Hakuna Chama cha Upinzani kitaongoza Serikali Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna Chama cha Upinzani kitaongoza Serikali Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nonda, Dec 13, 2010.

 1. N

  Nonda JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Si CUF, CHADEMA , NCCR au Chengine chochote. Sasa endelezeni kuhujumiana na longolongo !

  Mwana JF na wale wanatupia jicho JF,

  Angalia na sikiliza Mkapa segment..kuanzia dakika ya 2:46 mpaka 3:35

  Jiridhishe kwa kuangalia hii video, kwa hisani kubwa ya Mzee Mwanakijiji, Uone kuwa CCM hawana nia ya Kuachia madaraka hata pale wanaposhindwa au watakaposhindwa kupitia kisandukuni.

  Watalazimisha wawe washindi! Kivipi?

  Wao ni wamiliki wa Vyombo vya dola na Tume ya uchaguzi in the real sense kwa vile ndio wanaoongoza serikali kwa sasa, ingawaje vyombo hivi vinapaswa viwe vyombo vya Taifa, Umma.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Tutawaondoa kwa damu zetu na zao kwa faida ya wana na wajukuu wetu. Usiwe na shaka.
   
 3. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  kila chenye mwanzo kina mwisho, gavrilo principe mwanafunzi, mserbia wa sarajevo alimpiga risasi na kumuua franciss frednand dicteta binamu wa aliekua kiongozi wa ujerumani, na hatimae kuutokemeza ubabe wa watu hao. naamini kabisa hakuna lisilo wezekana. la muhimu tujiandae na tuwe tayari hata kufa kwaajili ya tanganyika yetu.

  ESTAMOS PREPARANDO PARA MORIR EN DEFENDIENDO NUESTRO PAIS,by FIDEL CASTRO,maana tunajianda kwa ajili ya kufa huku tukiilinda nchi yetu.
  nawasilisha
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Dec 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Mbona hiyo inajulikana, unataka kusema nini? si huwa mnaimba humu kuwa kuna chama mbadala, mbona naona unaanza kupata wasiwasi.

  Title yako ni kweli kabisa, hawatapata kuongoza nchi si kwasababu ya CCM! ni kwa sababu ziyo wapinzani halisi!
   
 5. K

  Kipre tchetche JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2010
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio maana tunahimiza tupate katiba
  mpya ..Hilo ndilo suluhisho na siasa za
  kisanii zitakuwa mwisho.
   
 6. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mapambano ndiyo yameanza tena kwa ustarabu sana.

  kwanza katiba ibadilishwe baada ya hilo tutajua cha kufanya...
   
 7. N

  Nyota Njema Senior Member

  #7
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ndugu ya Waberoya,

  Si kweli usemalo, ila nitakubaliana nawe kama lengo lako ni kutoa changamoto ya kudumisha maelewano kwenye vyama vyetu. Watanzania wengi tunapenda sana kukaa pembeni na kubeza tukifikiri kuwa kuna wajomba kutoka kulee... watakaokuja kutuwekea mambo yetu vizuri. Kama kweli lengo lako ni kuona nchi inapata mabadiliko ya kuiwezesha kuendelea, basi achana na haya mambo ya siasa nyepesi ili uuone ukweli na changamoto zake.

  Ni kweli kuwa baadhi ya vyama sasa muda umevidhihilisha kuwa vinapoteza mwelekeo wake na sasa vimebaki kuwa vyama maslahi kama ulivyo uongozi wa CCM. Tofauti na vyama hivi, CHADEMA sasa imejidhihilisha kwa watanzania kuwa ni chama mbadala na kinachovutia wote wanaotaka kuisaidia nchi. Kinachoendelea ndani ya CHADEMA si kuvunjika kwa chama bali chama kinaanza kusafisha udhaifu uliokuwepo ili kiweze kuwa na nguvu za kutosha kukabiliana na mikiki ya kujenga taifa bora, ambalo lilishaanza kupoteza mwelekeo kutokana na uongozi maslahi uliopo! Fedha, matumizi ya nguvu za dola pamoja na mtandao wa kifisadi walionao CCM hautaizuia nchi kupata ukombozi; hata Nyerere aliweza kuichukua nchi mikononi mwa wakoloni ilihali walikuwa na kila kitu walichonacho CCM leo hii. Watanzania tutakaposema inatosha, huo ndio utakuwa mwisho wao. Mchakato umeanza, kila mtanzania mwenye nia njema na kizazi chetu kijacho aunge mkono harakati hizi!
   
