Hakuna cha Bata wala Kuku wa kienyeji

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
6,000
4,586
Wanasiasa mjitahidi na muwe wakweli, hoja zingine ndio zinazokuja kuwatia matatani baada wananchi wakianzakuona mlichi kiaidi hawakipati. Leo hii unamjaza mpiga kura ahadi ambzo hata wewe mwenyewe hujakaa chini kuona kama zinatekelezeka au la. Kitu kimoja lazima wananchi wajuwe kwamba hakuna Bata wa bure, hakuna serikali iyenye uwezo wa kukulisha Bata mpaka uridhike, nikimaanisha hakuna serikali itakulipa mshahara unaokuwezesha wewe mvuja jasho kukaa chini na kula Bata.

Kama kweli hawa wanasiasa wanasema unaweza kufanyakazi na kula Bata, muwaulize kama mishahara itakuwa ya kiwango gani?? Badala ya wanasiasa kuwahimiza watu wajiweke akiba itakayo wakimu siku za usoni wao na familia zao, unawaambia piga kazi halafu kula Bata.

Ina maana utakuwa chapa kazi ukimaliza tu, ile pesa uliopata inaingia mfuko mmoja na kutoka mfuko mweingine ikirudi serikalini kwa njia ya kodi ya kula Bata. Sidhani kama hawa wanasiasa wamepata ushauri wa taasisi zinazo jihusisha na biashara au hata kwa hao wafanyakazi wenyewe kama kweli hiyo ahadi inatekelezeka au la. Cha msingi kama kuna mtu anataka kula Bata sio lazima asubiri kupangiwa na mwanasiasa.

Kuna nchi nyingi walikuja na mifumo kama hii ya kazi na Bata leo hii ni majanga, nchi kama Greece, mpaka hivi karibuni ulikua unawza kustaafu ukuwa na umri wa miaka 45, baada ya hapo unakula Bata mpaka kufa kwako. Yamewashinda leo hii wako chini ya usimamizi wa nchi zingine za Ulaya. Spain, unaweza kupumzika mchana kwa masaa matatu tena ukalala kabisa kabla ya kurudi kazini, uchumi wao ulikuwa matatani muda mrefu sana. Portugal hivyo hivyo kama Spain, wananchi kazi kidogo wanapoza na Bata, leo hii hawajijuwi wako wapi kiuchumi mpaka wanasaidiwa na nchi walizo zitawala.

Miaka ya nyuma nchi kama Japan na South Korea zilikiwa na hali mbaya kutokana na vita ya dunia, sidhani kama walikuwa na muda wa kuonja huyo Bata, mpaka leo hii wanajituma kama kanakwamba bado wako kwenye hali mbaya. Kwa mtu mwenye malengo huwezi kumpangia lini afanye kazi na lini ale Bata, muulize Diamond lini alikaa chini akala Bata.
 
Basi kama ndio hivyo tumlaumu aliyeweka sheria ya kufanya kazi masaa nane kwa siku,,
 
Mm maneno yangu ni yale yale,
Twafaa kuwezesha vijana ambao ni taifa la kesho, hata kwa kaz ngumu za masaa 12 ili tuu wajikwamue na kujua uchungu wa hela
Tutapata mabilionea wapya bahaz kupitia hilo, kwa huwex kufundishwa kuwa tajir ni akili ya mtu tuu
Na tutapata wawekezaji binafsi wengii tuuu, na kuwapa fursa wengine

Na sio fedha nyingi kubebwa na huyu kiongozi wetu mpuuzi

Serikalin hera itaendelea kuliwa tuuu siku zote
Hakuna mshika hela asiye jilimbikizia hela yeye kama yeye
 
Kuna watu wanategemea kulishwa bata na wanaume wakina Membe na Zito na kwa ufinyu wa kufikiri wanashangilia kabisa.
Pigeni kazi acheni ujinga.
 
Aisee, inasikitisha sana, wakati wenzutu majirani zetu wanajitutumua usiku na mchana, hapa mtu anahubiri kula bata. Duh
 
Kuna watu wengi hawajaelewa hashtag ya #KaziNaBata, wanahisi kuwa serikali ndo itatoa bata, amini hata kipindi cha JK ilikuwa ni cha #KaziNaBata, yaani unafanya kazi na ukipata una uwezo wa kula bata bila masharti yoyote ila siku hizi hata bar zina mda maalum wa kufunguliwa eti mda mwingine watu wanapaswa kuwa kazini, je hawa wanaofanya kazi za usiku wale bata mda gani!?
 
Watakuelewa basi? Watu wanapenda kuishi maisha ya maigizo Sana.
Ndio hapo sasa, watu hawakawii kulaumu pale wanapogundua kama wanasiasa walikuwa wanatumia kwa maslahi yao binafsi.
 
