Salaam,
Miaka yote tangu kupata uhuru, nchi za Africa, Tanzania ikiwemo, zimekuwa zikifanya siasa za kulaani nchi za magharibi zikiamini kuwa umasikini na matatizo ya nchi zao ni matokeo ya nchi za magharibi kuhodhi uchumi wa dunia.
Viongozi wa nchi na wanasiasa wa Africa mfano Julius Malema, Yoweri Museveni na hata Rais wetu wa Tanzania wamesikika wakilaani mbinu chafu zinazotumiwa na nchi tajiri zikiongozwa na USA kukwamisha maendeleo ya nchi zao.
Mimi naona njia wanayotumia kudai usawa siyo sahihi kwa sababu kinachotokea duniani ni ushindani wa kibiashara na uchumi na hivyo haiwezekani aliye juu kumuachia aliye chini kwa shinikizo na laana za kisiasa za majukwaani.
Uhuru wa bendera unaweza kupata kwa njia ya kulaani na kutoa matamko ya kisiasa majukwaani lakini sio ule wa kiuchumi na kibiashara.
Ili nchi masikini ziweze kunufaika na keki ya dunia tunapaswa kuwa na mikakati ya kimya kimya ya muda mrefu ambayo itahusisha kuwapatia elimu iliyo bora ya masuala ya kiuchumi na biashara ya dunia vijana wetu tukiwaandaa kuja kuwa washauri wa kiuchumi kwa mataifa yetu.
Pia mbinu nyingine yaweza kuwa kujifunza mbinu na mifumo inayotumiwa na mataifa ya magharibi kuendelea kuongoza dunia kwa undani zaidi.
Tunaweza kuchagua vijana wachache wakafanya utafiti wa sababu zinazowafanya wenzetu kuwa bora kila wakati na kila kitu kuanzia malezi ya watoto, uzalendo na uchapazi kazi.
LENGO LISIWE KUWAPITA WAZUNGU BALI WALAU NASI TUNUFAIKE NA KEKI YA DUNIA.
Wikiendi njema,
Sent using Jamii Forums mobile app