 8. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2010
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  sasa mbona ccm imeanza kucountdown?au itakua nchi isiyo na chama?sababu sasa hivi hiyo ccm inapumulia pua moja..!!
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mmeshakosa cha kuandika sasa!
   
 10. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mtu alieanza hii hoja is short sighted & narrow minded. Ila ajaanzasha kwa nia yakueleza ukweli sabab hataishi milele nakuona sisiem ikitawala bali anaogopa mabadiliko. Anachofanya hapa nikuwachokoza wapenda mabadiliko. Siwez mlaum sabab kwakusema haya, anaonyesha anafaidika na mfumo mbovu iliyopo na angependa uendelee milele. Hongera ila kumbuka, there's no record of any goverment that has a guarantee of ruling forever.
   
 11. P

  Paul S.S Verified User

  #11
  Dec 13, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kwanini wasitawale bana,
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Dec 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280

  Umenena vizuri sana ndugu yangu

  Hivi Demokrasia inaanzia wapi ndani ya chama au nje ya chama?

  sijabisha kuwa CDM ni mbadala wa ccm , ila NI MBADALA KATIKA YAPI? replacement? naona CDM kuna yaleyale ya CCM,nadhani ndio tafsiri sahihi ya mbadala.

  CDM kuna majungu, Slaa wenu ni mtu wa visasi na ana inferiority complex kiasi cha kuwaogopa watoto wadogo, Mbowe unaambiwa Mbabe kwani muasisi wa chama ni Mkwe wake! mnaambiwa viti maalumu bungeni mmejaza girlfriends, nyumba ndogo na ndugu.

  Same party tunaona mnavyobomona kwenye vyombo vyenu wenyewe vya habari, mkitumaini mtasimama na kujengeka?

  Is there anyone out there who think something good may come from these sop called oppositions and CDM included? common, you know how much they make?? is there any opposition leaders recently who have challenged government at a state that they can jail him?

  Nimabie kiongozi gani kati ya hawa mwenye uwezo wa kuongoza maandamano na kuweza kulala jela akikutetea wewe? au unafikiri mabadiliko yatakuja kwa ballot box? si umeona CCM wanavyofanya?

  au unataka kujipa matumaini ya comparison ya wabunge 26 na zaidi ya mia mbili?? lets speak the truth, CDM still have that opportunity to be a dream party for every Tanzania, they can start now, not with this leadership, not with these people that I know fully! Tuseme ukweli, unaweza kutukana we need revolution not evolution. CDM is exercising evolution which if you know you wouldnt be excited with it, the change will come 100 yrs from now!!

  Hivi una akili timamu wewe!!!! uko dunia gani??? Zenj wamelia miaka mingapi kuhusu faulo za CCM , wakati CDM inaingia kwenye uchaguzi walijua kuwa katiba mbovu? walijua kuwa NEC mbovu? YES walijua , what made them to participate in the election and cry later in the very basic thing that they were supposed to fight for? we need fair ground in elections opposition needed to prepare that! they didnt purposefully NA LEO UNASEMA CDM ndio wapinzani halisi utaamka lini ww unaibiwa?? unawapa watu kula yao mchana kweupe, nilisikia wanataka katiba mpya na NEC wamefikia wapi? wait for next 50yrs you will hear the same thing.

  tuache kudanganyana! watu tunaowajua truel leaders wamo ila wameminywa unataka nitaje majina yao??
  Kuna watu mnahitaji maombi kwa Gwajima, japo sio misukule

  Ebu sema, tumesema kuhusu akina RA na EL mara ngapi, ni nani wa kuwashtaki hawa watu? nenda nje ukaone vyama vya upinzani wanafanya nini na in politics this is very cheap campaigning!!! waambie kama wana mpango huo kama sio sema na wewe ukajiona unasiaidwa kumbe wanasema tu, wanasema tu, wanasema tu, na wewe probably unasikia tu unasikia tu

  Let think logically jamani!
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Ichukue changamoto hiyo na uiwakilishe kwa viongozi wa chama chako. Nakushukuru kwa mchango wako ila inaonekana hukufahamu ujumbe. Isome tene,na tena.
   