Lumumba wamepanic
IMG_20181207_110728.jpeg
 
Kuna watu wengi hawajaelewa hashtag ya #KaziNaBata, wanahisi kuwa serikali ndo itatoa bata, amini hata kipindi cha JK ilikuwa ni cha #KaziNaBata, yaani unafanya kazi na ukipata una uwezo wa kula bata bila masharti yoyote ila siku hizi hata bar zina mda maalum wa kufunguliwa eti mda mwingine watu wanapaswa kuwa kazini, je hawa wanaofanya kazi za usiku wale bata mda gani!?
Kwani leo hii kuna mtu amekazwa kujiridhisha na bata wake anapotaka? Wakati wa JK rushwa ilikithiri na watu walikuwa hata hiyo kazi hawafanyi, anatumia cheo chake kupiga deal na halafu anakula bata. Sasa kama unadhani huo ndio mfano unafaa kuendelea kutumila Tanzania, basi tutakua na Safari mdefu kufika waliko fika nchi zilizo endelea.
 
Hatuongelei mtazamo wa kula bata kwa mazingira ya rushwa bali ni mtazamo wa “work hard, play hard “
Kwani leo hii kuna mtu amekazwa kujiridhisha na bata wake anapotaka? Wakati wa JK rushwa ilikithiri na watu walikuwa hata hiyo kazi hawafanyi, anatumia cheo chake kupiga deal na halafu anakula bata. Sasa kama unadhani huo ndio mfano unafaa kuendelea kutumila Tanzania, basi tutakua na Safari mdefu kufika waliko fika nchi zilizo endelea.
 
Wengine kazi na Bata ndy zetu
Kitambo sana
Nyie mnajifanya hapa kazi wakati hamna lolote ndy watu wa kuigiza

Ova
 
Wanasiasa mjitahidi na muwe wakweli, hoja zingine ndio zinazokuja kuwatia matatani baada wananchi wakianzakuona mlichi kiaidi hawakipati. Leo hii unamjaza mpiga kura ahadi ambzo hata wewe mwenyewe hujakaa chini kuona kama zinatekelezeka au la. Kitu kimoja lazima wananchi wajuwe kwamba hakuna Bata wa bure, hakuna serikali iyenye uwezo wa kukulisha Bata mpaka uridhike, nikimaanisha hakuna serikali itakulipa mshahara unaokuwezesha wewe mvuja jasho kukaa chini na kula Bata.

Kama kweli hawa wanasiasa wanasema unaweza kufanyakazi na kula Bata, muwaulize kama mishahara itakuwa ya kiwango gani?? Badala ya wanasiasa kuwahimiza watu wajiweke akiba itakayo wakimu siku za usoni wao na familia zao, unawaambia piga kazi halafu kula Bata.

Ina maana utakuwa chapa kazi ukimaliza tu, ile pesa uliopata inaingia mfuko mmoja na kutoka mfuko mweingine ikirudi serikalini kwa njia ya kodi ya kula Bata. Sidhani kama hawa wanasiasa wamepata ushauri wa taasisi zinazo jihusisha na biashara au hata kwa hao wafanyakazi wenyewe kama kweli hiyo ahadi inatekelezeka au la. Cha msingi kama kuna mtu anataka kula Bata sio lazima asubiri kupangiwa na mwanasiasa.

Kuna nchi nyingi walikuja na mifumo kama hii ya kazi na Bata leo hii ni majanga, nchi kama Greece, mpaka hivi karibuni ulikua unawza kustaafu ukuwa na umri wa miaka 45, baada ya hapo unakula Bata mpaka kufa kwako. Yamewashinda leo hii wako chini ya usimamizi wa nchi zingine za Ulaya. Spain, unaweza kupumzika mchana kwa masaa matatu tena ukalala kabisa kabla ya kurudi kazini, uchumi wao ulikuwa matatani muda mrefu sana. Portugal hivyo hivyo kama Spain, wananchi kazi kidogo wanapoza na Bata, leo hii hawajijuwi wako wapi kiuchumi mpaka wanasaidiwa na nchi walizo zitawala.

Miaka ya nyuma nchi kama Japan na South Korea zilikiwa na hali mbaya kutokana na vita ya dunia, sidhani kama walikuwa na muda wa kuonja huyo Bata, mpaka leo hii wanajituma kama kanakwamba bado wako kwenye hali mbaya. Kwa mtu mwenye malengo huwezi kumpangia lini afanye kazi na lini ale Bata, muulize Diamond lini alikaa chini akala Bata.
Heri kutawaliwa na shetani kuliko kutawaliwa na Jiwe! Piga kelele lakini Membe ndiye Rais 2020 wewe jiandae kulipwa kipato halali kwa kufanya kazi sio kukaa humu JF kwa upambe ukisubiri buku 7
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom