imeachwa solemba ila watu wa migodini kupitia migodini imeonekana wanapata fao la kujitoa kupitia PPF kwa maelekezo kutoka juu japokuwa SSRA walizuia (it seem like wanawaziba mdomo maana wao wapo wengi na ni rahisi kuji-mobilize na kuchukua hatuwa kutokana na nature ya kazi yao ya kufanya kazi kwa kukaa eneo moja la kazi yaani camp, kasheshe kwa staff wengine sijui itakuaje maana ili wajiunge pamoja kudai haki yao inahitaji muda)

My take: huwa sipendi kiongozi wa taasisi au serikali anapotetea hoja yake na kutumia kigezo cha kulinganisha na nchi zingine kiasi kwamba huwa najiuliza haiwezekani na sie tukaanzisha chetu nchi zingine zikafuata. Mfano mwingine unakuta mwanasiasa akiulizwa swali kuhusu kiwango cha ukosefu wa ajira, unakuta ili aonekane yupo sawa atajibu simple kwa kusema hata nchi jirani tumeshinda kwa hilo hivyo tunakwenda vizuri wanasahau kwamba kila nchi ina mkakati wake hivyo kama wamefanya vibaya kwenye sekta flani sio justification ya sie kujisifu.

KABLA YA KUFUTA FAO LA KUJITOA KINACHOTAKIWA KUANGALIA HIZO NCHI DUNIANI AMBAZO HAZINA FAO LA KUJITOA WANAFANYAJE MAANA UKUTE WENZETU WIZARA ZINAZOHUSIKA NA AJIRA ZINAJITAHIDI KUSIMAMIA MIKATABA YA WANANCHI WAKE KWA KUWABANA WAAJIRI na mwisho wa siku hakuna kuachishwa hovyo kazi kama hapa kwetu Tz
 
Hamna kitu kibaya kujiona wewe ni bora kuliko binadamu wengine na mawazo mazuri zaidi ya binadamu wengine wote waliowahi kuishi katika ulimwengu huu. Kauli ya huyu Mkurugenzi inadhihirisha kuwa yeye ni bora zaidi na mawazo yake ni bora zaidi ya wengine. Issue inayohusu maslahi ya watu (individuals) lazima iamuliwa na watu (individuals) kwa umoja wao na ndo maana issue kama ya katiba ya Jamhuri tumeruhusiwa kila mtu kutoa maoni yake mbali na kwamba wapo wanasheria waliobobea kwenye mambo ya katiba na sheria lakini hawajaachiwa wao watutungie katiba. Na katika suara zima la Fao la kujitoa ni juu ya wahusika (contributors/members) wa mifuko kuamua namna inavyofaa kuchukua fao lao pindi wanapokuwa hawana kazi. Kauli kama ya Ramadhan ni kauli ya kipuuzi ya kuingilia uhuru wa mtu binafsi kwa maslahi ya kikundi kidogo katika jamii, jambo hili halikubaliki!

Haingii akilini mtu mwenye PHD akasema eti ukiacha/kuachishwa/mkataba kuisha utafute kazi sehemu nyingine uendelee kuchangia. Huyu mtu nadiriki kusema si mtanzania na kama ni mtanzania basi hayajui maisha ya watanzania na atakuwa msaliti mkubwa katika taifa hili tajiri la watu masikini, simuhukumu kwa lolote kwa kuwa nami si wa haki aliye na haki atamhukumu. Ramadhan hata kama utafumba macho na kuziba masikio bado nafsi yako inakuhukumu kwa maneno ya kejeli na ya dharau kwa watu wasio na hatia. Nani asiyejua kuwa pesa za mifuko ya jamii serikali/ mifuko yenyewe mmeziwekeza kwenye miradi ya muda mrefu kiasi kwamba inaelekea kufilisika na hiki ndicho chanzo cha kutunga sheria ya fao la kutojitoa ambayo nayo imepitishwa bila kujadiliwa bungeni kwenye schedule of amendements? Nani asiyejua ukweli huu? Leo hii unakurupuka eti duniani kote hakuna fao la kujitoa? I doubt you might be mentally insane or forced by your lower eagle!

Ramadhan na wote wenye mitazamo sawa na Ramadhani mkumbuke vyeo mlivyonavyo ni dhamana ya muda tu ambapo sisi ndio tunawalipa mishara, ipo siku we will bring you down on our floor na ndipo nanyi mtapata kujua kuwa ubinadamu ni zaidi ya cheo na mali zisizokuwa za haki. Tutapigania haki zetu si kwa upanga au mabavu, vitisho na sheria kandamizi kama mnavyofanya bali kwa kumtumainia yule aliye wa haki naye atatupigania. Hakika Ramadhani na watu wenye mtazamo kama wako kizazi chenu hakitapita bila kushuudia adhabu ya unyanyasaji na dhuluma mlizowatendea watanzania katika taifa lao!

Mkuu umenena....
 
