Hakuna anayetoa tathmini ya kina ya ufanisi wa Katiba ya sasa

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,242
Inashangaza sana kuona kuna kelele za wachumia tumbo wakidai katiba mpya.
Nawaita ni wachumia tumbo kwa kuwa hakuna common mwananchi anayedai katiba mpya bali ni viongozi wachache wenye ubinafsi.

Zaidi sijaona andiko lolote la maana na kina kutoka kwa maprofesa wetu wenye elimu za kuunga unga sana lililofanya tathmini ya nini kilichokuwa accomplished na katiba tuliyonayo.

Huwezi kwa upande mmoja ukasema nchi imeendelea au imepiga hatua halafu ukadharau katiba iliyopo...huo ni uhayawani.

Tumefanya chaguzi kadhaa kwa amani kwa katiba iliyopo hivi ni jicho la mchumia tumbo yupi lisilioona ubora wa Katiba iliyopo?

Hebu tuachane na fashion yaani kila akifanyacho mmarekani /mkenya basi na sisi tufanye ilimradi tuonekane tu...

let us stick to the plans of Founders of This nation...tuachane na blah blah.

Ukiwauliza mnataka kubadili nini kwenye katiba hutasikia cha maana zaidi ya issue ya uchaguzi.

#Siungi Mkono Katiba mpya na mijadala yake.
 
Anza na rasimu ya mzee Warioba na Katiba pendekezwa. Utagundua nini kinatakiwa kufanyika na ndiyo sababu hata Rais Samia ameunda kikosi kazi na anazungumza na Chadema. Kama bado huoni kitu sijui tusemeje tena
 
You’re out of touch. Katiba ni kwa ajili ya kuweka utawala bora nchini. Upungufu wa mfumo mzima wa utawala umejadiliwa mara nyingi katika majukwaa mbali mbali. Mambo ya kuzingatia kwenye katiba mpya yamependekezwa. Ndio maana kuna wadau wangependa katiba kamilike kwanza kabla ya tume huru ya uchaguzi.

Achana na maprofesa uchwara wa CCM. Just go back to real school. Katiba ni zaidi ya shughuli za kisiasa. Inagusa haki za msingi za watu wote katika sekta na fani zote. Ni mwananchi mjinga na siyejithamini atakayepuuza uwepo wa katiba madhubuti inayolinda maslahi yake dhidi ya watawala waonevu, mafisadi na waroho wa mali za watu. Watawala wanaofuja fedha za umma katika miradi ya maendeleo ya wananchi.
 
Kwamba ndugu Kikwete kuruhusu mchakato wa KATIBA mpya ktk uongozi wake ni WA CHADEMA yule? SSH kuruhusu mjadala naye pia ni MPINZANI?
 
Back
Top Bottom