Pure_sapiens
JF-Expert Member
- Dec 25, 2016
- 2,197
- 2,024
Habari wana GT. Natumaini sote ni wazima wa afya.
Leo naileta mada hii jukwaani mara baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu Uwepo wa Mungu lakini pia kuhusu imani na dini.Nilichogundua Mungu hana dini wala imani ya aina yoyote.Ila hizi imani na dini ni matokeo ya binadamu katika kutafuta ustawi wa jamii zao hapo kale.
Uwepo wa Mungu sina shaka nao kabisa nilishathibitisha hilo before na niliweka thread hapa, kupitia thread ile iliondoa utata kwa kiasi kikubwa kuhusu uwepo wa Mungu katika universe na pia kuweka hitimisho kuwa Mungu yupo.Mungu yupo katika kila jamii mbalimbali hapa duniani hapo kale hata sasa hakuna jamii/kabila/taifa ambalo halikuwa na Mungu fulani.
Plutarch myunani aliyekufa mwaka 120b.k na mwandishi wa habari za maisha ya wayunani na warumi. Katika kitabu cha kinachoitwa " Parallel lives of illustrious Greek and Romans"(maisha sambamba ya wayunani na warumi mashuhuri), alisema kuna miji isiyo na kuta, wala vitabu, isiyo na mfalme, wala nyumba, wala hazina, wala mahali pa kuchezea michezo, lakini mji usiyo na hekalu wala Mungu fulani hakuna mtu aliyepata kuuona mji wa namna hiyo, na hautauna kamwe"mwisho wa kunukuu.Kumcha Mungu ni sehemu asili ya mwanadamu.Hapa haijalishi ni Mungu wa namna gani....
Ukiisoma historia ya Ibrahimu(baba wa imani) ambaye ndiye chanzo cha hizi dini/imani za leo utagunduwa hakuwa na dini au imani ya dini. Ibrahimu aliamini Mungu tu na si tofauti na hapo.Dini zilianza miaka mingi baadae sana ili kustawisha jamii za watu na kutunza mila na tamaduni zao.
Hata jamii za kiafrika kabla ya ujio wa wakoloni walikuwa na Muingu yao ambayo waliabudu na kuitukuza.
Hizi imani/dini zinamwelezea Mungu kwa upotoshaji mkubwa hadi inafika hatua baadhi wa watu wanafikia kuhoji uwepo wake.
Sifa na tabia anazopakwa Mungu katika dini hizi za watu si za kweli hivyo zinaleta contradiction kuhusu uwepo wa Mungu.
Mungu ameumba ulimwengu na vilivyomo basi, alafu akawapa mamlaka viumbe wake waishi watakavyo.We jaribu kujiuliza kama Mungu angetaka binadamu tuwe na dini/imani ili kumjuwa yeye kwanini asingeweka moja tu kwa viumbe wake wote? Kwanini hadi asuburi binadamu wazue dini zao ambazo zinakinzana kumwelezea Mungu mmoja?
Hivyo hajaleta dini wala imani pia Mungu hajaumba sheteni.MUNGU YUPO ILA HANA DINI WALA IMANI.
Nawasilisha...