 14. N

  Nonda JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280

  Mkuu,
  Kama umemsikia kiongozi wako sawa, hakuna siri tena na wanazungumza kwa jeuri. Hakuna marefu yasio.........
  Itafika ......
  Yameshatokea katika nchi nyengine.
  Ni vizuri kuanza kutumia bongo ,ushawishi badala ya jeuri,kejeli na maguvu.


  kwa kila advantage ambayo kijani na manjano mmekuwa nayo kwa miaka yote hiyo,mnaipeleka wapi nchi hii?

  La msingi wafikishie ujumbe,wasome alama ya wakati. Sote tunaitakia mema nchi yetu ila kuna ukomo wa subira.
   
 15. N

  Nonda JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  CCM kama CCM kuna dalili hizo
  Lakini vyombo vya Umma,vyombo vya Taifa ambavyo vinatakiwa visimamie ustawi wa Taifa vinafanya kazi kama matawi ya CCM. Tatizo liko hapo tu.
  Lakini si hilo tu. Vyama vya upinzani haviko serious, vinahujumiana,pia vinajuwa kuwa Tume ya uchaguzi si huru, katiba
  haikidhi mfumo wa vyama vingi, na bado wanaingia katika uchaguzi.Vinalala usingizi wa pono, vinaamka baada ya kufungwa goli.

  narudia hili hakuna chama cha upinzani kinachoweza "kuishinda" pekee katika mazingira haya.
  Ni lazima viunganishe nguvu zao, vishirikiane, si lazima kuungana!
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  alikuwepo kamanda mmoja aliyeitwa Saddam Hussein al-tikrit, aliyekuwa akiiongoza nchi yenye utajiri wa Mafuta huku akiwa na kebehi na nyodo na ukatili dhidi ya Raia wa nchi yake na mataifa ya nje.


  Aliongoza nchi akisaidiwa na marafiki zake, binamu zake, ndugu, wanawe na watu wake wa karibu ambao aliwaamini ktk maisha yake.


  Alikuwa na utamaduni wa siku maalum ambayo huwa anaamka kisha anapiga Gobole lake kuelekea upande ilipo Marekani.


  Alikuwa na utamaduni yeye pamoja na waandamizi wake kuogelea na kuvuka mto mmoja ulioko nchini Iraq huku akifurahia maisha.


  Alikuwa ni mbishi, mwenye siraha kali za kivita.
  Alikuwa na jeshi na serikali yenye nguvu kiasi hata kufikia kuwatisha majirani bila hata kuwafokea.


  Aliweka watu wake ktk kila sekta muhimu.
  alikuwa na swahiba wake aliyeitwa Awad al-Bandel ambaye alikuwa ni jaji mkuu na alitumia cheo chake kuwahukumu kunyongwa au vifungo vya maisha watu woote watakaokwenda kinyume na matakwa ya Saddam.


  Lakini siku yake ilipofika Sheikh Saddam alikutwa ''NDANI YA DIMBA'' akiwa kachoka, dhoofu, na akionekana ni mwenye shida tele.


  Na tamati yake ilipofika Sheikh Saddam alinyongwa huku watu wakiwa wanamcheka na kumkebehi....


  So kila lenye mwanzo lina mwisho.
  Mateso yakizidi basi wokovu unakaribia
   
 17. f

  fredqbcc Member

  #17
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba tusichanganye mambo na kuwafanya wengine wasielewe vizuri mihimili na maana ya vyama vya siasa. Kiingereza au kizungu kiko so precise katika kueleza vyama vya siasa zaidi ya kimoja katika nchi moja vyaitwa opposition parties na sio tafsiri ya fitina muipelekayo kwa watanzania na kueleza kuwa Vyama vya SIASA tofauti na CCM ni vya Upinzani. Muogopeni MUNGU waambieni watu ukweli.

  Hivi Vyama vingine ni vya ushindani ambavyo vinataka kuja na alternative strategy ya kuwatoa Watanzania ambapo wamechelewa kushirikishana katika kuwandeleza Watanzania ili kuwapa maisha ambayo ni reliable with minimal or deleted hasles za wachache kuhodhi human resources, capital resources na kujifanya wao ni wateule na wamechaguliwa na Watanzania Wote Kidemokrasia .

  HAPA DAWA NI. La KUIREKABISHA KATIBA IENDANE NA MATAKWA YA WATANZANIA NA SIO CCM mujione mwa jua na kuweza kwa sababu mna state apparatus zote lakini swali lipo na ni rahisi "muuwe huyo kunguni kwenye kitanda chako atakumaliza na ukadhani nyumbani kwako kuna WACHAWI".

  CCM hawajui na kuona madhara ya msemo huu "Who will be controlling those who control" take care of the PEOPLE'S POWER one day utapata TAABU. HIVI hamjifunzi kung'atuka msemo wa Baba wa TAIFA Julius, alikuwa falsafa wa wakati hata katika dogo la kumbeba MREMA LYATONGA alisema acheni abebwe ninyi hamtaki kuwasikiliza Wenzenu.CCM mtanikumbuka ushauri wa BURE na kuanzia leo sitaki kuona mnasema vyama vingine ni vya UPINZANI jee hamnalo BARAZA la KISWAHILI katika SERIKALI YENU?.DHAMBIIIIIIIIIII, unaujua Mshaahara wake?
   
 18. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sisiemu is very sick already-kuiwazia kudumu milele katika utawala kuliishia kwenye vitabu vya mwenyekiti-vinginevyo Urusi tusingeona tunayoona-uchina-dola za kijamaa za ulaya mashariki -kwa hiyo tusiwavunje moyo wanaharakati ambao hawaangalii kikwete anaingia kupitia mlango upi???????-yale ya Ivory Coast ndiyo yameanza hivyo, kama ya mugabe yalivyoanza na kibaki alipoiga alijikuta wakenya wakichinjana kama kuku!!!!!!!!!!!!! kwani kwa Tanzania ni ajabu haya kutokea kutokea???????????????Nchi yo yote duniani utawala wa sheria ukishachakchuliwa kama Tanzania ya sasa, tarajia nguvu ya umma kuinuka!!!!!!It is only a matter of time!!!!!!!!!!!!and that time is not far from now!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. N

  Nonda JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Ni vizuri mumemsikia Mkapa hapo kwenye video na muda mfupi uliopita mulimsikia tena akiripotiwa kuwa anataka katiba mpya. Sasa ninyi ndio wa kufanya hitimisho ya nini kinaendelea, lakini la muhimu ni kuona vipi vyama ”mbadala” vinajitayarisha kuikabili kauli ya ”Ushindi ni lazima,mapinduzi daima”.

  Vita vya kuunda uongozi wa halmashauri inaendelea! na CCM wanafanya nini?
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,417
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Hakuna kinachoshindikana hapa duniani ni kuweka nia tu na dalili nzuri zimeshaanza kuonekana. Kule Mwanza JK alienda mara chungu nzima kumkingia kifua yule Waziri wake lakini bado Watanzania wakampiga chini na muda si mrefu ujao kama CCM haitabadilika ili kuweka maslahi ya Watanzania mbele badala ya mafisadi basi na wao watapigwa chini sehemu kubwa ya nchi yetu na CCM kubaki historia katika vitabu vyetu. Na wakishakosa madaraka hakuna atakayebaki ndani ya chama hicho wote watakimbilia vyama vingine.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...