Nimemsikiliza huyu mkurugenzi akiwa anaongea. Yaani ilibaki kidogo nipate hasara ya ka TV nilikokuwa nakaangalia kwa jirani. Kaonyesha wazi kuwa yeye sio mbunifu. Anasema eti hata wapi sijui huko hakuna fao la kujitoa. Mwambieni siku zote mambo mazuri ndio ya kuigwa. Wanatakiwa hao Ambao hawana hili fao awaalike waje waone tumewezaje sisi kuwa nalo kwa miaka yote na mifuko ikawa bado imara. Kwa akili yake kama ulaya au Amerika hawafanyi jambo fulani sisi hatutakiwi kulifanya?
 
Swali la kizushi, hivi sisi tunaishi kwa ajili yetu au kwajili ya watu wengine?? Maana kila kukiwa na upuuzi fulani lazima wafanye comparison na wengine......kwanini sie ndio tuwafanye wao waige toka kwetu?? Pia kama ni kuangalia wengine wanafanyaje, basi linapokuja suala la RUSHWA basi na wenyewe wajiuzulu ili kuendana na huo mfumo wa kimataifa kama wengine, mbona kwenye ufisadi na wizi hua hawajilinganishi na nchi nyingine ambapo viongozi husika hujiuzulu pale wanapokumbwa na kashfa????

Ulikuwa unawaza kama mie maana sie tunajifanya wazee wa ku-copy na paste ila hapo nilipo-bold umenifurahisha sana kwani ni ngumu kujiuzulu hawa watu (walitakiwa na wao waseme nchi zote mambo yanapokwenda vibaya ktk sekta flani inabidi kiongozi husika ajiuzuru)
 
Pole sana mkuu!tuko wengi wahanga wa hawa watu ambao binafsi nitasema 'the narrow minded'!Watu wasiokuwa na machungu na wananchi wao!Jitu linajiona km Mungu mdogo!cha muhimu tushikamane na ikiwezekana waburuzwe kortini!Zile ni hela zetu na si zao.
 
Kaniboa kweli huyu jamaa. Mwambieni imefika muda hao wa. Ulaya na amerika nao waje wajifunze huku. Asikariri kuwa vitu vyote vizuri lazima vitoke nje. Yukoje huyu?
 
Wanaogopa labda tutanza na Kaka Alfani
Ulikuwa unawaza kama mie maana sie tunajifanya wazee wa ku-copy na paste ila hapo nilipo-bold umenifurahisha sana kwani ni ngumu kujiuzulu hawa watu (walitakiwa na wao waseme nchi zote mambo yanapokwenda vibaya ktk sekta flani inabidi kiongozi husika ajiuzuru)
 
Pamoja na udokita wake "amezoea kukopi na kupaste" na anawaza kuwa JAMBO ZURI HALIWEZI KUANZIA TZ wala mambo au taratibu zilizopo haziwezi kurekebishwa na Tanzania.
Kweli "uchungu wa mwana aujua mzazi".....

Ndio shida yetu wabongo yaani kila kitu kitoke kwao kwa nini wao wasiige kutoka kwetu? akili finyu sana Very stupid indeed.
 
Mkizeeka mtapokuwa hamna mafao mnategemea kuomba omba? mnafanyiwa mambo mazuri ya kuwekewa akiba unapozihitaji kiukweli nyie mnalalama.
Zomba hebu kua na weledi some times? Kwa nini serikali iwaonee huruma wafanyakazi ambao si zaidi ya m3 wakati kuna watu zaidi ya 15m ambao hawapo kwenye mfumo wa pension? yaani huruma inakuja kwetu tu?
 
Kauli ya Dau ni ya Kijinga sjapata kusikia kwa mtu mwenye Level ya Elimu kama yake! Huko Duniani anakosema wamekubali Ushoga na mdoa za jinsia Moja zinaendelea anataka nasi tuige? Isitoshe tujiulize hivi wafanyakazi wapo wangapi kati ya population ya tanzania amabao wanategemewa kufanya kazi? mbona wapo wengi ambao hawachangii lakini mambo yao yanakwenda? Hivi Shelf Life ya Mtanzania ni miaka 60?

Wapendwa si issue ya watu wamigodini tu,wafanyakazi wengine wanatumia mafao hayo kujitoa katika kuajiriwa na kujiajiri baada ya muda fulani,pia kwa mfano kuna mfanyakazi amabaye ni Seasonal workers ambao baada ya msimu kazi imekwisha na wakati fulani hana uhakika kama seasonal nyingine atapata kazi.

Pia issue ya eti akiacha kazi au kufukuzwa atafute kazi nyingine ni hopeless kwa system ya chama hiki ambacho kinatuongoza, ambapo rate ya Unemployment people inaongezeka kila siku!

Patachimbika nyie subirini!!
 
Mkurugenzi wa NSSF Dr Ramadhan Dau amesema Fao la kujitoa limeondolewa ili kuendana na mfumo wa kimataifa kwani duniani kote hakuna Fao la kujitoa.

Amesema hata Zanzibar na Kenya hakuna kitu kama hicho.

Mkurugenzi huyo alitoa tamko hilo alipokuwa akihojiwa na Kamati ya bunge ya mashirika ya umma inayoongozwa na Zitto Kabwe.

Source: ITV Habari

Sishangai sana,watu na degree zao za nguo za ndani!
 
Back
Top Bottom