mpimamstaafu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,445
- 4,704
Kumekuwa na mjadala mpana katika mitandao ya kijamii juu ya Mh. Mbowe kugombea tena nafasi ya Uenyekiti wa Chadema Taifa.
Kumekuwa na shinikizo kutoka nje ya Chadema na baadhi ya Wabunge wa Chadema kina Mwambe, Komu na Kubenea kuwa Mh. Mbowe hafai.
Binafsi hao wa nje sioni kama ni tatizo kwani wanajua kuwa Mh Mbowe ni kiongozi imara akiondoka basi itakuwa rahisi kwao kuiua Chadema kwani mbinu mbalimbali wametumia lakini zimeshindikana.
Kwa hawa Wabunge naomba wanachama wa Chadema wawapuuze na ikibidi hata kwenye Chama wafukuzeni.
Hebu fikirieni viongozi wa Chadema zaidi ya 9 wako Mahakamani hao Wabunge hawajawahi hata siku moja kwenda Mahakamani kusikiliza kesi ya wenzio.
Mbunge Kubenea yupo hapa hapa Dar lakini anashindwa kwenda Mahakamani? Wana CHADEMA sidhani kama kuna kiongozi kwa sasa wa kuiongoza Chadema katika kipindi kigumu cha siasa za Tanzania zaidi ya Mh. Mbowe.
Kumbukeni misukosuko mingapi aliyopitia Mh. Mbowe katika utawala wa awamu hii? Mmeona Mh Lowassa kutikiswa kidogo tu Kakimbia Upinzani na kujiunga na CCM.
Wabunge kina Komu, Mwambe na Kubenea hata sero hawajawahi kulala, je wakitikiswa si siku hiyo hiyo watajiunga na CCM kama kina Ole milia Lowassa, Mwita na wengine?
Wana CHADEMA mpeni kura zenu Mh. Mbowe kwa uhai wa chama chenu.