Hakuna chama cha siasa kunachotaka serikali moja Tanzania?

Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Nimepitia sera za vyama vitatu vikuu hapa nchini, CUF, CDM and CCM sikuona hata chama kimoja kinachotaka kuwa na serikali moja...ya JMT

CUF-wao walianza tangu awali kwamba wakiingia madaraka wataanzisha serikali tatu..hayo ni kwa majibu ya mapendekezo mbalimbali za tume ..mfano nyalali, etc..

CDM- wao increasingly wameanza kuwafuata CUF kwa kudai serikali ya Tanganyika indirectly wanataka serikali tatu..ikiwemo serikali ya majimbo hapa niseme mimi napenda wazo la serikali ya majimbo ..nafikiri kutakuwa na ufanisi katika utendaji...

CCM- wao wamekazania serikali mbili na asiyetaka hilo nyerere alishasema aondoke kwenye chama walianza G55 wamenyamaza hawapo tena...

Swali: Iko wapi chama kinachotaka kuwa na serikali moja tu ya Tanzania..ambapo tutapunguza msururu wa viongozi (gharama), mgongano wa zanzibar ni nchi au si nchi, tanganyika irudi isirudi! tukasonga mbele kama nchi moja?

Iko chama kinachotetea serikali moja ya JMT?
 
HT

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,897
413
mi ioni logic ya kuwa na Muungano wa serikali lukuki. Tungegawa kanda zikawa majimbo chini ya serikali kuu moja. Yaani federal government na kila kanda ikawa some sort of 'state'.
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
mi ioni logic ya kuwa na Muungano wa serikali lukuki. Tungegawa kanda zikawa majimbo chini ya serikali kuu moja. Yaani federal government na kila kanda ikawa some sort of 'state'.

Natafuta chama cha siasa kitakachotamka hadharani kwamba inataka Tanzania kuwe na serikali moja si mbili wala tatu.
 
Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,688
470
wazazibar hawataki nchi yao ipotee kwa kuunda serikali mmoja labda chama kilazimishe na hiyo haiwezekani! wananchi wanataka serikali tatu, serikali ya ccm inataka serikali mbili. muungano hautadumu milele hata ukipunguza mambo ya muungano kwenye katiba yakabaki yale yale ya mwanzo bado watalalamika. Cha msingi ni kusikiliza wananchi wanataka nini?
 
Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Lazima tuwe realistic. Hapo mwanzo Tanganyika ilikuwa nchi peke yake na Zanzibar pia ilikuwa nchi peke yake. Kinachosumbua watu ni uoga, unafiki na ujinga(ignorance).
Hatuhitaji serikali moja, mbili wala tatu - kinachotakiwa ni kila nchi isimame kivyake turudi kuwa nchi jirani na Zanzibar iwe mwanachama mpya wa EAC.
Sielewi ni kwa nini watu wanang'ang'ania kuikana historia na kukumbatia ndoto za Alinacha. Tanganyika iwe nchi kamili na mfumo wake na serikali yake na Zanzibar nao waendelee kivyao, huku kung'ang'ana na serikali zisizoeleweka matokeo yake ndiyo hayo watu wanasherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi wanayoshindwa kuitaja.
Naamini kuwa umefika wakati watu waondokane na mawazo ya Nyerere yaliyofanya kazi miaka hiyo na sasa waende mbele na fikra mpya za kisasa. Hoja ya kulilia muungano ni kupoteza muda tu, hauna tija.
 
Chakunyuma

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
810
151
Kiukweli zanz hawatakubali serikali moja lakini hii ingepunguza sana gharama kwa kuwa haitawezekana basi hatuna budi tufikirie mfumo mzuri wa serikali zetu tatu, labda tuwe na raisi mmoja na serikali hizi mbili za Tanganyika na Zanzibar ziongozwe na mawaziri wakuu, waziri mkuu achaguliwe na Bunge au baraza la wawakilishi. Mawaziri sio lazima wawewabunge wanawezakuteuliwa nje ya bunge hii itaongeza ufanisi.
 
Laurel421

Member
Jun 28, 2011
23
0
moja si mbili wala tatu.
us.jpg
:crutch:
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,864
982
Jamani bado hii itakuja kwa maoni ya wananchi wenyewe na si vyama. Vyama visaidie kuwaleta wananchi karibu katika kufikisha mawazo yao.
Shida ya vyama vyetu vya siasa vingi hutunga sera na ilani zao bila kujua kwa hakika wananchi wanataka nini hasa, na badala yake mawazo ya viongozi ndio uchukua nafasi tena wakati mwingine kwa kuangalia maslahi yao ya baadae.
Binafsi naona kuna chaguzi mbili kati ya hizi na zote zinawezekana kama tu wananchi wanakubali.
1. Serikali moja
2. Serikali tatu
Vinginevyo hii ya sasa inatuingiza kwenye migogoro isiyokwisha maana viongozi wetu kwa mawazo yaliyojaa utashi wao wanatulazimisha kuingia kwenye serikali 2 na hii haitadumu milele hata kwa kutumia jeshi.
 
Losemo

Senior Member
Mar 30, 2010
183
30
Vyoote vilivyoumbwa na mwanadamu vina mwisho wake, Yatabaki yale yaliyopata baraka za Mungu mwenyewe. Nionavyo mimi hata hili la muungano litakwisha tu wala sio muda mrefu kutoka sasa
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Lazima tuwe realistic. Hapo mwanzo Tanganyika ilikuwa nchi peke yake na Zanzibar pia ilikuwa nchi peke yake. Kinachosumbua watu ni uoga, unafiki na ujinga(ignorance).
Hatuhitaji serikali moja, mbili wala tatu - kinachotakiwa ni kila nchi isimame kivyake turudi kuwa nchi jirani na Zanzibar iwe mwanachama mpya wa EAC.
Sielewi ni kwa nini watu wanang'ang'ania kuikana historia na kukumbatia ndoto za Alinacha. Tanganyika iwe nchi kamili na mfumo wake na serikali yake na Zanzibar nao waendelee kivyao, huku kung'ang'ana na serikali zisizoeleweka matokeo yake ndiyo hayo watu wanasherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi wanayoshindwa kuitaja.
Naamini kuwa umefika wakati watu waondokane na mawazo ya Nyerere yaliyofanya kazi miaka hiyo na sasa waende mbele na fikra mpya za kisasa. Hoja ya kulilia muungano ni kupoteza muda tu, hauna tija.

Kwanini watu wanashindwa au wanakuwa waoga kwa jambo ambalo ni rahisi tu...

Hivi hakuna chama jasiri litakalo sema tunataka kuwa na serikali moja ya Tanzania
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom